Sweet Pastor (Riwaya) - Pastor Mtamu

"si unaona sasa, kumbe kaja? Hawa ni watoto wetu Bwana"

"lakini nadhani hayupo tayari kwa hilo mana nimemkuta binti yangu kanuna na istoshe kaja na huyo anaesemekana ni mchumba wake"

"unasemaje?.. Amekuja na huyo binti mwingine"

"inavyosemekana"

"hebu nipe hii siku ya leo... Tutayamaliza, wewe ni rafiki yangu toka utotoni, mpaka sasa tupo pamoja.. Nataka tuwe ndugu sasa, hahahahaha.. Bwana Yohana kiwa huru Bwana"

Aliongea Mr. Jacob huku akiwa na furaha sana juu ya kutaka kumpa mtoto wake mke ambae ni mtoto wa rafiki yake

"sawa Mr. Jacob, staki binti yangu aolewe na vijana wa ajabu ajabu... Mimi ni mtu na heshima zangu"

Aliongea Mr. Yohana wakati huo Catherine ndio anazidi kujiskia raha na kupata nguvu zaidi mana swala hilo limeshikiliwa na wazazi,...

"usijali kabisa ndugu yangu... Bwana Yesu atuongoze"

Aliongea Bwana Jacob kisha simu ikakata,

 

Huku nyumbani kwa akina Adam akiwa ndio anaingia nyumbani kwao, Jessica aliwahi kumpokea mdogo wake, na anamheshimu sana mdogo wake,.. Jessica ndio mtoto wa kwanza katika hii familia,..

"imekuwaje huko wifi"

Aliongea Jessica huku akiingiza kibegi ndani,

"wala hakuna lolote, alimwambia tu kuwa ana mchumba wake"

Wakati huo wakiulizana hivyo Adam hakuwepo hapo, kumbe alishatoka kitambo tu, na Wakati huo ni mida ya saa 11 za jione kwenda saa 12,... Adam alifikia kwenye nyumba moja mpyaaaa, ila imeshaisha ujenzi, kumbe Adam ana nyumba kabisa yaani akirudi huko sio mtu wa kukaa tena kwa baba yake,... Ilikuwa ni nyumba kubwa mno na haistahili aishi pekee bali mke.. Katika nyumba hio kila kitu kilisha wekwa, yaani hapo ni kuhamia tu,...

"ondoa hofu, lazima uilewe na kaka yangu"

Ni huku kwa akina Adam, Jessica akiwa anamhakikishia Eva kuwa ni lazima aolewe na Adam,...

"sawa wifi yangu, ila kama hili jambo wamelishika wazazi, huoni itakuwa ni hatari kwangu"

"ondoa shaka, mimi namjua vizuri Adam... Nimemkuza mwenyewe.. Namjua haoi mtu pale"

Aliongea Jessica, lakini wakati huo Eva anataka kirudi nyumbani,... Haraka haraka Jessica anampigia Adam simu..

"we subiri upelekwe mpaka nyumbani unaogopa nini"

Aliongea Jessica huku simu ikiwa sikioni

"sawa"

 

"haloo Mtumishi... Njoo basi umpeleke mwenzio nyumbani"

Aliongea Jessica kwa kumuita Mtumishi,.. Ni jina ambalo wamelizoea kwa watu wengi na pia kutokana na kipawa chake..

"sawa nafika hapo sasa hhivi"

Kweli haikuchukuwa muda Adam alifika nyumbani kwao na kumchukuwa Eva,....

 

Sasa huku kazini baba yake Adam anatoka kazini, anawaza cha kumwambia mtoto wake, kwanini kaenda kuleta fujo katika nyumba ya watu,

 

Wakati huo mama yake Eva alikuwa hana raha mana toka mchana hajamwona mtoto wake,... Bite ambae ndio mdogo wake na Eva pia alikuwa ni mtu wa wasiwasi, tena mama ndio kabisa kwasababu asubuhi kuna maneno aliyasikia toka kwa akina Janet,.. Mama na mtoto wake bitw wakiwa wamekaa hapo nje kila mmoja kashika tama, na tayari kagiza kameshaanza kutanda,.. Waliona taa za gari zikiwaelekea huku waliko..., taa iliwakera mno mana walikuwa katika dimbwi la mawazo,.... Ghafla gari inasimama karibu yao na Adam anashuka na kumsalimia mama mkwe

"mama, shikamoo mama"

"marahaba baba, ooooohhh Mtumishi? Tumsifu Yesu Kristo"

"milele amina"

"karibu ndani"

Wakati huo Eva nae ndio anatoka ndani, bite akamkimbilia dada yake baada ya kusalimiana na shemeji yake,... Mama haamini kama leo mwanae kaletwa na gari japo aio mara moja kuletwa na gari, ila kwa sasa kuna changamoto kidogo hivyo lazima kuwepo na mshangao kiasi,...

"karibu baba Mtumishi"

"Ahsante sana...."

"biteeee, we bite... Hebu kalete maandazi haraka Mtumishi apate chai"

Aliongea mama kwa kumtuma bite, lakini Adam alikataa kupata chai kwa maana ya kuwahi nyumbani,... Kweli kwa akina Eva maisha si mazuri, yaani ni watu wanaomtegemea Mungu vibiashara vidogovidogo ambavyo mama huyo huweka nje ya kanisa ili apate kuuza angalau hata juisi,... Na ukiwaona huezi jua kama ni watu wa dhiki, mana wahenga walisema kuwa, UMARIDADI HUFICHA UMASIKINI,... Ghafla simu ya Adam iliita, kuangalia jina, alikuwa ni baba yake

"haloo mchungaji"

Aliita Adam huku simu ikiwa sikioni

"sijakukuta nyumbani upo wapi usiku unaingia huu"

"aahh nakuja sasa hhivi baba"

"hebu wahi nina maongezi na wewe"

"sawa"

Adam hakutaka kuchelewa, alimuaga mama yake Eva kisha akatoka zake nje... Aliingia katika gari lakini ghafla Eva kaja nae kaingia katika gari,

"nimeona sms yako, kuwa ukitoka nikufuate"

Aliongea Eva, kumbe hakutaka kumuita mbele ya mama yake...

"ndio, kwani ni vibaya kumuita mama mchungaji wangu"

"hahahahaha hapana si vibaya"

"ok... Shika hiki kiasi, kitawasaidia"

"lakini baba Mtumishi"

"lakini haitakiwi,... Ashukuliwe baba muumba kwa riziki kupatika.... Kwaheri, tuonane kesho kanisani.. Afu, naomba hio pesa ikiisha unipe taarifa,... Staki mama mkwe akakae juani tena, kuleni vizuri muombeni Mungu sana.. Mwezi huu huu naweza kuoa"

Aliongea Adam huku akiwasha gari

"Catherine au"

Aliongea Eva huku akiwa kashika tama

"sina uwezo huo, naoa nilichokipenda.. Hata vitabu vya Mungu viliandika, Mpende anaekupenda"

Adam aliongea mengi sana,... Kumbe hata kabla ya Adam kuondoka, yeye ndio alikuwa akitegemewa na familia ya Eva,.. Mana baba yake Eva alikuwa ni mzee wa kanisa moja wapo kati ya makanisa ya Mr. Jacob, hivyo baada ya kifo cha baba yake Eva,... Adam aliamua kubeba jukumu zima la familia hio, mana mzee yule alikuwa akiishi kwa sadaka za waumini, sasa hayupo, nani achukue sadaka.. Hakuna.... Hivyo Adam kachukuwa jukumu hilo peke yake.... Na anajua waliteseka sana kipindi yupo masomoni,.. Japo aliwaachia kiasi kikubwa cha fedha,..

"Mtumishi Jacob kaniita, hivyo wacha nimuwahi"

Aliongea Adam kumaanisha baba yake kamuita....

"sawa,... Naomba Bwana Yesu aingilie kati mahusiano yetu, mana tuna nia njema na huu ulimwengu"

Aliongea Eva,.. Na wakati huo ibada ikadondoshwa hapo hapo kwenye gari,... Mama na mtoto wake bite kusikia ibada inadondoshwa, nao wakaungana nao kwa kupiga magoti kisha kuomba sambamba na wao,..

 

Baada ya maombi, Adam aliondoka zake.... Sasa Eva anakwenda kukagua kapewa kiasi gan,...

"Yesu wangu, kakupa pesa zote hizi"

Aliongea mama yake Eva huku wakizimwaga mezani,...

"mama, unajua kweli Mtumishi Adam anaona mbali sana... Hhivi kajuaje kuwa humu ndani tunaishi kwa uwezo wa Mungu pekee... Kajuaje kuwa hatuna kitu.. Mama?? Ashukuliwe baba Muumba mbingu na ardhi"

Kiukweli pesa walizopewa zilikuwa ni nyingi, kwa haraka haraka, labda ni kitu kama laki tano hhivi, ila inazidi zaidi ya hapo...... Walifurahi sana na kuzidi kumuombea Mtumishi Adam

 

Huku kwa mzee Jacob akiwa kaketi Katika sofa la uvivu, yaani lile la kulala,... Ghafla alisikia honi ya gari,.. Alijua tu ni mtoto wake Adam ndio anakuja... Kweli alikuwa ni Adam, au Mtumishi Adam

Wakati huo mzee Jacob baada ya kumsikia mtoto wake Adam akiingia, basi aliitisha kikao cha dharura hapo ndani akiwemo mama na dada mkubwa wa Adam,... Huku katika paking Adam alipaki gari vizuri lakini hakushuka, sasa akawa anawaza ni jinsi gani ataongea na baba yake kuhusu swala la kuoa kwake,.. Lakini akiwa ndani ya mawazo, alikumbuka kitu fulani na kutoa simu yake na kumpigia mtu fulani ambae anajuana nae,..

 

Baada ya kuongea na huyo mtu, Adam alishuka katika gari, lakini kidogo alikuwa na tabasamu, sasa hatujui aliongea na nani na maneno gani,.. Adam aliingia ndani moja kwa moja mpaka mezani, mana alijua tu kukaa kwa watu hao mezani na hakuna hata mtoto wala mfanyakazi, alijua tu kuna maongezi yanaendelea hapo

"asifiwe Bwana Yesu Kristo"

Alitoa salamu ya kumsifu Bwana Yesu Kristo...

"milele amina"

Waliitikia wote watu watatu,.. Lakini kabla hajakaa, ghafla simu yake inaingia meseji... Aliifungua na kuisoma kimya kimya kisha akaendelea kukaa...

"ndio mchungaji, ulisema niwahi nyumbani"

Aliongea Adam huku anamwomba Mungu wake kwa lolote litakalotekea liwe zuri katika maisha yake,....

"nyumbani kwa Mr. Yohana ulifika saa ngapi"

Aliuliza Mr. Jacob

"nilikwenda time za jioni hhivi... Kuchukuwa begi langu"

"begi?? Begi gani tena"

"aahh wakati nashuka pale Airport,.. Alikuwepo mtoto mchungaji Yohana, na yeye ndie aliepokea begi langu"

"kwanini ulipokwenda huko ulikwenda na mwanamke, ingali nilishakupa taarifa kuhusu mtoto wa Mr. Yohana"

Aliongea Bwana Jacob, huku akihitaji jibu la kueleweka toka kwa Adam

"ndio baba... Kwanza samahani kama nitakukosea baba yangu,... Ni kweli ulinipa taarifa juu ya binti yule, lakini baba huoni utakuwa hunitendei haki kwa kunichagulia mke... Hapo utakuwa umenikosea baba... Kweli nataka kuoa lakini sikumtazama Catherine na pia hata kwenye akili yangu haipo kwa Catherine.... Baba, tafadhali sana, sijawahi kukutambulisha, ila nadhani ulishawahi kusikia, sasa mimi nataka kumuoa Eva na sio Catherine"

Adam aliongea huku mama na Jessica wakitikisa kichwa kumaanisha sawa kabisa kwa kile anacho kiongea Bwana Adam...

"yaani Eva huyu mtoto wa marehemu paulo"

"ndio"

"nipe sababu saba za kumwoa Eva"

"sasa mzee... Nitakuja kuongea sababu hapa, mwisho utaniona nimetusi sasa... Naomba unipe nafasi ya moyo wangu mzee.. Yule msichana mimi simjui, tunakutana tu kwenye kumbi mbalimbali na makanisani, sijui tabia yake sijui ni mzima au naniii.. Eeeeeee babaaa"

Sasa alipomaliza tu kuongea Adam, mara mama nae akaingilia kati na kusema

"ni kweli.. Kwanza yule mschana anavaa nguo za ajabu sana, yule msichana hata kanisani kwao utamkuta kavaa nguo za ajabu,.. Kwanini tumpe mtoto wetu mwanamke wa ajabu jamani baba Jessica"

Aliongea mama tena kwa msisitizo mkubwa ili aeleweke,....

"mimi nimeshasema.... Taka asitake lazima umuoe Catherine... We ulizani utabarikiwaje na Mungu usipo oa?? Lazima uoe ili Mungu akubariki"

"sijakataa kuoa baba, tatizo ni mke"

"nasema hhivi napiga simu mwanamke aandaliwe wiki hii uoe na kanisa lako"

"baba... Samahani sana.... Kama ni kanisa aitaki,... Wacha niwe mwinjilisti wa mitaani nikaitangaze injili kwa waumini waliokosa nafasi ya kufika makanisani... Sitaki kuoa iwe Eva ama Catherine... Alafu kesho nahamia nyumbani kwangu"

Aliongea Adam kisha akaondoka,.. Wakati huo simu imeganda skioni kwa Mr. Jacob,

"umeona sasa unamvunjia heshima mtoto wetu baba Jessica"

Aliongea mama huku nae akiamka kumfuata mtoto wake kule alipo elekea, na Jessica nae huko huko... Mara Mr. Yohana anapokea simu

"haloo Bwana Jacob"

"ahahahahah Bwana Yohana... Habari ya masaa mawili matatu"

"aahh salama tu Bwana Jacob vp hali"

Yohana alikuwa na furaha mana alijua anapewa jibu zuri juu ya Adam kukubali kuoa

"Bwana hapa ndio nimemaliza kikao na Bwana mdogo... Lakini kiukweli Bwana Yohana nguvu zangu zimeishia hapo, namuheshim sana kijana wangu... Na kitu ambacho nikiweza mpaka sasa... Sintokubali amuoe mwanamke anaemtaka yeye.. Ila sasa naomba umpe nafasi mtoto wako, awe karibu na kijana wangu, ili angalau wazoeane... Kwasababu hapa kwenye kikao kalalamika sana kuwa, hamtambui Catherine... Kwani wao hukutana katika kumbi mbalimbali na makanisani, sasa hawatambuani, hebu mpe nafasi binti yako awe karibu nae, angalau wajenge hata mazoea.."

Alimaliza kuongea Bwana Jacob huku Bwana Yohana akijibu kuwa

"aah hilo mbona halina shaka.. Mimi nataka tuwe ndugu kabisa... Sio urafiki tena, na undugu wetu utaunganishwa na watoto wetu"

"sawa kabisa... Mwambie tu ajitahidi kiasi, mana Bwana mdogo ana msimamo huyo, namjua mwenyewe"

Aliongea Bwana Jacob wakati huo yupo peke yake hapo sebuleni,..

"ondoa shaka, hapo watakutana, mana hata Catherine hana mchezo mchezo kabisa"

 

Lakini Mr. Jacob kuna swali alimuuliza Bwana Yohana kuhusu binti yake, na wakati huo huo Adam ndio anakuja sebuleni kwa ajili ya chakula... Lakini Adam aliposikia hilo swali alisita kuja sebuleni kwanza ili asikie vizuri, mana lilikuwa ni swali la siri... Na hata sisi wasomaji hatutakiwi kulijua.... Adam alisikiliza umakini mzee wake akimuuliza Bwana Yohana kuwa.....

 

Hatujui kamuuliza nini lakini Adam alisikia peke yake, na hata kuja sebuleni hakuja tena akaishia mlangoni na kurudi chumbani kwake

Maongezi ya Mr. Jacob na Mr. Yohana yaliisha baada ya kupata vyema, hivyo kwa sasa Catherine ni yeye na juhudi zake za kuwa karibu na Adam, kazi ipo hapo...

 

Baada ya siku kadhaa kupita na leo ni siku ya Jumapili,.. Familia ya Mr. Jacob ikiwa katika maandalizi ya kuwahi kanisani katika misa ya kwanza, ikumbukwe kuwa Adam toka arudi Nigeria katika chuo cha Biblia, alikwenda kuabudu katika makanisa mengine ya baba yake, mana kuna kanisa kuu na kuna makanisa ya kawaida, na hayo makanisa ya kawaida yana mapasta wengine, mana huyu Mr. Jacob yeye ni Bishop, hibyo kateua mapasta kwa ajili ya malanisa mengine, sasa kuna kanisa kuu ambalo Bishop mwenyewe hilitumikia kutoa huduma kwa waumini wake,... Sasa kanisa hilo kuu Adam hajawahi kufika toka aliporudi masomoni,.. Sasa leo Jumapili ndio anakwenda katika kanisa hilo, wote walikamilika walikuwa kama watu saba hivi skose.. Baba, mama, watoto wanne, na mfanyakazi wa ndani wa kike.. Walipanda katika usafiri tofauti tofauti,... Bishop Jacob alipanda yeye na mtoto wake wa mwisho na mke wake,.. Na Adam alipanda yeye na mfanyakazi na dada zake wawili,.. Kanisa wanalo lielekea ni moja..

 

Katika kanisa hilo wapo waliokuwa wakiabudu kwa mapambio,.. Na walikuwepo viongozi wenye vipawa kwa ajili ya kutoa huduma kwa waumini wao, na hapo ni katika hatua za kumsubiri mchungaji Jacob ama Bishop Jacob kuja kutoa huduma ya neno la Mungu,...

 

"dada, ajui niwawahishe kwanza, mana nahitaji kwenda kumchukuwa Eva ili awahi misa ya kwanza"

Aliongea Adam wakati huo walikuwa njiani...

"twendeni tu kwani gari si inatosha"

Aliongea Jessica huku Adam akikata kona katika njia ya akina Eva, mana Eva na mama yake na mdogo wake hua wanachelewa misa ya kwanza, na misa ya kwanza ni bora zaidi kuliko hata misa zinazifuatia... Uzuri aliwakuta wakiwa tayari wamejiandaa, mara moja walipanda gari ili kuwahi misa ya kwanza...

 

Huku kanisani, Bishop Jacob akiwa tayari keshafika kanisani na huduma ilianza mara moja, lakini sasa katika waumini wa mbele, alionekana Catherine,... Hii siri ya Catherine kuwepo hapa anaijua mzee peke yake.. Mana aliambiwa kuwa aanze kujenga ukaribu na Adam,.. Sasa ndio kaanza kuja kanisani kwao, na hata huyu Catherine wana makanisa mengi kama ilivyo Bishop Jacob... Hivyo huku kaja kwa kazi maalumu,.. Bishop Jacob alianza kuhubiri kwa kishindo kama ilivyo kawaida yake,..

 

Huku katika lifti ya kupanda juu akiwemo Jessica, Martha, sekwa, Eva, Bitris na mama yao,... Lifti ilifika mahala husika na walitoka ili kwenda katika ukumbi wa maombi, sauti ya Bishop Jacob inasikika ikitoa mahubiri yake mazuri sana.. Lakini ghafla simu ya Adam inapata meseji, hivyo kitendo hicho kilimfanya asimame na kuisoma mesji,.. Sasa yeye aliposimama wale aliokuja nao wakatangulia mbele,...

"mwanangu, namuona Catherine hapa kanisani"

Adam alishtuka, ilikuwa ni meseji iliotoka kwa mama yake,...

Lakini hakujali, aliendelea na safari ya kuingia kanisani,...

 

Sasa waumini walikuwa wakisikia tu mtoto wa Bishop Jacob karudi, lakini hawakuwahi kumwona kwasababu alikuwa hasalii kanisa hilo,...

Sasa ile Adam anaingia tu,... Hata baba yake alishangaa, waumini walinyanyuka wote na kusema

"tumsifu Yesu Kristo Mtumishi Adam"

Hata Adam alishangaa, yaani waumini wanampenda kupita maelezo,... Hata Catherine haamini kuwa kanisa zima limenyanyuka kwa ajili ya Adam... Mzee Jacob haamini, yaani mtoto wake anakubalika kuliko yeye,

"asifiwe Bwana mwokozi wetu"

Aliongea Adam huku akipunga mkono,.. Lakini sasa vile alivyokuwa akipunga mkono, waumini wengi walikuwa wakitetemeka,.. Adam anashangaa mbona baadhi ya wingi wa waumini hutetemeka... Akajaribu kupungia tena... Sasa kumbe Adam hajajua kuwa sio waumini peke yao,.. Mana ndio alikuwa akiwapungia mkono,.. Ghafla ilisikika sauti ikisema

Kama kawaida ni
Whatsapp au piga +255 758 018 597


Kama Hauna App Yetu Bofya HAPA KUPAKUA


 

Post a Comment

0 Comments