Mama
kwa haraka akaniziba mdomo wangu huku tukiwa tumejibanza kwenye migomba mingi
sana, iliyopo karibu kwenye kijumba chetu cha udongo huku tukimshuhudia baba
akipigwa kipigo na watu walio valia mavazi meusi huku wakiwa wamezificha sura
zao kwa vitambaa. Bariki kali na mvua kubwa inayo endelea kunyesha katika eneo
hili la kijiji chetu cha Umbwe hapa Moshi, ikamfanya mama azidi kunikumbatia
huku akilia kwa sauti ya chini chini sana. Machozi na hasira zikazidi
kunitawala, ila sina uwezo wa kufanya kitu chochote nikiwa bado ni mtoto mdogo
mwenye umri wa miaka sita.
“Wewe
si unajifanya mjanja kuwashawishi wakulima wezako kukataa mimi kuwekeza kwenye
hichi kijiji si ndio?”
Sauti
ya mwanaume aliye zungukwa na watu hawa wanao endelea kumtesa baba ilisikika
vizuri, japo mama alijitahidi kuniziba macho yangu nisishuhudie kitendo hicho
anacho fanyiwa baba yangu, ila nikazidi kujitahidi kuangalia ila mama aliigeuza
sura yangu pembeni na nikaendelea kunikumbatia. Niliendelea kusikia miguno ya
baba yangu na kilio chake cha maumivu.
“Sasa
utakufa kama shujaa mpuuzi, mpigeni hadi afe na mwili wake mukautupe shambani
kwake”
Sauti
ya mwaunaume huyo iliyoa maagizo hayo na kuwafanya watu hao kuendelea kumpiga
baba kwa magongo mazito. Kwa bahati mbaya ikapiga radi mwanga wake ukaangaza
kila eneo hili.
“Kuna
watu kule kwenye migomba”
Kijana
mmoja alizungumza huku akinyoosha mkono wake kwenye eneo hili tulilo jificha na
mama. Kwa haraka mama akanishika mkono wangu wa kuli na hapakuwa na budi tena
zaidi ya kuanza kukimbia.
“Lole
kimbia”
Mama
alizungumza huku akiniachia mkono na kuanza kuchechemea.
“Ndefo
mama”(Mama twende)
Nilizungumza
kwa lugha ya kichaga huku nikijaribu kumshika mkono mama ila mama kwa ishara
akaniomba nikimbie kwani watu hao wanazidi kutukaribia. Machozi ya yakazidi
kunimwagika usoni mwangu, kwani sina uwezo wa kupambana na wanaume hawa na wala
sina uwezo wa kumtetea mama yangu. Mama kwa ishara ya mkono akazidi
kunisisitizia niweze kukimbia ili kuyaokoa maisha yangu.
Nikakimbia
kwenye hii migomba mingi, huku nyuma nikaanza kusikia sauti ya mama yangu
akipiga mayowe ya kuomba msaada. Ila mvua na mingurumo hii ya radi na umbali
tulipo kutoka jirani mmoja hadi mwengine ni swala ambalo ni gumu sana kusikika.
Kila nilipo jaribu kusonga mbele, nikajikuta nikisita kabisa kuendelea na
safari hii. Nikaangaza angaza chini na kuona fimbo, nikaichukua na kuanza
kurudi eneo nilipo muacha mama yangu huku machozi yakinimwagika usoni mwangu na
hasira ikiwa imejaa kifuani mwangu.
Nikafika
katika eneo ambalo yupo mama yangu, nikawakuta vijana hawa sita wakimbaka kwa
nguvu, jambo lillo nifanya nianza kumchapa mmoja wao.
“Ametokea
wapi huyo mtoto”
Kijana
mmoja ambaye ndio yupo katikati ya mapaja ya mama alizungumza huku akiwa amevua
kitambaa kilicho kuwa kimeiziba sura yake.
“Mpigeni”
“Mkuu
ila huyu ni mtoto”
“Mtoto
mpigeni na mumuue”
“Ja….ma…..ni….musi….mp……”
Mama
alizungumza kwa shida sana kwani amepigwa kipigo kizito sana na kubwa juu.
“Muondoeni
hapa”
Kijana
huyo anaye endelea kumuingilia mama kinguvu alizungumza na vijana wake wawili
wakanishika na kunibebe juu juu. Nikajitahidi kwa nguvu zangu zote ili mradi
niweze kujitoa mikononi mwao na kwenda kumsaidia mama ila utoto wangu na kuto
kuwa na nguvu, ukawafanya vijana hawa kunihimili. Vijana hawa wakaendelea
kunibeba huku wakinitandika magofi mazito pamoja na ngumi katika kila sehemu ya
mwili wangu.
“Tumuue”
Kijana
mmoja alizungumza kwa ukali huku wakinibwaga chini kama mzigo wa kuni.
“Hapana
huyu ni mtoto mdogo sana, hatuna haja ya kumuua”
“Tumepewa
agizo na mkuu?”
“Ni
bora tumtupe huko kwenye korongo, akafie mtoni”
Niliweza
kuyasikia mazungumzo ya vijana hawa vizuri sana, ila uwezo wa kusimama sina kwa
maana wamenipiga sana ngumi na makofi kana kwamba wana mpiga mtu mzima mwenzao.
Wakanisukumia bondeni kwenye korongo kubwa na nikaanza kumbingirika huku
nikipia kelele za kuomba msaada, ila galfa nikahisi kishindo kikubwa kichwani
mwangu na taratibu macho yangu yakapoteza uwezo wa kuona na sikujua ni nini
kinacho endelea.
***
Nikaanza
kusikia sauti ya watu wawili wakizungumza huku mmoja akiwa ni mwanamke. Sauti
ninazisikia ila kile wanacho kizungumza kwangu ndio mtihadi kabisa kwani ni
lugha ambayo siifahamu. Nikafumbua macho yangua, taratibu ila ukungua mwingi
ulio yatawala macho yangu ukanifanya nisiweze kuona watu hao.
“Heii
boy”
Niliisikia
sauti ya kike ikizungumza pembeni yangu.
“Ameamka”
“Unajisikiaje
kijana?”
Watu
hawa waliendelea kuniuliza maswali ambayo sikuweza kuyajibu kwa maana siwaoni
vizuri.
“Unaweza
kuzungumza?”
Mwanamke
aliniuliza kwa sauti ya upole.
“Tumuache
apumzike kwa muda ndio tumulize maswali”
“Ila
ni kijana mzuri sana”
“Yaa
sijui ni kwa nini waswahili wanawanyanyasa watoto hivi”
Nikajaribu
kumtazama mwanaume huyu, taratibu nikaanza kuiona sura yake, ni mzee wa kizungu
mwenye mvi nyingi sana kichwani mwake. Nikamtazama mwanamke aliye simama
pembeni ya mzee huyu, naye ni bibi wa kizungu, ila hajazeeka sana kama huyu
mzee.
“Mtengenezee
supu nzuri ya kuku”
Mzee
huyu alizungumza, bibi huyo akambusu mumewe shavuni kisha wakatoka ndani hapa.
Mzee huyu akavuta stuli na kukaa pembeni ya hichi kitanda. Akaanza kunishika
shika mguu wangu wa kushoto, taratibu nikautazama mguu wangu na kujiona nikiwa
nimefungwa bandeji kwenye mguu mzima. Nikaanza kulia, kwa maumivu niliyo anza
kuyahisi mara tu ya kuuona mguu wangu.
“Hapana
kijana usilie”
“Nipo
wapi…...?”
Niliendelea
kulia huku nikijitahidi kukaa kitandanii. Mzee huyu akajitahidi na kunirudisha
na kulala. Maumivu ya kichwa nayo yakazidi kunichanganya. Mzee huyu akachukua
moja ya bomba la sindano lenye dawa na kunichoma mkononi mwangu. Taratibu
nikaanza kuhisi usingizi ulio nifanya nilale fofofo ndani ya muda mchache tu.
***
Baada
ya siku mbili nikapata nafuu kidogo hata ya kuka mwenyewe kitandani, mzee Klopp
na mke wake Bi Jane Klopp, kama walivyo jitambuisha jana, wakaniomba waweze
kuzungumza na mimi. Kwa haraka haraka katika kipindi hichi cha siku hizi mbili
nilizo kaa nao wamekuwa ni watu wa kunijali kwa kila jambo. Muda wao mwingi
wanautumia katika kunitazama na kujua hali yangu inaendeleaje.
“Unaitwa
nani?”
Bi
Jane Klopp aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Eheee?”
“Unaitwa
nani?”
Nikajaribu
kukumbuka jina langu, ila nikajikuta nikishindwa kulikumbuka kabisa.
“Je
unajua ni nini kimekukuta?”
Bi
Jane Klopp aliendelea kuniuliza kwa upole, ila nikashindwa kabisa kufahamu ni
kitu gania mbacho kimenipata.
“Hapana,
kwani nipo wapi?”
Niliuliza
kwa suati ya upole na unyonge.
“Upo
Arusha mjini”
“Nimefikaje
fikaje?”
Bibi
Jane Klop wakatazamana na mume wake huku wakionekana kujawa na mshangao sana.
“Okay,
siku chache zilizo pita tulikuwa Moshi, kwenye matembezi yetu ya kufanya
uchunguzi ulio tuleta huku nchini Tanzania, kwa bahati nzuri tuliweza kukuta
kwenye moja ya mto ukiwa umepoteza fahamu, ilikuwa ni alfajiri sana.”
Mzee
Klop alizungumza kwa upole huku akinitazama usoni mwangu.
“Tulipo
kuchunguza vizuri tukagundua kwamba upo hai, tukaona sio mbaya tukakusaidia kwa
maana bado ni mtoto mdogo sana”
“Asanteni”
“Usijali,
ni jukumu letu. Je unakumbuka kama una ndugu, au marafiki ambao tunaweza
kuwasiliana nao wakaja kukuchukua hapa?”
Nikatingisha
kichwa huku nikijitahidi kuvuta japo taswira ya mtu yoyote ninaye mfahamu
kwenye maisha yangu ila sikuweza kukumbuka. Kitu kilichopo hapa kichwani mwangu
ni hawa wazee wawili mbele yangu.
“Kutokana
hapa Tanzania tumebakisha muda mchache wa kukaa, basi tutafanya mpango wa
kuondoka na wewe na kurudi nchini Ujerumani yalipo makazi yetu sawa”
“Sawa”
“Na
kuanzia leo utaitwa Ethan Klopp, hilo ndio litakuwa ni jina lako”
“Ethan
Klopp?”
“Ndio
hilo ndio jina lako kuanzi hii leo”
Nikatabasamu
kidogo kwani ni jina zuri kwa upande wangu na wala sioni sababu ya kukataa
kulikataa kwa maana jina langu halisi silifahamu.
“Na
sisi tutakuwa ni wazazi wako, kwa maana tuna binti yetu mmoja tu yupo nchini
Ujerumani, na wewe utakuwa ni mtoto wetu wa pili sasa”
“Ninashukuru
sana”
Nikajikuta
furaha ikinitawala moyoni mwangu. Taratibu bibi Jane Klopp akanikumbatia kwa
nguvu, huku akitawaliwa na furaha.
Siku
zikazidi kusonga mbele huku hali yangu ikizidi kuimarika, matibabu anayo
nipatia bibi Jane Klopp na mume wake yananifanya nizidi kuwa imara. Wakaanza
kunifundisha vitu vingi, na wakazidi kushangazwa na uwezo wangu wa akili kwani
katika kipindi cha muda mchache kila wanacho nifundisha basi ninakielewa kwa
haraka na ni vigumu sana kuweza kukisahau. Wakaanza kunifundisha Kijerumani,
japo ni lugha ngumu kidogo ila nikajitahidi hivyo hivyo ndani ya mwezi mzima
nikawa tayari nipo vizuri kwenye lugha hiyo na hawa wakiniongelesha ninaweza
kuwaelewa na kuwajibu kiufasaha.
“Ethan
unajua wewe ni genius?”
Bibi
Jane Ethan aliniambia tukiwa jikoni nikimsaidia kuandaa chakula cha usiku.
“Genius
ndio nini?”
“Ni
mtu mwenye upeo mkubwa wa kiakili, tofauti na watu wengine”
“Mtu
akiwa hivyo ndio anaitwa Genius?”
“Ndio,
ninakuahidi, nitahakikisha kwamba tunakupatia elimu bora unakuwa mtu bora
kabisa hapa duniani”
“Nashukuru
sana mama”
Bibi
Ethan kama kawaida yake akainama kidogo na kunibusu kwenye paji langu la uso
ikiwa ni ishara ya upendo ambao amenizoesha kuanzia siku ya kwanza kuanza
kuishi nao.
“Ukiwa
mkubwa Ethan unapenda kuwa nani?”
“Mmmmmm……nahitaji
kuwa na nguvu?”
“Hahaaa…..hata
hapo mbona una nguvu. Au unataka kuwa na nguvu ya kisiasa, kiuchumi au
ushawishi katika jamii?”
“Yoyote
tu ila nahitaji kuwa na nguvu tu”
“Hupendi
kuwa dokta, au rubani?”
“Mmmmmmhhhh”
“Kweli?”
“Ndio
mama”
“Basi
kama nitaendelea kupewa maisha marefu basi nitahakikisha kwamba unakuwa na
nguvu mwanangu”
“Nashukuru
sana mama”
Tukaendelea
kuandaa chakula hichi cha usiku, hatukuchukua muda mrefu sana tukafanikiwa
kumaliza kupika, nikasaidana na bibi Klopp kutenga chakula mezani, baada ya
maandalizi hayo yote kunalizika nikaelekea chumbani kumuita baba ambaye ni mzee
Klopp.
“Ohooo
nina kuja sasa hivi?”
“Sawa
baba”
Nikaanza
kuelekea mlangoni, ila kabla sijafika mlangoni akaniita, nikageuka na
kumtazama, kwa ishara ya mkono akaniita na nikafika hadi kwenye kiti alicho kaa
huku akiwa ana andika andika vitu kwenye kipakato chake(laptop)
“Kuna
shule za primary, nilikuwa ninazitafuta hapa, nahitaji tukirudi Ujerumani uende
ukasome, je ni ipi kati ya hizi mbili ni ipi hapa unaipenda?”
Mzee
Klop alinonyesha majengo makubwa mawili ya shule zilizopo kwenye nchi ya
Ujerumani ambapo kila siku nina tamani siku zao za kuishi hapa nchini Tanzania
ziishe ili nirudi nao Ujerumani.
“Hii
hapa”
Nilizungumza
huku nikimuonyesha jengo moja zuri.
“Umeipenda
hii?”
“Ndio
baba”
“Sawa,
tena hizi ni shule za watoto wenye uelewa maalumu. Tumeweza kugundua kwamba una
uwezo huo”
“Nashukuru
baba”
Unyenyekevu
na utii ndio ngao yangu kubwa sana ya kuendelea kuishi na wazee hawa, malengo
yangu na nia yangu ni kuhakisha kwamba nina pata nguvu kubwa kwenye maisha
yangu, na nilazima yatime pale tu nitakapo kuwa mtu mzima. Tukatoka kwa pamoja
humu chumbani na kurudi sebleni, tukapata chakula cha usiku kwa pamoja kisha
tukasali ibada ya usiku kama ilivyo kuwa desturi waliyo jiwekea. Baada ya sala
wao wakaelekea chumbani kwao na mimi nikaelekea chumbani kwangu na kulala.
Baada
ya siku wiki tatu, kuisha, siku ya kuondoka nchi Tanzania ikawadia, kila hatua
zote za kiserikali za kuondoka na mimi nchini humu walizikamilisha, japo
sifahamu sana kuhusiana na mambo hayo. Tukapanda ndege ya shirika la Fast Jet
hadi jijini Dar es Saalam ikiwa ndio mara yangu ya kwanza kufika katika jiji
hili ambalo nilikuwa nikilisikia sikia tu kipindi cha nyuma kwamba ndio jiji
zuri sana hapa nchini Tanzania.
‘Lazima
nitawale hili jiji siku’
Nilijikuta
nikila kiapo moyoni mwangu huku nikitazama magorofa marefu, tukiwa njiani
tunaelekea katika hoteli ya karibu ili kupumzika kwa muda ili kesho asubuhi na
mapema tuweze kuondoka na ndege kuelekea nchini Ujerumani. Tukafika hotelini,
mzee Klopp na mkewe wakachukua chumba kimoja, huku na mimi wakinipangishia
chumba changu. Baada ya kupata chakula cha usiku, tukaelelea katika vyumba
vyetu ili kupumzika ili kesho alfajiri na mapema tuwe tumewasili katika uwanja
wa ndege. Shauku na hamu ya kwanza ya kupanda ndege, nimesha imaliza kwa
kupanda ndege kutoka Moshi hadi jijini hapa Dar es Salaam. Shauku yangu ya pili
ni kwenda nchini Ujerumani kuishi kabisa. Uzuri wa mataa katika magorofa mengi
ninayo yaona kwa mbali, ukanifanya muda wangu mwingi sana niutumie nikiwa
nimesimama dirishani hapa nikishangaa taa hizi.
‘Nilazima
uwe na nguvu ya kuawala hili jiji’
Niliisikia
sauti nzito akilini mwangu iliyo nistua kidogo na kunipa wasiwasi. Damu mwili
mzima ikaanza kunisisimka na vinyweleo vyangu vikaanza kusimama. Mapazia
yaliyopo pembeni yangu hapa dirishani yakaanza kupepea, jambo lililo zidi
kunifanya niwe na wasiwasi kwa maana madirisha ni ya vioo na yote yamefungwa
vizuri sana na hakuna nafasi ya upepo kuweza kuingia na kuyafanya mapazia haya
kutikisika.
‘Ethan…..Ethan…….Ethan……’
Niliisikia
sauti ya kiume ikiniita kwa mbali, nikajaribu kuangaza macho yangu ndani ya
chumba hichi ili niweze kuona ni nani anaye niita ndani ya hichi chumba ila
sikuweza kuona zaidi ya mapazia kuendelea kutingishika sana. Woga ukanijaa,
mwili mzima ukazidi kunitetemeka.
“ETHAN……..”
Sauti
hii nzito nikaisikia vizuri kwenye masikio yangu, taa zote ndani ya chumba
hichi zikazima na nikaona kivuli cha mtu chenye mwanga hafifu sana kikiwa
kimesimama kwenye moja ya ukuta wa humu chumbani huku kivuli hicho kikionesha
mtu huyo akiwa amevaa joho kubwa sana, ila haonekani kichwa ni kipi wala miguu
ni ipi jambo lilo nifanya niaguke chini mzima mzima huku nikitamani kupiga
kelele ila sauti yangu haikuweza kutoka.
“Usiogope,
mimi sio mbaya kwako”
Sauti
ya mwanaume huyu ikazidi kuniongelesha, jasho lililo tokana na joto kali
likazidi kuniandama.
“Najua
nini unacho kiwaza na kukifikiria. Nitakusaidia, kadri siku zitakavyo zidi
kwenda ndivyo kadri nitakavyo zidi kuwa rafiki yako na msaada wako kwako.
Usimuambie mtu wa aina yoyote habari hii umenielewa?”
Nikamjibu
kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba nimelewa.
“Endapo
utazungumza chochote kwa mtu yoyote basi mtu huyo nitamuua. Lala salama na
usiku mwema”
Mara
baada ya mwanaume huyo kuzungumza hivyo, taa zote zikawaka na kila kitu
kikarudi kwenye hali yake, hapakuwa na pazia hata moja ambalo liliweza
kutingishika. NIkasimama kwa haraka na kuanza kutembea hadi mlangoni ili
nikawaeleze Bi Jane Klopp na mumewe habari hizi, ila nilipo kumbuka kwamba endapo
nitamualeza yoyote atakufa, basi hamasa hiyo ya kuwaambia, ikaanza kutetea na
mwishowe nikajikuta nikirudi kitandani mwangu na kuaa. Kusema kweli katika siku
ambazo sikuwahi kulala ni hii ya leo, sauti ya mwanaume huyu ambaye sifahamu ni
nani ikazendelea kujirudia kwenye masikio yangu.
Nikastuka
baada ya kengele iliyo fungwa mlangoni humu kuanza kuita, nikatazama saa ya
ukutani nikaona ni majira ya saa kumi na moja kasoro alfajiri. Nikakumbuaka
kwamba jana usiku bibi Jane Klopp aliniahidi kwamba atakuja kuniamsha muda huu
ili nianze kuajiandaa kwa ajili ya safari kwa maana ndege yetu inaondoka saa
kumi na mbili asubuhi. Kengele ikaendelea kuminywa, taratibu nikashuka
kiyandani na kuanza kutembea hadi mlangoni, nikaufunga mlango nakweli nikamkuta
bibi Jane Klopp akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.
“Umeamkaje
Ethan?”
“Salama
mama, wewe je?”
Niliitikia
huku nikijifanya kama nina usingizi mwingi, ila kwa namna moja ama nyingine
sina usingizi wa aina yoyote zaidi ya woga wa tukioa ambalo nilikutano nalo
jana usiku.
“Tumeamka
salama, jiandae tuianze safari”
“Sawa
mama”
“Haya”
Bi
Jane Klopp akaondoka mlangoni kwangu, nikafunga mlango na moja kwa moja
nikalifwata sehemu begi langu la nguo lilipo, nikafungua zipo ya pembeni,
nikatoa mswaki wangu pamoja na dawa yake, kisha nikaelekea bafuni. Nikasafisha
kinywa changu, ndani ya muda mfupi nikiwa tayari nimesha maliza kukisafisha
kinywa hichi. Nikaoga haraka haraka kisha nikarudi chumbani, nikavaa nguo
nilizo kusudia kuzivaa katika safari hii, ambayo tayari hamu yake imerudi
kwenye mstari hata tukio lililo tokea jana usiku likaanza kunipotea kwenye upeo
wangu wa akili.
Nilipo
hakikisha kwamba nimemaliza kila kitu, nikamuomba Mungu kama nilivyo fundishwa
na Bi Jane Klopp, ili awe kunitangulia katika safari hii, kisha nilipo maliza
sala yangu, nikatoka chumbani humu huku nikilivuta begi langu. Kwa bahati nzuri
nikakutana na Bi Jane Klopp pamoja na mzee Klopp wakitoka kwenye chumba chao
huku nao wakiwa tayari wamesha jianda. Nikamsalimia mzee Klopp kwa heshima
zote, kisha tukaelekea nje ya hoteli hii na kumkuta yule dereva ambaye
alituleta jana hapa hotelini akiwa tayari amesha fika kama vile alivyo elezwa
na bi Jane Klopp aweze kuwahi asubuhi na mapema kwenye hotel hii.
Baada
ya dereva kuingiza mabegi yetu nyuma ya taksi yake hii, mimi na bi Jane Klop
tukaingia kwenye siti ya nyuma huku Mzee Klopp akipanda siti na kukaa siti ya
mbele pamoja na dereva.
“Ethan
mwanangu, unajisikiaje?”
Bi
Jane Klopp aliniuliza huku akiwa amenishika mkono wangu wa kulia huku akiminya
minya kiganja changu.
“Ndio
mama, nina furaha sana”
“Unakwenda
kuyaanza maisha mapya sasa Ethan”
“Kweli
baba ninakwenda kuanza maisha mapya”
“Ila
tutakuwa tunarudi Tanzania mara kadhaa, kuitembele hii nchi si unafahamu kwamba
hii ndio nchi yako”
“Ndio
mama”
“Hata
ikatokea kwamba tumekufa, ila Tambua uhalisia wako wewe ni upi, wapi umetoka na
tunaamini kwamba ipo siku utakutana tena na ndugu zako”
“Sawa
mama”
Swala
la ndugu zangu bado kwa upande wangu ni kitendawili, nina jaribu kuvuta
kumbukumbu za kumkumbuka japo hata mama yangu wa kunizaa ila sipati hata
taswira yake. Tukafika uwanja wa ndege, tukapitia hatua zote ambazo kama abiria
anatakiwa kupitia, muda wa abiria kuelekea kwenye ndege tunayo paswa kusafiri
nayo, ukawadia. Tukaingia kwenye ndege hiyo bibi Jane Klopp na mumewe wakaa
katika siti za mbili huku mim nikikaa siti ya pembeni yao, ila na abiria
mwengine ambaye ni mwana mama wa kiafrika. Nikamsalimia mwana mama huyu kwa
heshima sana, hadi mwenyewe akanishangaa. Akaitikia salamu yangu huku
akiwaametabasamu.
“Unaitwa
nani mtoto?”
“Ethan
Klopp”
“Anaa
mimi naitwa mama Lukas”
“Nashukuru
kukufahamu mama Lukas”
“Unasafiri
peke yako?”
“Hapana,
nipo na wazazi wangu, hao hapo”
Nikawaonyesha
Bi Jane Klopp na mume, ambao nao kwa furaha wakasalimiana na mama huyu.
“Kusema kweli nimetokea
kukupenda sana mtoto….. nyota ya mtoto inaanza kung’aa kabla
hajafika ujerumani… nini kitatokea … matamanio makubwa anayopitia …
Riwaya hii ina visa
vizito vya kimapenzi, vita, matukio ya mshangao….
Whatsapp - +255 758 018 597
KURASA ZAIDI YA 500 KWA 1000 TU
0 Comments
Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu
Emoji