Tafrani ya Pendo (Riwaya) - Utamu 18+ “Prosper! Prosper! Prosper! Mshike baba yako ataniua!” Alisema mama huyo na baadaye kukaa kimya huku akiendelea kutoka damu, hiyo ndiyo ilikuwa kawaida mama huyo aliishi kwa mateso jambo lililomkera sana Prosper na dada zake.
“Baba mwache mama! Kwanini unampiga hivyo si keshakufungulia mlango?”
“Wee unanishika unataka kunichangia na mama yako siyo?”
“Sitaki kukupiga baba lakini naomba usimpige mama kiasi hicho hana kosa!”
Wakati Prosper akiongea maneno hayo tayari Kasanda na Nyamizi walishafika na kumnyanyua mama yao aliyekuwa amelala chini akiwa amepoteza fahamu huku damu nyingi zikimtoka mdomoni, midomo yake ya juu na chini ilikuwa imevimba kwa ngumi aliyopigwa na mume wake, wakambeba na kumpeleka chumbani kwao ambako walimmwagia maji akarejewa na fahamu.
“Mama twende polisi!” Kasanda alimshauri mama yake.
“Hapana watoto wangu tukienda polisi baba yenu atafungwa! isitoshe sisi Wanyamwezi hatutakiwi kabisa kushtaki polisi tunapopigwa na waume zetu”
Watu wote katika kijiji cha Tutuo barabara ya kwenda Sikonge walikoishi Prosper na wazazi wake walitambua ukorofi wa mzee Kabaka na hakuna mtu aliyediriki kumkemea, kila mtu alimuogopa.
Kama ungefanikiwa kukutana na mama Kalunde, sio siri machozi yangekutoka, alikuwa ni mama wa makamo, mrefu mwenye umbile la kitutsi,rangi ya ngozi yake ilikuwa nyeusi lakini iliyojaa makovu mengi, kwa kumwangalia ungegundua kabisa kuwa mama huyo aliwahi kuwa tishio wakati wa ujana wake!
Alikuwa ni mama mwenye mateso, alipigwa karibu kila siku na mume wake,hakuwa na sikio moja tayari lilishakatwa na mumewe! Jicho lake la kulia lilikuwa chongo baada ya kupasuliwa na mume wake wakati wa kupigwa miaka miwili kabla ya siku hiyo! Alikuwa ni mama aliyepata mateso makubwa mno katika maisha yake ya ndoa.
Wakati hayo yote yakitokea Prosper alikuwa na umri wa miaka 17 akimalizia kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Sikonge, pamoja na matatizo aliyokuwa nayo alifanikiwa kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano katika shule ya sekondari ya St.Magreth ilikuwa ni shule ya bweni, na ilikuwa ni lazima aende kuishi bwenini akiwaacha dada zake Kasanda na Nyamizi pamoja na wazazi wake.
“Prosper tutaweza kweli kumhimili baba akimpiga mama?”
“Mungu atawasaidia dada zangu sina budi kwenda shule ili niwasaidie baadaye!” Prosper aliwaeleza dada zake wakati wa kuagana, akaondoka kwenda zake Moshi shuleni.
Alipofika shuleni kwa mara ya kwanza alikuwa amechelewa na kilichomchelewesha zaidi ilikuwa ni ada, mama yake Kalunde alilazimika kufanya vibarua katika mashamba ya watu ili aweze kupata pesa za kumwezesha Prosper kwenda shule! Baba yake hakujali kabisa.
“Prosper mwanangu usifanye michezo shuleni, si unaona maisha yetu yalivyo na unaona nilivyohangaika? Baba yako hana msaada wowote, yeye ni pombe kila siku na kunipiga mimi tu, familia nzima tunakutegemea wewe uje kuwa mkombozi wetu kajitahidi mwanangu!”
“Sitakuangusha mama nakuahidi! “
“Sawa mwanangu!”
Darasa lao lilikuwa na wafunzi hamsini na mbili kati yao wasichana wakiwa kumi na saba! Ni Prosper peke yake aliyeonekana kuwa na uwezo mdogo kifedha na watu wengi walimdharau, alikuwa na nguo zilizochanika na madaftari yake yalikuwa ni ya kurasa shirini na nne ambayo hayakutumiwa na wanafunzi wengi shuleni hapo! Yalidaiwa kuwa ya watoto wa shule za msingi.
Pamoja na umasikini wake Prosper alijitahidi sana na masomo kama alivyomuahidi mama yake na hiyo ni kwa sababu aliifahamu familia yake, alitaka asome ili apate uwezo wa kuwakomboa ndugu zake, barua zilizokuja kutoka nyumbani kwao zilimweleza juu ya kipigo alichopata mama yake na Prosper alilia.
Wanafunzi wengi walimtenga sababu ya umasikini wake isipokuwa msichana mmoja tu aliyeitwa Belinda!Msichana huyo alimsaidia Prosper kwa vitu vingi shuleni ikiwemo Sabuni, mafuta na hata sukari na wakatokea kuwa marafiki wakubwa.
Katika mtihani wa mwisho wa muhula aliwashangaza wengi pale alipoibuka na kushika namba ya kwanza kati ya wafunzi wote! Ni matokeo hayo ndiyo yalianza kumpa heshima na marafiki wengi shuleni.
Shule zilipofungwa kwa sababu Prosper hakuwa na nauli ya kumrudisha hadi nyumbani kwao Tabora, ilibidi abaki shuleni peke yake akijisomea! Alimkumbuka sana mama yake na alitaka kwenda nyumbani lakini kwa sababu hakuwa na nauli alilazimika kubaki peke yake shule nzima.
Shule zilipofunguliwa wanafunzi wote walirejea shuleni na yeye na Belinda msichana aliyeonekana kutoka familia tajiri jijini Dar es Salaam, walisoma na kufanya kila kitu pamoja Belinda alikuwa miongoni mwa wasichana wagumu kuelewa masomo yao, lakini Prosper alitumia muda wake mwingi kumfundisha hatimaye akawa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri katika mitihani yao.
Mwisho wa muhula wa pili Prosper alishika tena namba ya kwanza darasani kwake na Belinda aliibuka katika kumi bora! Kila mtu mpaka walimu wake walishangaa,hilo liliukomaza zaidi uhusiano wao.
“Prosper utakwenda Tabora likizo hii?”
“Mimi? Mimi? Hapana sitakwenda!”
“Kwanini?”
“Sina nauli ya kunipeleka nyumbani nendeni tu mtanikuta!”
“Hapana Prosper this time ni lazima uende!”
“Nitakwenda na nini sina nauli Belinda?”
“Nitakupa nauli ya kukupeleka na kukurudisha!” Alisema Belinda.
Prosper hakuamini aligeuka na kumwangalia Belinda usoni, wote wawili walijikuta wakitabasamu na baadaye kukumbatiana na kuanza kupigana mabusu usoni, Belinda alijaribu kuupenyeza ulimi wake kuuingiza mdomoni kwa Prosper lakini Prosper aliuma meno yake kuonyesha hakupenda kitu hicho kitokee!
“Belinda unataka kufanya nini?”
“Nakupenda Prosper tafadhali tunyonyane ndimi!”
“Nitatapika Belinda sijawahi kufanya kitu kama hicho hata siku moja!”
Belinda alishindwa kuendelea lakini alijua ni kwanini Prosper alisema hivyo, alimwachia na wakaendelea na safari yao kuelekea mabwenini kujipumzisha wakisubiri siku inayofuata.
Asubuhi kitu cha kwanza alichofanya Belinda ni kumkabidhi Prosper kiasi cha shilingi 80,000 kwa ajili ya nauli ya kumpeleka Tabora na kumrudisha shuleni.
“Belinda mbona pesa hizi ni nyingi sana!”
“Zitakazobaki utawanunulia wazazi na ndugu zako zawadi!”
“Ahsante Belinda, sikutegemea!”
“Ahsante wewe kwani bila wewe mimi nisingefanikiwa kimasomo? Isitoshe nakupenda Prosper huwezi kupata taabu wakati mimi nina kitu!”
“Belinda mzazi wako ni nani hasa hapa nchini?” Ilibidi Prosper aulize, sababu alishangazwa na msichana mdogo kama Belinda kuwa na kiasi kile chapesa.
Belinda alimweleza kila kitu kilichokuwepo katika maisha yake, alieleza pia juu ya utajiri wa baba yake na jinsi baba yake alivyompenda sababu alikuwa mtoto pekee wa kike! Hakuacha kumweleza juu ya mama yake wa kambo.
“Nina kila kitu nyumbani isipokuwa upendo wa mama, mama yangu wa kambo ananitesa sana, hanipendi amewafanya hata kaka zangu wa kambo pia wanichukie!”
“Unafikiri ni kwanini?”
“Kwa sababu wanajua baba ananipenda na kuna uwezekano wa kupata sehemu kubwa sana ya mali yake akifa, hiyo nafikiri ndiyo sababu kubwa!”
“Pole!”
“Ahsante, lakini nataka uelewe nakupenda na tukirudi kutoka likizo safari hii nataka kila mtu aelewe jambo hapa shuleni ili wavulana waache kunisumbua!”
“Huogopi kuchekwa Belinda!”
“Kwanini?”
“Sababu mimi ni masikini!”
“Nakupenda kwa jinsi ulivyo Prosper!”
Ni kweli Prosper alikuwa na sura ya kumvutia kila mwanamke kilichomsumbua kilikuwa ni umasikini.
Prosper alikata tiketi ya treni na kusafiri hadi Tabora mjini ambako alipanda mabasi ya kumpeleka hadi nyumbani kwao Tutuo, kiasi cha kilometa sabini hivi kutoka Tabora mjini, njia nzima alimfikiria mama yake alitaka sana kumwona!
Ulikuwa umepita muda mrefu bila kuonane naye! Mawazo juu ya dada zake na baba yake hayakumuumiza kichwa sana, alimuwazia mama yake zaidi, alimpenda sana na hapakuwa na mtu mwingine kama mama maishani kwake!
Aliposhushwa na basi kituoni kitu cha kwanza alichofanya ni kukimbia dukani na kununua vitenge doti tatu kwa ajili ya mama yake na pia alinunua magauni mawili kwa ajili ya dada zake, Nyamizi na Kasanda! Hakusahau kumnunulia baba yake suruali nzuri! Moyo wake ulijaa furaha, alikuwa na hamu kubwa mno ya kuiona familia yake tena.
Baada ya manunuzi hayo alinyoosha moja kwa moja kwenda nyumbani kwao,njiani akiwa amebeba begi lake alishangaa jinsi ambavyo watu walimwangalia na kuonyesha masikitiko.
Alipofika nyumbani kwao hakuna mtu aliyejitokeza kumpokea, mlango wa nyumba ulikuwa wazi, ilibidi aingie hadi ndani akiliita jina la mama yake, lakini hakuitikiwa, mwisho alianza kuita majina la dada zake lakini bado ilikuwa kimya.
Wakati bado akijiuliza maswali kichwani mwake alitokea rafiki yake mkubwa aliyeitwa Kategile na kusimama mbele yake.
“Pole sana Prosper bahati mbaya umechelewa mazishi!”
“Ya nani?” Aliuliza kwa mshangao Prosper.
“Baba yako!”
“Baba?”
“Ndiyo!”
“Baba kafariki lini?”
“Wiki iliyopita!”
Prosper alianza kulia na majirani wengine zaidi walifika na kuanza kumpa pole, walishangaa kuwa hakuwa na taarifa hizo!”
“Sasa mama na ndugu zangu wapo wapi?”
“Wapo kituo cha polisi kati mjini Tabora”
“Wamefanya nini?”
“Ni wao ndio walimpiga baba yako na kumuua!”
Siku iliyofuata asubuhi Prosper alikwenda moja kwa moja kituo cha polisi kati kuwaona ndugu zake pamoja na mama yake, alilia machozi alipomwona mama yake akiwa mahabusu, aliomba kuongea naye akaruhusiwa na wakapewa chumba yeye na mama yake pamoja na dada zake waongee.
“Mama kweli mlimuua baba?”
“Mwanangu nililazimika kufanya hivyo kwani alichukua kisu na kunikata sikio langu la pili…..”Mama yake Prosper alianza kulia.
“Alilitoa?”
“Halipo mwanangu, nimepoteza masikini yangu yote mawili baba yako alikuwa katili mno alistahili kufa na ninakiri nimemuua!”
“Ulimuua na nini?”
“Nilimpiga na mchi kichwani akaanguka na kufa! Huo ndio ukweli mwanangu!”
“Mama ulishindwa kweli kufuata ushauri wangu?”
“Nisamehe mwanangu!”
“Mama hautafia gerezani ni heri nifungwe mimi na kunyongwa lakini wewe uwe huru nakupenda mno mama!” Alisema Prosper huku akilia.
Baada ya maongezi Prosper alirejea mjini ambako alikwenda moja kwa moja kituo cha polisi kati mjini Tabora.
“Naomba kuonana na mkuu wa kituo!”
“Wewe nani na una shida gani?”
“Nina maongezi marefu kidogo siwezi kukueleza wewe!”
Alionyeshwa ofisi ya mkuu wa kituo na kuingia.
“Shikamoo mzee!”
“Marahaba nikusaidie nini kijana!”
“Mzee unakumbuka mzee Kabaka aliyeuawa siku chache zilizopita?”
“Ndiyo si yule aliyeuawa na mke wake?”
“Ndiyo! Yule ni baba yangu na aliyemuua si mama yangu ni mimi! Nilitoroka baada ya kitendo hicho na ninakueleza wazi kuwa nimerudi ili mama yangu aachiwe mimi ndiye niwekwe rumande!”
“Kweli?”
“Huo ndio ukweli ni mimi niliyempiga baba na mchi kichwani akafa!”
“Kwanini?”
“Kwa sababu alikuwa anamtesa mama yetu!”
“Mungu wangu!Afande Charles!”
“Naam Afande!”
“Hebu njoo hapa mara moja!”
Sekunde tano tu tayari askari alisimama mbele ya meza ya mkuu wa kituo.
“Ndiyo afande!”
“Mchukue huyu kijana umpeleke rumande, kumbe ndiye aliyemuua baba yake kule Tutuo na sisi tukawakamata mama yake na dada zake sasa amejileta mwenyewe! Peleka mahabusu haraka na mama yake na dada zake waachiwe mara moja”
“Sawa afande!”
Askari alimnyanyua Prosper na kumzaba vibao kadhaa usoni, kisha akamchukua +255 758 018 597 whatsapp. +255 758 018 597
DARASA LA ENGLISH COURSE 

Nafahamu wewe ni msomaji mzuri wa simulizi zetu na unatuamini sana, zaidi tumependa kukuletea huduma ya ENGLISH COURSE kwa njia ya online na uso kwa uso kama upo dar es Salaam (+255 758 018 597).


Post a Comment

0 Comments