Riwaya - Tamu ya Masu (utamu, chombezo, 18+)


Miezi miwili baadaye, Masumbuko, Solomon na wenzao wawili wakaamua kulivaa jiji la Dar es Salaam kwa minajili ya kutafuta maendeleo zaidi.

Waliipanda treni pamoja lakini Solomon na wale vijana wengine wawili waliteremkia Morogoro kinyemela bila ya kumtaarifu Masumbuko. Treni ilipoingia jijini Dar Es Salaam saa 6 mchana ndipo Masumbuko alipobaini kuwa wenzake walimtoroka.

Sasa akajikuta akikabiliana na mazingira magumu zaidi. Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia jijini Dar. Afanye nini?
“Mimi ni mwanamume,” alijiambia na kujipa ujasiri. Akawa tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

Kwa siku tatu mfululizo akawa akila mihogo ya kukaanga mitaani na wakati mwingine akijipatia mlo kwa akinamama lishe; wali, maharage na kushushia maji mengi katika kuongeza ujazo tumboni. Usiku ulipoingia alijichimbia katika majengo ambayo ujenzi wake haujakamilika na kutoka alfajiri ya siku inayofuata.

Hatimaye akaamua kuirudia ile kazi yake aliyoiacha kule Tabora. Katika siku hizo tatu alikuwa akishinda kwenye vijiwe vya kahawa na ni hapo aliposikia simulizi nyingi kuhusu jiji hilo. Na ndipo pia aliposikia kuwa kuna soko kubwa katika eneo la Kariakoo, soko ambalo vijana wengi huenda kufanya kazi za kubeba mizigo hapo.

Kwa kuwa aliishi katika jiji geni, na alihitaji kupata pesa ya kula na matumizi mengine, ikibidi hata kupata nauli ya kumrudisha Nzega, aliamua kulisaka hilo soko la Kariakoo.

Siku chache baadaye alikuwa akifanya vibarua vya kubeba mizigo kutwa nzima katika soko hilo.

Masumbuko akawa hapati hata muda wa kuoga wala kufua nguo. Akawa mchafu kupindukia. Sasa hakutofautiana na taahira. Lakini hakuacha kujishughulishsa na kazi hiyo ya kubeba mizigo . Aache, halafu ale nini?

Wiki moja baada ya kuanza kazi hiyo, siku moja kitu kama saa 5 hivi, alimwona mama mmoja mnene aliyekuwa na mizigo iliyomwelemea.

Alikuwa bado yu mwanamke mbichi japo unene ulimvamia kwa nguvu. Kwa mtazamo wa harakaharaka alimwona mwanamke huyo kama awezaye kumkomboa na dhiki iliyomzunguka.

Akamsogelea kwa mwendo wa taratibu. Kisha “shikamoo” ikamtoka.
Mwanamke yule aligeuka na kumtazama. Akajiwa na huruma pale macho yao yalipokutana. Aliibaini dhiki iliyogubika katika maisha ya Masumbuko kupitia katika macho yake. Naam, macho ya Masumbuko hayakuhitaji maelezo ya ziada katika kumtambulisha kuwa yuko katika lindi la matatizo.

“Marahaba, hujambo?”

“Sijambo, mama yangu,” Masumbuko alijibu. Kisha, papohapo akaongeza, “Samahani, mama, naomba nikusaidie mizigo yako. Mimi siyo kibaka. Nina kama wiki moja na nusu tangu niingie hapa mjini. Kwetu ni Nzega. Kwa kweli nina maisha ya taabu sana tangu nifike hapa.”

Mama yule alitua mizigo chini kisha akamkazia zaidi macho Masumbuko. Akatikisa kichwa kwa huruma.

Alimwona kuwa ni kijana ambaye amejaaliwa sura nzuri na umbo zuri, lakini furaha ambayo ilitakiwa kujidhihirisha katika uso wake ilifichwa katika macho yale yenye kila aina ya majonzi na dhiki ya maisha. Hiyo ilikuwa bayana kufuatia ngozi yake iliyokauka, nywele chafu na timtim sanjari na mavazi chakavu yaliyomsitiri maungoni.

Akamwambia, “Beba mfuko huo twende kwenye gari lilee...” alimwonyesha kwa kidole.

Masumbuko alifanya kama alivyoelekezwa. Akavibeba vifurushi vile na kuviingiza katika buti la gari, Mercedes Benz jeusi. Kisha akaambiwa aingie garini. Takriban saa nzima baadaye walikuwa Bunju 'A', nje ya jumba kubwa la kifahari.

Eneo hilo la Bunju 'A' halikuwa na nyumba nyingi, lakini hizo chache zilizokuwapo hazikuwa za kawaida. Baadhi zilikuwa ndogo na baadhi zilikuwa kubwa, lakini zote zilivutia.

Kwa vyovyote vile, kwa Mtanzania wa kawaida, ambaye huishi kwa kupata mlo mmoja kwa siku, akiziona nyumba hizo hataamini kuwa ni za Watanzania wenzake, na kama ataambiwa kuwa ni za Watanzania basi haitamwingia akilini kuwa pato walilotumia kwa kuzijenga nyumba hizo ni la halali.

Miongoni mwa nyumba hizo ni jumba hili ambalo gari hili limeegeshwa nje yake, na Masumbuko kukaribishwa ndani.

Naam, kwa mara ya kwanza Masumbuko akajikuta ndani ya sebule ambayo hajapata kuiona tangu azaliwe. Masofa makubwa yenye umbo la kobe, meza na viti vinavyoendeshwa kwa mitambo maalumu, televisheni kubwa iliyojengewa eneo maalum ukutani, na zulia lipumualo ni baadhi tu ya samani zilizomshangaza.

“Karibu, karibu ujisikie kama uko kwenu...umesema kwenu ni wapi vile?” mama yule alimtazama usoni huku akiachia tabasamu la mbali.

“Nzega.”

“Yeah, Nzega. Basi ujione kama uko Nzega, Unyamwezini.”

“Asante, mama,” Masumbuko aliitika huku bado kasimama. Alionekana bado akiendelea kuustaajabia umaridadi wa sebule ile.

“Keti tu hapo sofani,” yule mama alimwambia. “ Mbona unasitasita? Keti wala usihofu.”

Masumbuko aliketi. Yule mama naye akaketi katika sofa jingine.

“Mimi naitwa Chausiku. Na...” akasita kidogo kisha akaita kwa sauti kali, “Mwanahawa!”

“Bee!”

“Njoo!”

Muda mfupi baadaye binti mmoja akaingia, akamtupia macho kidogo Masumbuko kisha akayahamishia kwa Chausiku.

“Na huyu ni Mwanahawa,” Chausiku aliendelea huku akimtazama Masumbuko. “Anaitwa Mwanahawa. Ni mdogo wangu, baba mmoja, mama mmoja.”

Masumbuko aliitika kwa kutikisa kichwa huku akimtazama Mwanahawa. Huyu Mwanahawa alifanana sana na Chausiku. Lakini kufanana huko kulikuwa ni kwa sura tu, kwa maumbile walitofautiana sana.

Chausiku alikuwa ni mnene, tipwatipwa wakati Mwanahawa alikuwa na mwili mdogo lakini katanuka mapajani na kulitengeneza umbo la 'nane.' Akilini mwa Masumbuko, Mwanahawa alivutia zaidi na hata angestahili kushiriki kwenye kinyang'anyiro chochote cha ulimbwende.

Hata hivyo hakupata muda wa kumtazama zaidi Mwanahawa, mara Chausiku akamuuliza, “Na wewe jina lako ni nani?”

“Masumbuko.”

“Masumbuko?” Chausiku alimuuliza, akionekana kutomwamini.

“Ndiyo, Masumbuko.”
“Ok,” Chausiku aliitika huku akitikisa kichwa na papohapo akamgeukia Mwanahawa. “Mwanahawa, huyu ni, mfanyakazi wetu mpya. Atakuwa akiwalisha ng'ombe...” akasita na kumtazama Masumbuko. “ Ulishawahi kuchunga ng'ombe?”

“Ndiyo. Nzega kuna ng'ombe wengi. Nimeshachunga ng'ombe, mbuzi na hata kondoo.”

“Basi hiyo nd'o kazi ninayoweza kukupa. Utaiweza?”

“Ndiyo, mama.”
instagram @kulayasimulizi
“Ok, Mwanahawa kamwonyeshe chumba chake cha kulala. Kisha umpeleke bafuni akaoge na umpe nguo nyingine. Hizi alizovaa zichomwe moto.”

“Sawa dada,” Mwanahawa alijibu kwa kunyenyekea.

“Halafu, najua ana njaa. Mtayarishie chochote. Mwenyewe unajua utakachomwandalia. Kila kitu kipo.”

“Sawa, dada.”

Chausiku akamrudia tena Masumbuko. “Wewe pumzika. Lakini ningependa ujue tu kuwa hapa ni kwa nani. Ni kwa Waziri wa Misosi na Maraha. Anaitwa Kisu Makalikuwili. Unamfahamu?”

“Ni'shamsikia redioni akitangazwa,” Masumbuko alisema huku akiyaepuka macho ya Chausiku aliyekuwa akimtazama sawia.

“Basi hapa nd'o kwake,” Chausiku alikazia. “Uko nyumbani kwa waziri! Lakini kwa sasa hayupo. Yuko kwenye mkutano nje ya nchi. Nitamtaarifu kwa simu juu ya ajira yako. Na kwa kuwa umetoka mikoani, najua hatakuwa na kipingamizi chochote. Hawapendi vijana waliokulia hapa Dar na kulizoea jiji. Nakuomba tu ufanye kazi kwa bidii, na uwe na tabia njema. Ukiwa na tabia mbaya atanilaumu mimi. Umesikia?”

“Ndiyo, mama.”

“Haya, tutaonana jioni.”

Akatoka huku mwili wake ukiendelea kutikisika kwa namna ya kipekee, na kuwa kama aliyeamua kuutikisa makusudi kwa madhumuni aliyoyajua mwenyewe; Pwata...! pwata...! pwata....!

Muda mfupi baadaye masikio ya Masumbuko na Mwanahawa yalinasa ngurumo ya Mercedes Benz ikilalamika nje ya geti.

**********

MWANAHAWA alifanya kama alivyoagizwa. Kwanza alimwonyesha Masumbuko chumba cha kulala. Chumbani humo kulikuwa na kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita, sofa moja dogo, televisheni ndogo, kabati kubwa la nguo na vikorokoro vingine vilivyoongeza unadhifu wa chumba hicho.

Baada ya hapo alimwonyesha bafu ili akaoge. Bafu lenyewe lilikuwa ni chumba tu kisichokuwa na kitu chochote. Mtu ilibidi uminye kidude fulani ukutani, na hapo sinki kubwa lingetokea ardhini. Baada ya shughuli zako zote, unakanyaga kidude kingine sakafuni, sinki litazama polepole na kupotea machoni pako.

Kuzijua kanuni hizo kulihitaji kufundishwa. Masumbuko asingeweza kuzijua kanuni hizo; alifundishwa na Mwanahawa.

Baada ya kuoga alivaa nguo nyingine alizopewa na Mwanahawa kisha akaenda sebuleni ambako alipata kifungua kinywa; maini ya kukaanga, maziwa moto na mayai ya 'macho ya ng'ombe.'Wakati akiendelea kupata stafutahi hiyo, Mwanahawa alikuwa chumbani kwake ambako alibadili mavazi na kurejea kwa Masumbuko.
instagram @kulayasimulizi
Awali alikuwa amevaa gauni zito la kitambaa kilichoshonwa kwa namna isiyovutia. Lilikuwa ni gauni mahsusi kwa shughuli za nyumbani.
Sasa alibadilika. Alikuwa amevaa kijipensi kifupi na blauzi yenye matundu madogomadogo. Vititi vyake vichanga vilituna kwa kiburi kifuani kama vile vinamdhihaki yeyote yule avitazamaye.,

MAMA mwenye nyumba, Chausiku, mke wa Waziri wa Misosi na Maraha Kisu Makalikuwili, alirejea saa 3:45 usiku. Masumbuko akiwa chumbani alisikia geti likifunguliwa ngurumo ya gari ikivuma kwa nguvu. Yeye akaendelea kutulia tu chumbani humo. Nusu saa baadaye akasikia mlango wa chumba alicholala ukigongwa.

Akainuka na kwenda kufungua. Akashangaa pindi alipofungua na kumwona Chausiku mlangoni. Na si kwamba alishangazwa tu kwa kumwona Chausiku mlangoni, bali pia ni jinsi alivyokuwa. Chausiku alikuwa amejifunga kanga moja tu kutoka kifuani! Mwili wake teketeke, uliong'ara, ulikuwa umepuliziwa manukato yaliyovutia, yakajaa chumbani humo.

Wakati Masumbuko akiwa bado amepigwa butwaa, Chausiku alipitiliza moja kwa moja kitandani. Akajipweteka kivivuvivu, tabasamu likichanua usoni pake. Kisha akasema, “Sasa njoo. Funga mlango kwa komeo uje tuongee.”

Masumbuko alitii. Lakini badala ya kumfuata mwajiri wake pale kitandani, yeye aliketi sofani.

“Unakaa wapi huko?” Chausiku aliuliza kwa ukali wa kuigiza. Haikuwa dhahiri kuwa alifoka kutoka moyoni. Akaongeza, “Nimesema njoo hapa tuongee. Hapo ndio hapa?”

Sasa Masumbuko akalihama lile sofa na kumfuata mwajiri wake pale kitandani, kisha mama mwenye nyumba mnene mwenye hips pana, na mwenye mwanya akaanza kum…… jimama hili lilimfanya nini mvulana huyu? Whatsapp +255 758 018 597

Post a Comment

0 Comments