Uchungu wa Utamu (Riwaya) - 18+

Haikuwa rahisi kuamini kuwa moja ya kitu alichokifuata Gosbert katika chuo kikuu kilicho makao makuu ya nchi na serikali na chuo kinachobeba jina la mkoa maarufu unaosifika kwa uzalishaji wa zao litengezalo divai na mvinyo, ilikuwa kusomea digrii ya kwanza ya taaluma ya elimu na nyongeza ya digrii ya pili katika uhusiano na mapenzi. Hakika Gosbert aliwika kama jogoo aliyekuwa katika kipindi cha kubarehe kwa kuwasumbua kina dada katika chuo hicho. Hakuna sketi iliyokatisha mbele yake ikiwa na ubora asitake kujua ndani ilibeba kitu gani. Hata katika makundi ya mijadala ya masomo ya usiku watu walimwogopa kwa kazi yake ya urijali wa jogoo kuwika na kupanda mtungi. Hakika kwa tabia aliyoionyesha hapo chuoni wanachuo wenzake walimpachika jina la Dokta Love almaarufu kama Mr. Lover boy. Jina hilo lilisadifu uhalisia wa tabia yake kwani aliwafunua sketi mabinti wadogo hata wanawake walio umri sawa na mama yake. Hakika Gosbert alisifika kama shujaa maalum aliyemfano wa jogoo kwa kuwika katika vifua vya wanawake. Gosbert alikuwa amekwishaharibu katika block B namba 98 kwa kuonja utamu wa kila binti na mwanamke aliyekuwemo ndani chumba hicho. Tabia ya kuwika na kusimama juu ya vifua vya kina dada iliwakera na kuamua kumshikisha adabu kijana huyo wa bush aliyeuvamia mji kwa staili ya pekee ya kuutafuta utamu wa mapenzi na ladha ya kupendwa katika moyo wake. Christina aliinua simu yake na kubonyeza namba fulani kisha akaweka sikioni na kuanza kusikia simu ikiita upande wa pili na kupokelewa,

"Haloo bebi wangu mambo vipi!Nimekumisije baba?Njoo basi room jamani"

"Uko block gani na chumba namba ngapi"

"Niko block B chumba namba 98. Njoo mpenzi wangu jamani. Uniletee na chipsi mayai sawa baba!"

"Hilo wala usijali mama!Nitakuwa hapo baada ya dakika kama ishirini hivi. Uko na kina nani. ?"

"Niko mwenyewe baby, wenzangu wametoka, wamekwenda town kula bata na wapenzi wao. Njoo ufaidi penzi tamu baba. . .

"Sawa mama nitakuja muda si mrefu, nitegemee baada ya sekunde kadhaa, nitakuwa hapo. "

Simu ilikatwa na kuwekwa mezani huku vicheko vikitawala katika chumba hicho. Kama wasemavyo waswahili kipya hakinyemi ingawa kidonda tena upya wa. . . . . . . . . . . Gosbert aliiona nafasi hiyo adimu kwake kama golden chance ya kufaidi penzi jipya toka kwa first year na hakutaka kuipoteza kwa siku hiyo. Masikini Gosbert kama angelijua mtego ulio mbele yake asingethubutu kuinua miguu yake na kuelekea katika block aliloelekezwa.  Mtego ulioandaliwa ulikuwa na lengo la kumnasa paka anayedokoa mboga jikoni na kumbabua kwa moto mkali. Dakika chache na sekunde kadhaa baadae Gosbert alionekana akikwea ngazi kuelekea floor ya nne chumba namba 98. Gosbert alikuwa akitupa macho juu ya namba za milango iliyokuwa katika floor hiyo. Mara macho yake yalitua katika mlango ulioandikwa namba 98. Aliusogelea mlango huo kisha akaugonga ngo!ngoo!

"Hodi humu ndani!Hodi wenyewe!"

Gosbert alinyonga kitasa hicho ili kimruhusu aingie ndani lakini kitasa hicho kilimkodolea macho na kumwambia asubiri ruhusa kutoka ndani kwa wenyeji wake. Christina aliwaambia wenzake wajifiche ili wamnase mwizi wao anayechezea na kudhalilisha miili yao. Christina aliuendea mlango akaingiza funguo na kunyonga kitasa kilichouruhusu mlango kufunguka na kulakiwa na tabasamu la mgeni wake. Gosbert aliingia ndani huku akielekezwa aketi katika deka ya chini ya kitanda kilicho kushoto pembeni ya mlango. Christina alifunga vizuri mlango na kuuondoa ufunguo katika kitasa kisha alirejea kitandani na kuketi karibu na Gosbert. Gosbert alimkabidhi mfuko mweusi uliohifadhi viazi ulaya vilivyoshikamana na mayai pamoja na vipande vya nyama vilivyotungwa kwa ustadi katika vijiti maalum. Christina uliupokea mfuko ule na kuuweka mezani, kisha akamuuliza Gosbert,

"Samahani baby, mbona hujaniletea soda jamani. "

"Tazama vizuri mpenzi, soda imo ndani ya huo mfuko. "

"Ok asante sana baby Kwa kunijali. "

"Usijali mama, mtoto mzuri kama wewe anahitaji matunzo tena. . . . . . . . . . . . "

 Gosbert hakupoteza muda,  alimsogelea Christina na kuanza kumkumbatia huku akimpiga mabusu ya nguvu shavuni mwake. Katika hali ya kustaajabisha Gosbert alihisi……

Kama kawaida ni
Whatsapp au piga +255 758 018 597Kama Hauna App Yetu Bofya HAPA KUPAKUA


 

Post a Comment

0 Comments