Riwaya - Kakatika (18+)

“We binti njoo hapa,” nilikuwa napita kwenye mtaa mmoja kule Temeke, nikaitwa hivyo na mbaba mmoja aliyekaa kwenye benchi la kijana anayeosha viatu, wenyewe mnamuita ‘shuushaina’!
Kwa jinsi yule mbaba alivyonitumbulia macho, mwenyewe nikaogopa, nikajikuta nimemfuata…
“Shikamoo,” nilimwamkia huku nikiangalia pembeni kwa woga.
Mimi nilitarajia ataniambia amenifananisha na msichana anayemjua…
“Marhaba! Unaitwa nani wewe?”
“Rhoda.”
“Rhoda nani?” aliniuliza kwa ukali mpaka nikataka kukimbia. Moyoni nikasema ‘he! Huyu mbaba vipi? Mbona ana maswali kama polisi wa Kilwa Road?’
“Rhoda Musalanga,” nilimjibu.
“Unakaa wapi?”
“Kule juu Wailesi.”
“Kwa mzee nani?”
“Khaa! Kwa mzee nani kivipi? Si kwa baba yangu!” nilijipa ujasiri na kumjibu hivyo…
“Baba yako anaitwa nani?” kabla sijamjibu, nilimwona yule kijana msafisha viatu akiachia tabasamu. Niliamini amejua swali la yule mbaba ni la kijinga…
“Jamani, si nimekwambia naitwa Rhoda Musalanga, si ndiyo baba yangu mzazi…”
“Una simu?” aliniuliza swali jingine. Ina maana swali lake la awali alishalijua jibu lake.
“Kwani we unataka nini?”
“Nataka nini! Si nataka namba yako ya simu, hebu nitajie,” aliniambia huku akiwa amenitumbulia macho. Sijui ilikuaje, si nikajikuta nikizitoa namba zangu. Nilimtajia moja baada ya nyingine, kisha akatumbukiza mkono mfukoni na kutoa noti mbili za shilingi elfu kumi…
“Hizi utakunywa soda…umeolewa?”
“Akha! Mi sijaolewa,” nilimjibu kwa kukataa mpaka na mabega.
Kifupi mimi nilikuwa nimemaliza masomo ya sekondari na nina miaka 22 tu, lakini kutokana na umbo langu kuwa kubwa, wengi waliamini niko kwenye ndoa tayari.
Kwanza nilikuwa mrefu, si mnene sana lakini pia si mwembamba. Umbo langu ni namba nane! Katikati katikati kweli, juu kifuani palijaa sawasawa na katikati kwenda chini nilijengeka kama vile nilitengenezwa kwenye kiwanda cha magari cha Mjapan.
“Nitakuoa mimi… we nenda,” aliniambia yule mbaba huku akimwangalia msafisha viatu.
Kwangu lilikuwa tukio la ajabu sana. nilifika nyumbani na kukaa kimya, sikumwambia mama wala dada yangu, Agatha. Najua ningemwambia dada Agatha angeniambia nimpeleke na yeye kwa yule mbaba.
Nilikwenda Temeke kwenye maduka makubwa, nikanunua makufuli yangu matano kwa zile pesa, nikazidi kuwa wa kisasa zaidi. Maana mtaani naitwa Amber Rose kutokana na umbo langu lilivyo. Na vijana wengi walishatangaza dau mpaka la pesa nyingi ili wanipate lakini walikosa bahati hiyo, akaipata mmoja tu, Mwafyale ambaye ana duka la vipodozi Temeke Mwisho.
Sasa niliishi nikitegemea kupata ujumbe wowote kutoka kwa yule mbaba maana mimi sikuwa na namba yake.
Kweli bwana, saa saba juu ya alama mchana akanipigia simu, nikapokea haraka sana maana nilikuwa na shauku ya kutaka kujua nia yake kwangu…
“Hujambo?”
“Sijambo…shikamoo…”
“Unaamkia mara ngapi kwa siku?”
“Nilisahau, samahani sana…”
“Utakula jeuri yako…uko wapi?”
Nilitamani kwanza kujua maana ya mimi kula jeuri yangu kabla hata ya kumjibu nilipo. Lakini nikahisi ni msemo, nikamjibu swali lake…
“Mimi niko nyumbani…”
“Wapi?”
“Si nilikwambia jamani…huku mitaa ya Wailesi…”
“Utakula jeuri yako…njoo hapa mitaa ya Temeke Hospitali…mimi nakaa hapa,” alisema kwa sauti ya ukali iliyojaa amri…
“Kwani huyu mbaba ni nani? Mbona amri amri…mtu simjui hanijui halafu ananiamuru kama mwanaye, kwa nini lakini?” niliwaza moyoni, lakini nikashindwa kumuuliza…
“Nije kufanya nini sasa..?”
“We…utakula jeuri yako…unajifanya hujui siyo?”
“Mimi sijui!”
“Wewe njoo utajua kwa nini nimekuita.”
“Mkeo je?”
“Sina…”
“Mh! Wewe ulipo hapo huna mke kweli?”
“Nilimfukuza.”
“Kwa nini?”
“Haikuhusu…wewe njoo haraka.”
Nilijikuta nikimpa dakika kumi na tano tu kwamba, nitakuwa nimefika mitaa hiyo.
Niliingia bafuni kuoga chapuchapu kisha nikavaa. Tena kwa ndani nilivaa kufuli moja mpya. Nje nikapigilia suruali ya skin’taiti nyeusi na blauzi juu nyeupe, miguuni sendoz, nikaondoka zangu bila kumuaga mama wala dada.
Nilipofika mitaa ya hospitali nilimtwangia simu, haraka sana akapokea…
“Oya mi nipo hapa hospitali…”
“Njoo moja kwa moja mpaka kwenye kontena mbele hapa, utanikuta.”
Nilitembea kunyoosha njia mpaka kwenye kontena, nikamkuta amekaa na wenzake wawili wakinywa bia. Yeye alivaa pensi na fulana…
“Kaa hapa…wee mletee bia huyu yoyote lakini ya baridi,” alimwambia mhudumu.
Niseme ukweli, nakunywa pombe kwa hiyo agizo hilo kwangu halikuwa geni na aliyenifundisha kunywa pombe ni jamaa yangu, Mwafyale, mwenyewe nimezoea kumwita Mwana FA.
“Yoyote?” aliuliza mhudumu. Mhudumu mwenyewe ni jianajike f’lani. Ukimwangalia hivi ana sura ya kufumaniwafumaniwa tu…
“Kwani huuzi bia?” yule mbaba aliuliza…
“Sasa si nimekwambia lete yoyote lakini ya baridi…”
“Eti anti, nikupe bia gani?”
“Yoyote.”
Yule mhudumu aliondoka akicheka.
Baada ya kunywa bia moja, mbaba alinisimamisha na kuniambia…
“Twende huku la sivyo utakula jeuri yako.”
Jamani wewe…wapi sasa?”
“Hutaki?”
“Siyo kama sitaki…nataka kujua tunakwenda wapi?”
“Si kule…mimi si mtu mbaya kwako. Ningekuwa mbaya ningekupa pesa yangu? Twende.”
Maneno yake yalikuwa kama kumsukuma mlevi, kwani nilijikuta miguu ikikubali kwenda yenyewe bila kulazimishwa huku nikiwa najishangaa.
Tulikwenda kuingia kwenye nyumba moja kubwa sana. Ina vyumba huku na huku, katikati ni korido pana. Ilionekana kila chumba kilijitegemea. Kwa hiyo hakukuwa na chumba na sebule. Ilikuwa maalum kwa ajili ya kupanga tu.
Basi, yule mbaba aliingia kwenye chumba cha katikati kwa kufungua kufuli na funguo alizokuwa nazo.
“Karibu, pita,” aliniambia huku akinipitisha mlangoni, akaweka pazia la mlango vizuri kisha akaufunga kwa kitasa cha ndani…. Whatsapp kupata full +255 758 018 597  au pakua Kulaya Simulizi App kupitia hii link
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.swahili.simulizi&hl=en


Post a Comment

0 Comments