Hapana Madam (Riwaya) - Utamu



‘Mwalimu nimesikia kila kitu, hivi kweli kwa kuwa nimekataa ndiyo uingize mwanaume mwingine, sijakudhania mwalimu kumbe una tabia za kishenzi hivyo,’’ John alimweleza mwalimu Magdalena aliyekuwa akimwangalia bila kujibu, roho ilimuuma akashindwa kujibu lolote zaidi ya kutoka machozi.
John hakujali machozi ya mwalimu Magdalena, aliondoka kwa haraka huku akimrushia maneno machafu mwalimu wake huyo aliyeonekana kuzidi kuingiwa na huzuni, kwani alifikiria kurudi ndani angekutana na mwenyekiti aliyekuwa na uchu wa kumbaka na mwanafunzi aliyekuwa akimpenda ndiyo hivyo amemjibu hovyo.
Mwalimu Magdalena alijifikiria kwa zaidi ya dakika 10 akajikuta akiishiwa nguvu taratibu aliposimama katika mlango akakaa chini kwa hasira alizokuwanazo machozi yalizidi kumtoka.
Mwenyekiti aliita kwa jazba akimtaka mwalimu Magdalena arudi ndani ili atimize alichokusudia, lakini kila sauti ya ukali ya mwenyekiti ilipomwita mwalimu Magdalena akajikuta akiingiwa na ujasiri akasimama na kumtaka mwenyekiti atoke nje ya chumba chake.
“Mwenyekiti nimekuvumilia vya kutosha, nimekuheshimu vya kutosha na pia umenidhalilisha vya kutosha, naomba utoke kwangu kabla sijafanya maamuzi magumu tokaaaa…’’ alifoka mwalimu Magdalena huku akikifuata kilipo kisu
Sauti hiyo ilimtisha mwenyekiti, hakufikiria kama mwalimu huyo angeweza kubadilika, hivyo aliiangalia sura ya mwalimu Magdalena ilikuwa ikibadilika taratibu, tabasamu lake lilianza kupotea ndita zikaanza kujitokeza, mikono yake iliyokuwa imeshika kisu ilianza kutetemeka kiasi cha kumtisha mwenyekiti, kwa haraka akavuta shati lake lililokuwa juu ya kitanda cha mwalimu Magdalena akaliweka begani na kutoka kwa haraka.
“Naondoka lakini na wewe jiandae kuondoka, siwezi kukaa na aibu lazima nawe uondoke kijijini kwangu mi ndiyo mwenyekiti,’’ alijinadi mwenyekiti huku akiwa ameshika mlango tayari kwa kuondoka, mwalimu Magdalena hakujibu kitu zaidi ya kumuangalia kwa sura ya ukali.
Mwenyekiti alipotoka hali ya mwalimu Magdalena ilirudi taratibu lakini mawazo yake yote yalielekea kwa mwanafunzi John, alifikiria namna ya kumpata kabla haijafika siku ya pili na akaanza kusambaza taarifa zake ambazo hazikuwa za kweli.
Kwa haraka akavaa nguo zake akatoka na kwenda nyumbani kwa John, hakujali muda alitembea kwa umbali gani wala alikutana na nani, alichokuwa akikifikiria ni kukutana na John na kuzungumza naye ili tofauti zao ziwe katika muafaka.
Alifika karibu na nyumba ya kina John akatumia nafasi yake ya ualimu akamuomba John wakasogea karibu ya nyumba yao na kuzungumza.
“John sikiliza wewe siyo mtoto kihivyo, unavyonifanyia sijapenda mimi ni binadamu naumia au kwa kuwa nimekuonyesha nakupenda,’’ alijieleza mwalimu Magdalena lakini John alikuwa kimya
“Nazungumza nawe John mbona hata haunijibu kwa nini hivyo, sikiliza mimi sikufanya chochote na mwenyekiti wala sikumuita wakati ulipoondoka ghafla nikasikia mlango ukifunguliwa na unajua uliniacha nikiwa katika mazingira gani hivyo nikajua kwamba ni wewe umerudi na giza la ndani sikuweza kuona nilidhani wewe John lakini sauti na mikono iliponigusa nikagundua siyo wewe kumbe alikuwa mwenyekiti ameingia akitaka kunibaka na pale ulipokuja kugonga ukawa umenisaidia asiweze kutimiza azma yake, nashukuru kwa kurudi tena lakini kama utanifikiria vibaya Mungu anajua, ninakuhakikishia sikufanya lolote na mwenyekiti,’’ anasema mwalimu Magdalena, taratibu machozi yalimtoka akamuangalia John naye machozi yalimtoka, akainuka na kumfuata mwalimu Magdalena akaanza kumfuta machozi.
Wakati mwalimu Magdalena anasimama ili amshukuru John kwa kumkumbatia, baba yake John anamuona akifanya hivyo, anakasirishwa na jambo hilo anawasogelea.
“Huo ndio ualimu wenye weledi, nauliza huo ndiyo weledi, nyie walimu wasichana kwa nini hivi, ni matatizo haujaolewa wewe, umeletwa huku kutufundishia watoto wetu ama kuwaharibu,’’ alifoka mzee Katuba baba wa John.
“Mzee kukumbatia si vitu vya kawaida kuna jambo la kusikitisha kanihadithia John nikamkumbatia kwa kumfariji kwani kuna tatizo,’’ alijibu mwalimu Magdalena kwa kusitasita huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka machoni mwake.
“Nimesema mambo yenu ya kizungu huko huko mjini kwenu, huku kwetu hatutaki upuuzi wenu kama mmekuja kufundisha mfanye kazi ya kufundisha siyo kuharibu watoto wetu na we John haya ndani haraka,’’ akafoka na kumtaka John aingie ndani.
Mwalimu Magdalena akaondoka kwa haraka akikwepa kelele za mzee Katuba, aliyekuwa akimfokea huku akimfuata.
Hakuwa na furaha, mwalimu Magdalena aliingia na wasiwasi kwamba huenda hali hiyo ikamharibia kazi yake kijijini hapo, lakini licha ya hofu hiyo akajikuta akifarijika kutokana na kufutwa machozi na John mwanafunzi aliyempenda.
Alipofikiria jambo hilo nuru ya uso wake ikawa inarudi mvuto wake ukaangaza upya kama hakuwa na majonzi, aliruka huku na huko akifurahia siku hiyo kwani alishasahau yote yaliyomtokea kabla.
Akiwa njiani wakati huo wa usiku akipita kwenye njia nyembamba iliyokuwa na majani mengi huku pembeni kukiwa na mahindi yaliyokauka akaanza kuhisi kitu, kwani muonekano wake ukaanza kubadilika tena, alihisi anaona vitu ambavyo hakuvitambua vilikuwa vikitokea mbele yake na vingine vilikuwa vikitokea katika shamba la mahindi vikimfuata.
Giza lililotanda eneo hilo liliongeza vitisho kwa mwalimu Magdalena, kwa haraka akatambua kwamba huenda ikatokea tatizo eneo hilo, akaanza kujihadhari akavua viatu virefu alivyokuwa amevaa akavishika mkononi kisha akavuta nguo yake ndefu na kuishika mkono mmoja akaanza kutembea kwa tahadhari.
“Si nimekubamba ulifikiri utakimbia hadi lini,?’’ Sauti ilisikika lakini mtu hakuonekana, mwalimu Magdalena alishindwa kuendelea mbele akarudi nyuma huku mapigo ya moyo wake yakidunda kwa haraka.
Sauti na kitu kilivyoonekana kama sisira kilizidi kumfuata alivyokuwa akirudi nyuma alikotoka huku akiwatazama, kilichosikika hapo ni kicheko cha kejeli na sauti na woga aliyokuwa akiitoa mwalimu Magdalena.
“Nisaidieni nakufaaaa’ kwa haraka mwalimu Magdalena aligeuka na kukimbia huku akipiga kelele huku lile alilodhani kuwa ni sisira likizidi kumfuata na sasa likaonekana kuwa ni mtu alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike.
Lakini kabla hajafika mbali ghafla mwalimu Magdalena akakamatwa na kufumbwa mdomo, sauti haikusikika tena, alihangaika kujitoa katika mkono huo lakini hakuweza alijitupa huku na huko lakini mkono hule ulimshika vema ili sauti isitoke.
Alikukuruka ili ajitoe katika mikono iliyombana vema, lakini hakuweza kuitoa, alijitahidi kujitoa mbele ya mtu huyo aliyemfumba mdomo, sauti pia miguu yake havikumsaidia kufanya chochote kujikwamua kutoka eneo hilo.
Mwenyekiti alishangaa kutosikia sauti ya mwalimu Magdalena, akaangaza huku na kule, lakini hakuweza kutambua wapi alipo mwalimu Magdalena, alinyanyua macho huku na huko, lakini hakufanikiwa.
Taratibu Mwalimu Magdalena alikuwa akipoteza nguvu kutokana na kubanwa na asiyemjua, mtu yule alimvuta eneo lingine ili kumkwepa mwenyekiti aliyekuwa akimsaka mwalimu Magdalena ili atimize ahadi yake.
Mwenyekiti alianza kuhamaki alipojificha mwalimu Magdalena, akavua kinyago alichokivaa kuficha uso wake, akaingia katika majani anayohisi mwalimu Magdalena amejificha.
Mwenyekiti alikanyaga majani yale akiamini mwalimu Magdalena amejificha na yupo peke yake, akazidi kusogea ghafla, naye akashtukia amekabwa na kitu asichokijua.
Mwenyekiti alipiga kelele huku akijitahidi kutoa mkono uliomkaba, lakini hakuweza, akatumia akili za kuruka sarakasi na kujidondosha huku na huko, akapata nafasi ya kujinasua katika mkono huo, hakuwa na ulazima wa kupambana na mtu asiyemjua, akaamua kutimua mbio.
Mwalimu Magdalena taratibu akanyanyuka na kutaka kukimbia, lakini yule mtu aliyemkamata na kumziba mdomo akamkamata kisha akajitambulisha kwake.
“Sitaki, sitaki, sitaki mwenyekiti,’’
“Mwenyekiti, mwenyekiti ndiyo nani mi siyo mwenyekiti, nimekusaidia ulikuwa katika hatari nimekuokoa,’’ walishindwa kuelewana kutokana na giza lililotanda siku hiyo, mwalimu Magdalena alianza kupunguza woga lakini hakutambua sura ya mtu huyo aliyemweleza kuwamba amemuokoa.
Alijitahidi kumtazama lakini hakuweza, mtu huyo alitambua kwamba mwalimu Magdalena anataka kumtambua ni nani, akaingiza mkono wake mfukoni kwake akatoka na simu akawasha tochi kisha akajimulika usoni na kumtaka mwalimu Magdalena amwangalie.
“Wewe ni nani? Umesema ni mwalimu, mwalimu gani na huku umefuata nini?’’ alihoji.
“Mimi ni mwalimu Jokam, wengi wanapenda kuniita Joka.’’
“Joka’’ alihoji kwa hofu mwalimu Magadalena.
“Ndiyo ni Joka kwa kuwa ni mtaalamu wa hisabati, huwa sishindwi chochote katika hisabati na nililetwa kijiji hiki muda mrefu lakini sikupenda lakini kuna jamaa yangu aliniambia aliwahi kufika huku na kuna fursa nyingi huku ndiyo nimekuja kuangalia kama ni kweli nije kufanya kazi huku.’’ Alifafanua mwalimu Joka.
“Tatizo ni nini hadi huyu mwenyekiti akuwinde hivyo.’’
“We acha tu ni story ndefu.’’
“Nisimulie nitakusaidia.’’
“Najua utanisaidia, ila turudi kwanza nyumbani kisha kesho asubuhi nitakuhadithia kama unataka.’’
“Sawa ila mimi ni mwenyeji wa mwenyekiti.’’
“Sasa mwenyekiti mwenyewe ndiyo huyo umemtimua.’’
“Kazi ipo kweli kweli sasa nifanyeje?’’
“Twende kwangu mambo mengine yote utajua asubuhi, maana ni usiku na umenisaidia sana kuniokoa, ila mimi sihitaji hata fursa zilizopo, kesho mapema nitaanza safari ya kurudi mkoani kwetu bora nikawe mama wa nyumbani huko kuliko kuteseka hapa na mwenyekiti,’’ alilalama mwalimu Magdalena.
“Ahaaa! Huyu mwenyekiti ndiyo akusumbue wewe nitadeal naye we niachie mimi tena nitamweka wazi kwa watu wote, kwani hana mke.’’
“Hata sijui,’’ alijibu mwalimu Magdalena.
Mazungumzo yao yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi,
 WHatsapp +255 758 018 597 kupata full
Email - emanmic@yahoo.com

Post a Comment

0 Comments