Riwaya - SAPE UHAINI (Ya VIta, Mapenzi)‘Sikia baby! Nitakuambia kwasababu umeng’ang’ania nikuambie, lakini usinione kama naanza kuwa na mawazo ya kipumbavu’ akaonya
‘Wewe niambie tu’ mwanaume msimamo wake ukabaki hapo hapo
Kujibu ilikuwa rahisi, lakini namna ya kuelezea mawazo yake ndio ikawa tatizo. Ataeleza vipi, katika ufafanuzi upi mpaka aeleweke?
Akakaa kimya kwa sekunde kadhaa akijiuliza wapi pa kuanzia? Mawazo yakamtuma kuanza na ushahidi moja kwa moja. Akaona kuna umuhimu wa kueleza mawazo yake huku akionyesha na mifano hai. Akaifunua tena albam yake na kuikagua picha moja iliyokuwa inamuonyesha yeye na mtoto mmoja wa kike wa kihindi wakiwa ufukweni mwa bahari
‘Nilikuwa nafikiri… Kwa jinsi bosi wangu anavyompenda huyu mtoto wake, basi kama tukimteka, anaweza kulipia fidia ya mamilioni ya shilingi kama vile wanavyofanya katika filamu za kimafia’ akatoa maelezo yake kwa ufupi sana huku akimuangalia mtu wake kwa wasiwasi mkubwa akijua kwamba sasa ataonekana kama mtu anayeanza kudata
Kwa jinsi Chan’duu alivyokuwa akimuangalia, dhana yake kwamba ameongea utumbo ikashika kasi. Aibu ikamvaa usoni akashindwa kusema lolote kwa sekunde kadhaa. Akataka kunyanyuka huku akiwa anasema ‘Nilikuambia yatakuwa mawazo ya kijinga..’ lakini kabla hajasimama wima na wala hajamalizia maneno yake
Chan’duu akamshika mkono na kumshusha kwenye sofa
‘Una uhakika na unachokizungumza?’ Chan’duu akauliza akiwa amekaza macho
‘Si nimekuambia kuwa ni mawazo ya kijinga!’ akajibu akiwa sasa aibu imemvaa rasmi
‘Sijakuuliza kuhusu mawazo yako kama ni ya maana au ya kipumbavu, ninachotaka kujua ni kwamba unahakika kuwa bosi wako anampenda sana mtoto wake na akitekwa anaweza kulipa fidia ya mamilioni ali aachiwe?’ Chan’duu akauliza akiwa akilini mwake anaanza kuona picha za matukio asiyoyajua Follow Instagram @swahilisimulizi
‘Hilo nina hakika nalo asilimia bilioni zote, ila naona ni kitu kisichowezekana kuweza kumteka huyo mtoto’ akajibu akimuangalia bwana wake usoni akiona kuwa hapa sasa wanaanza kufanyana kama watoto wanaoanza kuwaza kiutu uzima.
Sasa ikawa zamu ya Chan’duu kuzama katika dimbi la mawazo, akishika wazo hili na kuliacha akishika wazo lile na kulitupa, akili yake ikiwa inajaribu kuumba kitu huku ikiwa haimpi njia sahihi za kuweza kulijua jambo hilo
‘Baby, hebu tuachane na wazo hilo la kijinga, acha nikapike chakula tule’ msichana akasema akimkamata begani bwana wake ili kupima ni vipi wazo lake limepokelewa rasmi.
‘Hapana baby, unajua umezungumza jambo kubwa sana japo kama wewe mwenyewe hujajua. Si umesema watu wanafanya katika filamu? Sasa wewe unadhani yale matukio ya katika filamu ni matukio ya kuigiza tu? Yale ni matukio ambayo huwa yanatokea kweli katika jamii, na kwa vile hapa nchini halijawahi kutokea tukio kama hilo basi tulikifanya kwa umakini tunaweza kupiga hela mbaya. Niamini mke wangu’ Chan’duu akasema kwa kusisitiza huku akinyanyuka, sura imemuiva kama mtu aliyepigwa kibao cha kushitukiza
Akapiga hatua na kuliendea kabati
Akatoa fulana na kuivaa
Akarudi kwenye sofa na kuchukua simu yake
‘Nakuja’ akaaga bila kusema anapokwenda huku akiwa amekunja uso akionekana kama mtu aliyepatwa na jambo zito lililomchanganya kupindukia.
Msichana akabaki akiwa ameshangaa tu akiwa hawezi kujiuliza wala kujijibu juu ya suala hili lililotokana na mawazo ya kujipitia tu kichwani. Ni vipi sasa wazo hili limeanza kujiumba na kuwa jambo la maana na lenye kuzalisha kitu kikubwa? Akajiuliza swali hili tena na tena
Akanyanyuka na kutaka kuelekea nje lakini alipofika mlangoni alikuwa hajui alitaka kutoka ili aende wapi. Akarudi katika sofa na kuketi kwa kifupi alikuwa amechanganyikiwa.
Akakaa na kuanza kufikiri kwa kina ni kitu gani kilimfanya kuwaza alichowaza, na kipi bwana wake anaweza kufanya katika kuthibitisha kwamba wazo lake ni la maana na linaweza kuzalisha matokeo makubwa. Mara wazo likamjia kwamba umasikini unawafanya sasa kuanza kuwaza upumbavu. Hapa akatabasamu kwa mbali lakini akajiona kama anajicheka ujinga. Tabasamu likamtoka.
Akajiegemeza katika sofa akili yake ikiwa haiwazi hili wala lile
Ikifika mchana Sofi huwa alikuwa anatoka na kwenda tena shule kumfuata mtoto. Wakirudi, tayari mfanyakazi mwenzake ambaye ndie huwa anaishi na mabosi zake na kuwa mpishi na mtayarishaji wa shakula, huwa ameshandaa msosi, wanakula, anamtayarisha mtoto na kumpeleka kulala mpaka jioni mabosi wanaporudi na yeye kuwa siku yake ya kazi imekwishia hapo, anasubiri siku nyingine zikatike ili achukue mshahara wake kiduchu na kuutia kibindoni
Japo kama familia hii ya mabosi zake haijui vizuri, kwa undani, lakini kuna sifa mbili kuu alikuwa anazijua kindakindaki
Sifa ya kwanza, ni ubahili ulioambatana na roho mbaya wa bosi wake wa kiume, na sifa ya pili, ni kuhusu bosi wake wa kike alivyo mkali na mkorofi juu ya watu wengine na mapenzi makubwa aliyonayo mama huyo juu ya mtoto wake mdogo
Kiundani kabisa Sofi kazi hii alikuwa inaifanya kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kupata kazi nyingine. Kusoma hajasoma, na mtu wa kuweza kumuunganishia kibarua sehemu nyingine alikuwa hana. Mapenzi juu ya mabosi zake alikuwa hana hata chembe na wala alikuwa hajali kuwaona wanacheka ama wamenuna wanagombana au wanachekeana
Sasa leo hii wazo hili lililompata ghafla juu ya umafia ambapo ameshauona sana katika filamu anazoziangalia kwa mabosi zake kupitia televisheni, hakuwa anawaza kabisa kwamba anaweza kusababisha hali ya huzuni na mtafaruku kwa familia ya mabosi zake
Umasikini wake na umasikini wa familia yake kijijini sio kitu kikubwa kilichomfanya kuwaza alichokisema, ila tu jambo hili liliuvaa moyo wake ghafla na wala halikumfanya kujihisi kwamba anawaza ushetani Follow Instagram @swahilisimulizi
Akakaa hapo varandani kwa muda wa masaa mawili mfululizo bila kujijua wala kunyanyuka kwenda popote mpaka usingizi ukampitia
Kilichokuja kumgutusha usingizini ni simu yake ya mkononi kuita
Akiwa bado ana mang’amung’amu ya usingizi, kiuvivu kabisa akapeleka mkono na kuichuka simu yake na kuiweka sikioni, lakini kipindi anaiweka tu katika sikio lake nayo ikakata
Hakuangalia mpigaji, akashusha mkono chini ili aiweke simu chini na kuendelea kuuchapa usingizi
Lakini kipindi ndio mkono unadondokea katika sofa tu simu ikaita tena
Huku akihisi anasumbuliwa na kukatishwa stimu ya usingizi akasonya kidogo na kuipeleka simu sikioni
Akaipokea bila kutazama ni nani anayepiga
‘Hallow’ akasema kwa sauti ya chini iliyojaa uchovu
‘Sasa wewe muda wote nakupigia simu hupokei maana yake nini?’ mpigaji akauliza kwa kulalamika
‘Ah! Hamna beby, nilikuwa sijaisikia mana umeniamsha usingizini’ akajibu akijua kwamba anongea na Chan’duu
‘Hujasikia wakati simu imeita zaidi ya mara nne?’ mwanaume akauliza tena kwa msisitizo
‘Nilikuwa nimepitiwa wangu’ akajitetea
‘Sasa hebu nyanyuka ujimwagie maji uvae vizuri upendeze kisha uje hapa Mwembechai katika hii Bar tunayopenda kuangalia mpira’ Chan’duu akasema kiamri
‘Kuna nini baby? Mimi najihisi usingizi Bwana’ akasema kwa sauti laini ili amshawishi bwana wake kuachwa aendelee kulala
‘We hebu acha ujinga. Nyanyuka na ufanye fasta kuna mtu anataka kuongea na wewe’
‘’Kuna mtu anataka kuongea na mimi? Mtu gani huyo!?’ akauliza akiwa ameshangaa
‘Ndio. Na fanya haraka’ Chan’duu akajibu kwa amri bila kumuainishia ni mtu gani anayetaka kwenda kuzungumza naye
‘Mtu gani huyo? Mbona sikumbuki kama tuna ahadi na mtu. Au kuna ndugu yako anataka kuniona?’ akang’ang’ania kuelezwa
‘Hapana sio ndugu yangu, ila ni jamaa yangu katika mishemishe, anataka uhakika kuhusu dili uliloniambia’
Hapa usingizi Sofia ukamruka
‘We Chan’duu! Yani jambo ambalo tumelizungumza mimi na wewe tayari unatafuta watu unataka kuwaingiza? Sasa hata hatujapanga chochote unaanza kumwaga siri? Mimi nilikuambia wewe ili kama inawezekana tufanye wawili sasa ..’
‘Baby.. Hebu acha porojo’ akamkata kauli kwa ukali ‘huyu mtu ni mzoefu katika mambo hayo japo kama si katika matukio kama hayo lakini anayajua na anaweza kuwa msaada mkubwa sana’ akamalizia na maneno ya kumtoa wasiwasi
‘Mh! Mbona unanitisha? Kama vipi tuachane nalo mana mimi niliongea kama utani tu’ akataka kukwepa
‘Sofia nimesema acha ujinga, hebu njoo huku tuongee mambo ya maana usitake kunikorofisha kabisa au kwasababu sijakutandika siku nyingi sasa unaaanza kunizoea?’ akauliza kwa ukali
‘Hapana baby ila..’
‘Hakuna ila, nakupa dakika kumi na tano iwe umeshafika’ akaamrisha na kukata simu
Sofi akabaki na simu yake mkononi akiwa haamini kwamba Chan’duu wazo hili amelishupalia zaidi ya alivyodhani
Akiwa anamjua mwanaume wake alivyokuwa hapendi kuchezewa, akanyanyuka na kwenda maliwatoni kuoga
Aliporudi ndani akavaa jinz na tshat na kutoka
Akafika barabarani akachukua bodaboda na kuanza safari
Ilikuwa yapata saa tatu sasa za usiku
Akaingia Mtaa wa Kwimba maeneo ya Mwembechai katika Bar aliyoelekezwa Akatoa simu yake na kupiga ili kuuliza bwana wake alipo
‘Njoo huku kiti moto utatuona tumejitenga pembeni kabisa huku mwisho’ akapewa maelezo
Akamlipa dereva bodaboda na kuelekea ndani moyo wake ukimpiga vibaya sana akili yake ikiwa inajiuliza maswali yafuatayo

Chan’duu jambo hili mbona kalichangamkia sana wakati hajawahi kumsikia hata siku moja kuzungumzia suala la kupata hela nyingi kwa wakati mmoja, na wala hajawahi kumuona na ishara za kuweza kufanya kazi zilizokaa kijambazi jambazi?
Akapishana na muhudumu na kupita meza za karibu
Akasimama kidogo kuangalia pembe ya kwanza lakini hakuwaona walengwa wake
Akaangalia pembe ya pili
Akamuona aliyemkusudia lakini tofauti na alivyodhani, kwani alimuona Chan’duu akiwa peke yake chupa za pombe tu ndio zikiwa mwenza wa kumpa ushirikiano
Huku akienda alipo mtu huyo moyoni alikuwa akijiuliza kama huenda bwana wake anamletea utani
Lakini alipofika karibu na meza na kutupa macho akagundua kwamba Chan’duu hakuwa peke yake kwani kulikuwa na chupa za pombe katika upande wa pili wa meza ikiwa ni ishara kwamba kuna mtu mwingine mahala hapo inawezekana amekwenda msalani tu kujisaidia
Akavuta kiti na kuketi
Muhudumu alipokuja akaagiza Redbul na mtu wa jikoni kwani nyumbani alikuwa hajapika na alikuwa hana mpango huo kwa muda huu uliosonga
‘Ebu niambie vizuri kinachoendelea’ akadai maelezo kabla hata ya kukaa vizuri
‘Unajua baby kitu ulichokizungumza ni bonge la dili, lakini kama unavyoona kwamba si kitu cha mimi na wewe tu peke yetu kukikamilisha, hivyo nimechekecha akili nimeona bora tutafute patna kwa ajili ya kushuhulikia hili swala’ Chan’duu akajibu taratibu kwa kufahamisha zaidi kuliko kutoa maelezo
‘Kwanini unasema hivyo?’ Sofi yeye akataka maelezo zaidi
‘Kwanza kuna suala la wapi pa kumuhifadhi huyo mtoto tukishamteka, kisha kuna mambo yatakuja kujitokeza na nilazima tutaka msaada’
‘Mambo gani hayo?’
‘Kwasasa siwezi kukufafanulia kwani mimi kazi za kuhifadhi kago zinazotafutwa na polisi nimeshawahi kuzifanya na najua mambo yanayotokea. Kwasasa ridhika tu kwamba hii kazi tunahitaji msaada na huyu jamaa anatufaa sana’
‘Huyo mtu ni nani na mnajuana vipi?’ akauliza akijua kwamba sasa hakuna kurudi nyuma
‘Mshikaji anaitwa Mfaume lakini wengi wanapenda kumuita Kijogobwire..’
‘Kijogobwire?’ Sofi akadakia kwa kuuliza
‘Ndio jina lake la utani sijui kwanini wanamuita hivyo lakini hilo ndio jina lake maarufu’
‘Ehe!!’ Sofi akaitikia bila kujua anataka kuchangia nini
‘Huyu jamaa ninamjua kutokana na kufanyakazi za kuiba kwenye magodauni kisha mali ndio huwa tunatafutia wateja, yeye ni mzoefu wa kazi na ana sehemu nyeti ambazo tunaweza kumficha mtu wetu baada ya kumteka na kudai fidia kiulaini kabisa. Na hata tukitaka kampani yeye anaweza kututafutia watu wa kazi zaidi’
Sofi akafikiria maelezo haya kwa kina kisha akasema
‘Sikia baby.. Unajua hili suala itabidi tujitahidi kulifanya sisi watatu tu kwani tukiwa wengi tunaweza kugeukana kisha ikawa balaa huko mbele’ akaonya
‘Usijali tutalipanga kwa umakini wa hali ya juu kisha baada ya hapo wewe mwenyewe utaona’ akajibiwa Follow Instagram @swahilisimulizi
‘Enhe, na huyo bwana Kijogobwire yuko wapi?’ akauliza kwa utani
‘Kuna mtu anaongea naye hapo nje kidogo’
Sasa ikabidi Chand’uu kunywa bia yake na Sofi kunywa Redbul yake kila mmoja kichwani akiwa anafikira zake
Chan’duu akili yake ikiwa mbali akijaribu kuratibu katika kichwa chake suala zima la utekaji na ufanikishaji wake na jinsi mchezo huu watakavyoucheza kwa tahadhari kubwa.
Sofia mawazo yake yote yalikuwa juu ya Kijogobwire, akiwaza mtu huyo yukoje?
Mawazoni mwake akamchukulia kwamba kwa vyovyote atakuwa mrefu eliyejazia mwili na kuwa kama mbeba vitu vizito huku akiwa na sura ngumu yenye kuonyesha kwamba ni mtu hatari aliyekubuhu katika kazi za wizi
Kwa vyovyote mtu huyu mwenye umri wa miaka thelathini na tano au hata arobaini, atakuwa hata kama hana makovu makubwa lakini kovu usoni mwake hazitakosekana
Sura yake itakuwa siyakuvutia na atakuwa mtu ambaye hacheki wala kutabasamu muda mwingi atakuwa mkimya akiwaza dili za wizi tu
Mtu mwenye dili za wizi kiasi cha kazi hatari kama hizi kuonekana ndio anafaa kushirikishwa, kwa vyovyote hatakuwa mtu mwema wala mwenye kuvutia
Hakuna namna nyingine mtu huyu aitwaye Kijogobwire anaweza kuwa zaidi ya hivyo alivyomfikiria yeye
Wakati akiwa bado yuko mbali kimawazo akili yake ikimuumba Kijogobwire katika namna anayotaka yeye, mara akasikia mtu akisema
‘Sory nilikuwa naongea na jamaa yangu kuna dili la nguvu litaingia leo usiku’
Sofi akanyanyua sura na kumuangalia mtu huyo aliyetoa kauli hiyo
Cha kushangaza ni kwamba, mtu huyo aliyesema hivyo alivuta kiti na kuketi mahala ambapo Kijogobwire alitakiwa kukaa
Mtu huyu aliyekuwa mbele ya Sofi alikuwa mweupe, mzuri kisura, si mrefu lakini si mfupi, mwembamba, aliyevalia kinadhifu, uso wake umejenga tabasamu la kuvutia na kupendeza, umri wake hauzidi miaka ishirini na nne
‘Sofi huyu ndio Kijogobwire’ akatambulishwa
Wakati mshangao bado uko wazi usoni mwake kwa kumuona mtu tofauti na alivyomjenga katika mawazo yake akasikia sauti laini na nzuri kutoka kwa Kijogobwire ikisema
‘Niambie patna, mambo yako kama mr alivyoniambia?’
Whatsapp +255 758 018 597 kupata full
Instagram  BOFYA HAPA

Post a Comment

1 Comments

Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)