Ilikuwa jumatatu tulivu sana katika mitaa ya
Arusha nchini Tanzania.
Siku iliyoanza kwa manyunyu ya mvua na radi
kidogo katika Jiji la Arusha. Kutokana na manyunyu hayo ya mvua, hali ya
ubaridi iliongezeka katika jiji la Arusha. Baridi iliyowafanya watu wengi
kuyakumbuka makoti yao na kuyatia mwilini.
Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa Twaha
Matiga, ilikuwa siku ambayo alikuwa anatimiza ndoto kubwa sana katika maisha
yake. Alichaguliwa kujiunga na chuo cha Udaktari wa Binadamu Jijini Arusha. Na
jumatatu hiyo ndio Ilikuwa siku yake ya kuripoti pale chuoni.
Twaha alikuwa na furaha sana. Hata ile hali ya
baridi haikumchukiza kabisa. Hakuwa anaihisi baridi kabisa. Mawazo yake yote
yalikuwa juu ya kutimiza ndoto hii kubwa sana katika maisha yake.
Wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza
walikusanyika katika ukumbi wa Chuo kwa ajili ya usajili. Walikuwa wanafunzi
wengi sana. Toka mikoa mbali mbali Tanzania, waliokwenda jijini Arusha kuisaka
elimu.
Baada ya maelezo ya awali ya utambulisho toka
uongozi wa chuo, pale ukumbini, sasa ulifika muda wa kupanga foleni ili usajili
uanze.
Kila mtu alikuwa anagombea nafasi ya kukaa mbele
ili angalau asisote sana kwenye foleni. Ilikuwa ni fujo sana !
Twaha alikaa kwenye kiti cha plastiki
akiangalia vurugu zile. Hakuwa na wasiwasi wowote, alijua maadamu amechaguliwa
kujiunga na Chuo kile, basi atasajiriwa tu.
Baada ya fujo kutulia, Twaha naye alienda
kujiunga kwenye foleni. Alikuwa mtu wa mwisho katika foleni ile ya usajiri.
Alikaa kwenye foleni huku akiwaza safari yake
ya elimu ilipotokea.
*********
Twaha aliwaza jinsi alivyosoma kwa shida shule
ya Sekondari Bagamoyo. Wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumsomesha. Hivyo
alipata shida sana kupata mtu mwenye moyo wa kumsomesha. Ilibidi mchana asome
sana, ili jioni afanye biashara ndogondogo ya kuuza karanga ili aweze kupata
hela ya mahitaji madogomadogo ya shule.
Baba yake Twaha alikuwa mvuvi . Lakini pesa
akizopata kutokana na kazi yake ya uvuvi zilitosha kuilisha familia yake tu.
Hii ilitokana na Mzee Mafiga kuwa na familia kubwa ya watoto saba.
Mama yake hakuwa na kazi zaidi ya kuchuuza
samaki mtaani, samaki wa mumewe. Inamaana ilikuwa sawa na kusema, baba na mama
yake Twaha walikuwa wanafanya biashara moja. Baba anavua samaki, tena kwa zana
dhaifu za uvuvi na mama anawauza kwa kuwachuuza mtaani.
Katika watoto wote saba wa baba na mama Twaha.
Twaha pekee ndio alikuwa anasoma shule. Wengine wote hawakutaka hata kusikia
neno shule. Hawakuona umuhimu wa shule. Waliona kaka yao akivyoteseka kwa ajiri
ya kusoma. Kupata sare, madaftari na michango midogomidogo ilikuwa shida.
Nduguze Twaha wote walikuwa wanashinda pwani wakijitafutia
ridhiki. Hata hivyo hawakuwa wanapata ridhiki ya kutosha.
Pamoja na shida zote hizo, Twaha alijitahidi
sana katika masomo ili afanikiwe, na kuisaidia familia yake iliyotopea katika
dimbwi la umaskini.
Ukweli alikuwa anafanya vizuri sana darasani.
Siku zote alikuwa anaamini elimu ndio mkombozi wake. Elimu ndio silaha pekee ya
kuishika kwa maskini kama yeye.
Na aliishika kweli elimu kweli kweli.
Mungu hamtupi mja wake ! Alifanikiwa kumaliza
kidato cha nne pale shule ya Sekondari Bagamoyo, na kufaulu vizuri sana.
Twaha alichaguliwa kujiunga na masomo ya
kidato cha tano katika shule ya Sekondari Ndanda.
Pamoja na kuijua thamani ya elimu, lakini
alipofaulu, Twaha pia aliitambua thamani ya pesa.
Alijua kwamba kumbe pesa na elimu vilikuwa
vinaenda sambamba.
Twaha hakuwa na pesa kabisa ya kuweza
kumpeleka shule.
Kwanza nauli kutoka Bagamoyo hadi Mtwara, mkoa
iliyopo shule hiyo Ilikuwa mtihani.
Hapo hujajumuisha pesa ya ada pamoja na vitu
vingine vya shule.
Ndoto yake ya kusoma Twaha ilikomea hapo. Alihisi
hawezi tena kuendelea na kusoma.
Hata wazazi wake walimwambia hivyo!
Baba yake alikuwa na jukumu zito la
kuhakikisha familia inakula, familia inatibiwa, familia inavaa pia . Hakuwa na
kipato cha kutosha kumuwezesha Twaha kwenda Mtwara kusoma.
Twaha alikuwa na akiba ya shilingi elfu kumi
iliyotokana na biashara zake za kuuza karanga jioni.
Kumbuka Twaha ndiye alikuwa mkubwa katika
familia hii. Alikuwa na ndugu sita nyuma yake, wote wakimwangalia yeye.
Aliamua kuzifuta kabisa fikra za kukata tamaa.
Aliamini kukata tamaa ni dhambi kubwa sana
katika maisha.
Aliyakumbuka vizuri maneno ya Mwalimu wake wa
Kiswahili wakati anasoma pale Bagamoyo sekondari.
"Usipende kukata tamaa ukiwa bado
unaishi, pambana hadi pumzi yako ya mwisho, hakuna linaloshindakana chini ya
jua".
Maneno hayo ya mwalimu wake yalijirudia katika
kichwa chake.
Aliapa lazima asome kwa njia yoyote ile.
Alikuwa anajiona mwenye wajibu wa baadae
kuwasaidia wazazi wake. Kusaidia ndugu zake pia.
"Lazima nisome !"
******
Alihisi maneno hayo anayesema polepole maneno
hayo. Haikuwa hivyo, yalisikiwa na mtu aliyekuwa mbele yake katika foleni ile
ndefu ya usajiri.
"Unaonekana una mawazo sana kaka"
Sauti nyororo ya dada aliyekuwa mbele ya Twaha ilipenya kwenye masikio yake.
"Hapana, sina mawazo dada"
"Mbona unaongea peke yako sasa ?"
Hakujibu.
"Naitwa Awatiph"
"Naitwa Twaha"
"Tunaweza kuonana baadae sehemu tofauti na
hapa?"
"Bila shaka"
Walibadilishana namba zao za simu palepale
kwenye foleni.
Zoezi la usajili lilichukuwa saa zipatazo
tano. Hatimaye Twaha akasajiliwa kama mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha
udaktari Arusha.
Kuwa Daktari ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi
sana. Alikuwa anajua masomo ya msingi ili awe Daktari.
Alikazana sana katika masomo hayo. Alijitahidi
sana katika somo la Kemia. Alijitahidi sana katika somo la Fizikia, na
alijitahidi pia katika somo la Baiolojia.
Alifanikiwa kupata A katika masomo hayo matatu
pale Bagamoyo Sekondari.
Alikuwa anapenda awe daktari ili aje kusaidia
wananchi maskini wanaoteseka kwa kukosa pesa za matibabu.
Siku zote alikuwa anajisemea mwenyewe.
"Mimi ndiye daktari pekee nitakayekuwa mkombozi kwa maskini wote wanaoteseka
kwa maradhi mbali mbali kwa kukosa pesa za matibabu"
Baada ya kusajiriwa, Twaha alienda katika
Hosteli za chuo kupumzika.
Alijilaza kitandani huku akikumbuka misukosuko
ya safari yake ya elimu. Alikumbuka alivyoteseka kipindi kile anatafuta hela ya
ada pamoja na ya matumizi ili aende kusoma shule ya Sekondari Ndanda.
Alienda kuomba serikalini lakini
hawakumuelewa. Alienda kuomba kwa Mbunge wake naye hakumuelewa . Hakupata hela
ya ada, hakupata hela ya nauli.
Bado alikuwa na elfu kumi ndani, chini ya mto wake
wa kulalia.
Ilikuwa bado wiki moja ili shule ifunguliwe.
Na Twaha akaanze kidato cha tano. Sasa ndoto yake ilikuwa inaanza kuyeyuka.
Hakuwa na njia ya mkato ya kumpeleka shule.
" Si ruhusa kukata tamaa katika maisha
ukiwa bado unaishi.."
Kauli ya mwalimu wake ilijirudia tena katika
kichwa chake.
"Sasa kwanini mimi naruhusu kukata tamaa
nikiwa bado ninaishi. Tena na afya tele.
Haiwezekani !
Lazima niende Mtwara nikasome
Usiku wa siku ile alipata wazo. Wazo ambalo
lilipewa baraka na kichwa chake.
Aliamua kwenda Mtwara kwa miguu! Alikuwa
ameamua hivyo!
Usiku ule ule aliweka vitu vyake vyote sawa.
Tayari kwa safari.
Asubuhi aliwaambia wazazi wake.
"Baba na Mama mimi leo naenda shule
"
"Umepata ada mwanangu ?" Mama yake
alimuuliza kwa sauti yake ya upole.
" Hapana"
"Sasa utaenda vipi shule ?" Baba
yake alimuuliiza nae.
" Kwa miguu"
"Miguu ?"
"Ndio wazazi wangu. Lazima niende Mtwara
kusoma. Na nimeamua kwenda Mtwara kwa miguu !"
Alisema akiwa anajiamini sana.
"Hivi Twaha unaujua umbali wa Mtwara
kutoka hapa ?"
"Siujui, lakini nitafika !"
"Ni mbali sana Mtwara, huwezi kwenda kwa
miguu Twaha !" Mama yake alimwambia kwa sauti yake ya upole.
"Nimeshafunga kila kitu changu. Ilibaki
kuwaaga nyinyi na ndugu zangu. Nakubali Mtwara ni mbali. Lakini bila elimu
safari yetu ya kuelekea kwenye mafanikio inazidi kuwa mbali. Bora niumie kwa
kutembea kwa miguu kuisaka elimu. Kuliko kuumia kwa umaskini huu uliotukuka!.
Umaskini umeweka kambi nyumbani kwetu. Hautaki
kutuacha hata kidogo. Na kitu pekee kinachoweza kuufukuza umaskini huu kipo
Mtwara.
Lazima niende Mtwara ! "
"Tufanye utaenda Mtwara kwa miguu. Je
hela ya ada utaitoa wapi?" Baba alimtupia swali zito.
Alifikiria kidogo akajibu.
"Nitajua huko huko Mtwara. Lakini lazima
nifike Mtwara kwanza. Mambo mengine yatajijibu huko huko."
Wazazi wake hawakuwa na jinsi. Walimruhusu
aende Mtwara !
Mama yake alikuwa analia machozi kwa kumuonea
huruma Twaha. Baba yake alikuwa anamhurumia pia.
Twaha alikuwa jasiri na imara katika msimamo
wake. Alidhamiria kwenda kusoma Mtwara kwa njia yoyote ile !
Baba aliwaita ndugu zake wote. Akawaambia juu
ya safari ya Twaha ya kwenda shuleni Mtwara, tena kwa miguu !
Ndugu zake wote walisikitika sana. Kila mmoja
aliingia ndani na kutoa akiba aliyojiwekea na kumpa.
Twaha alianza safari yake ya kutoka Bagamoyo
kwenda Mtwara akiwa na elfu ishirini tu.
Familia nzima aliiacha kwenye majonzi makuu.
Hakujali !
Hakusikitika !
Alidhamiria kwenda kusoma. Alidhamiria kweli
kwenda Mtwara kwa miguu !
*************
Twaha alikuwa katikati ya mawazo, simu yake
iliita.
Aliangalia kwenye kioo cha simu yake, alikuwa
Awatiph !
Aliipokea na kuanza kumsikiliza.
"Hallo"
"Mambo Twaha "
"Safi Awatiph, nambie"
"Nipo tu, nilikuwa na ombi moja Twaha
"
"Nakusikiliza"
"Naomba nikualike chakula cha usiku
leo"
"Haina shida, wapi ?"
"Tukutane Tengeru hoteli saa mbili
usiku"
"Sawa Awatiph "
"Sawa baadae"
Simu ikakatwa.
Alipoambiwa habari ya chakula cha usiku.
Alikumbuka kitu.
Alimkumbuka Aziza.
Mwanamke aliyesoma nae shule ya Msingi kule
Bagamoyo, na kuja kukutana nae kama bahati jijini Dar es salaam. Alikutana nae
kama bahati siku ile anatembea kutoka Bagamoyo kuelekea Mtwara kwa miguu.
Siku ile alitembea kweli kwa miguu kutoka
Bagamoyo hadi Dar es salaam. Alipofika Mwenge ndipo alipokutana na Aziza akiwa
anauza duka la simu pale Mwenge.
Ni Aziza ndiye aliyemuona na kumwita Twaha.
"Mambo Twaha?"
"Safi Aziza, za siku ?"
"Nzuri, vipi mbona na begi mkononi,
unaenda wapi ?"
"Mtwara "
"Mtwara utapata gari sahivi. Saa saba hii
Twaha ?"
"Naenda kwa miguu "
"Miguu ?!!!"
"Ndiyo Aziza"
Twaha alimsimulia kila kitu Aziza kuhusu
maisha yake.
Alivyofika mwisho aliukuta uso wa Aziza
hautamaniki.
Umerowa kwa machozi. Alimuonea huruma, na
kuahidi kumsaidia.
"Ngoja nikupe hela hii ukapumzike
Hotelini. Halafu kesho nitakusafirisha Mtwara. Na pesa ya ada nitakupa"
"Ahsante sana Aziza yaani sijui nikushukuru
vipi dada yangu."
"Jioni nikifunga hapa nitakupigia simu
tukapate chakula cha usiku sehemu"
"Sina simu Aziza"
Aziza alitoa simu moja iliyokuwa kwenye droo
pale dukani na kumkabidhi. Kwa siku ile alimuona Aziza kama Mungu mtu. Alienda
kutafuta chumba cha kupumzika. Kebby hoteli lilikuwa jibu lake. Akaingia ndani
na kukaa kitandani. Aliitoa ile simu aliyopewa na Aziza na kuichaji
Kebby hotel ilikuwa hoteli nzuri ya kisasa
yenye gharama nafuu iliyokuwa Kijitonyama. Ilikuwa na kila kitu ndani. Kwa Twaha
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala kwenye hoteli kubwa kama ile.
Siku ile ilikuwa ni moja ya siku aliyokuwa na
furaha sana. Ndoto yake ya kusoma ilikuwa inaenda kutimia. Tena inatimizwa na
mtu ambaye hakutegemea kabisa. Kweli usimdharau mtu yeyote duniani. Ingawa yeye
na Aziza hawakuwa marafiki kipindi wanasoma, lakini walikuwa wanaheshimiana
sana. Heshima ile bila shaka ilimpa moyo Aziza wa kumsaidia leo hii.
Saa moja kamili walikutana na Aziza pale Kebby
hoteli. Kulikuwa na mgahawa mzuri wa kisasa mbele ya hoteli ile. Walikaa na
kupata chakula cha usiku.
Wakati wanakula waliongea mambo mengi sana na
Aziza.
Aziza alimsimulia mambo mengi sana Twaha
kuhusu maisha yake. Kumbe kwa sasa Aziza alikuwa mke wa mtu. Alimsimulia mateso
aliyokuwa anayapata toka kwa mumewe.
Mumewe hakuwa anampa vizuri haki yake ya ndoa
.
" Sasa Twaha mimi nitakupa hela"
"Nitashukuru sana yaani dada yangu"
"Lakini kwa sharti moja tu"
"Nipo tayari kufuata sharti lolote
Aziza"
"Kweli ?"
"Kweli nakwambia"
"Nitakupa shilingi laki tano leo. Na
nitakuwa nakutumia matumizi kila utakapohitaji. Lakini nao……….. hii ni Love
& Action Novel, utakutana na mapenzi na mambo ya vita pia kama vile
unaangalia movie naamini utaenjoy sana mkasa huu mzito mtu wangu ..
Tukutane whatsapp +255 758 018 597
0 Comments
Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu
Emoji