Limbwata (Riwaya) - Utamu 18 +Bebi, bado natafuta mbona utaenjoy sana tu nakupenda toa mawazo yako hayo, "Nalijua hilo lakini mi nina wivu juu yako, na hata kazi yako sijaipenda huyo mwanamke anaekurudisha kila siku kwa gari na kwanini umuambie mimi dada yako, yaani naumia sana mume wangu wa kunifanyia hivi kweli kila kitu umesahau""Kwani nini kinachoharibika? mimi nafanya hivi ili tuwe na maisha mazuri, nimeshakuambia niamini hutaki aaa mi nawahi kibaruani bwana" aliongea kijana huyo aliefahamika kwa jina la Saidi na kumuacha mpenzi wake akiwa na sitofahamu kichwani mwake. Mrembo huyo aliefahamika kwa jina Maimuna alijiinua kiunyonge akufurahia hata penzi lake kwa Saidi, Saidi nae akumpa huduma zinazostahiki kama mkewe. Umri wake unajitosheleza kuwa na watu wenye pesa lakini alibaki kwa Saidi wake, na Saidi aliishi na Maimuna baada ya kumpa mimba, tena walikuwa kidato cha 4, Maimuna shule aliacha hata Saidi aliacha nae na penzi lao liliwashangaza wengi ndipo wazazi wa mamuna waipokuja juu mno ikamlazimu Maimuna ampeleke Saidi nyumbani kwao. Na Saidi yeye alikuwa hana wazazi hivyo alikuwa akiishi na uncle wake, wazazi wa Maimuna walimwangalia ninyi yao na kumtazama Saidi wakaona wote ni watoto na wameamua kuishi wawili basi wazazi walipitisha swala hilo tena awakumtoza Saidi hata senti wazazi walitaka aishi na binti yao vizuri ndipo Saidi amebeba majukumu mazito, aliangaikia kibarua akapata. Alipiga kazi huku akiakikisha Maimuna anaishi vizuri na hasa mwanae alie tumboni. Siku zilisogea wawili hao wakiishi pamoja ndipo siku moja mkewe alizidiwa na kwakuwa Saidi pesa zilikuepo akiba ndipo akaaamua kukodi taxi na kumpeleka hospitali, alisubili majibu lakini daktari majibu aliyompa yalifanya asikitike. Mkewe Maimuna amejifungua lakini mtoto kafariki Saidi alitamani aitwe baba akiwa na miaka 21 tu lakini haikuwa hivyo, na tangu tukio hilo Saidi upendo ulipungua kwa mkewe na akaja kupata kazi ya shamba boy kwenye Nyumba ya kitajiri, nyumba hiyo ilikuwa ya familia ya watu wanne yaani baba, mama, kijana wao wa kiume na binti yao wa kike. Saidi alipewa jukumu la kumchunga binti huyo aliefahamika kwa jina Natasha. Ilifika wakati Natasha alimzoea Saidi na akawa anampeleka kwa gari mpaka nyumbani kabisaa na kitu hicho kilimkera sana Maimuna, alijua tu anaibiwa penzi lake lakini Saidi ni Wa kujitetea siku zote, Saidi alimuacha mkewe akilalama na kuondoka zake kazini, alifika na kuingia ndani na kumkuta Natasha yuko bize na mambo yake. Natasha alipotupa macho alimuona Saidi aliacha mambo yake na kumkimbilia, alipomfikia alimkumbatia"vipi Saidi wangu""poa" alijibu jibu la mkato na kutoa mikono ya Natasha kiunoni kwake"acha bwana Natasha utaniaharibia kazi mi si nipo""mi sitaki bwana, mi nataka uje kukaa hapa kwetu we uwoni aibu kukaa na dada yako nyumba moja""hayo achana nayo yule sister wangu hivyo yaani""Ok sasa mbona anaonyesha ana wivu juu yako utafikiri mtu wake kumbe! mh""achana nae ni sister wangu tu" aliongea hayo Saidi akionyesha dhahiri usaliti kwa mkewe, muda ulishaenda Natasha alitoa kiasi cha pesa na kumkabidhi, kisha akamsindikiza tena kwa gari. Natasha alimpeleka Saidi kwake, walipofika huko Saidi alishuka kwenye gari na kumsihi Natasha asishuke lakini Natasha hakuwa muelewa Saidi aliingia ndani na kumkuta Maimuna kajilaza zake sakafuni, Saidi alimstua mkewe kwa kumpiga miguuni"oh mume wangu huyo vp huko""Safi tu mbona umelala unaumwa""Hapana nimechoka tu mume wangu, basi ngoja nikuandalie chakula mume wangu""Mh mi sio mlaji kiukweli nisikuongopee mke wangu mi nishakula huko nilipotoka si unajua kazi yangu hii""Mimi nimepika chakula kingi lakini mwenzangu umeshiba? lakini mbona umebadilika laazizi""Mke wangu wivu wako umepitiliza sasa too much sasa, mimi siku hizi nitakuwa nikilala huko huko maana aaa""Sasa kazi gani hiyo unajua fika kuwa mimi ni mkeo lakini hujali hilo, huonyeshi mapenzi yoyote sawa tu""aa ushaanza yani sina raha nawe kwanza kuna mgeni wangu nahitaji nimsindikize maana nimemueka kweli nje" aliongea hayo Saidi na punde tu Natasha aliingia ndani na kumshika Saidi mkono"Umeshasahau kama umeniacha nje.. Whatsapp +255 758 018 597.
Hakikisha umefollow Page yetu Mpya ya Instagram kwa kubofya Link hapa chini.Tunahitaji wewe ndio uffolow kwakuwa ni member wa swahilisimulizi.com
https://www.instagram.com/swahilisimulizi/ Full story whatsapp +255 758 018 597

Post a Comment

0 Comments