Riwaya - Vita Maisha (Kivita/kijasusi)



Emanuel ambaye alikua mwandishi bora wa habari Africa alipata nafasi ya kufika Marekani sasa anapata nafasi ya kwenda Iran kikazi, alikaa nchini Tanzania kwa takribani wiki moja na ndipo safari yake ya kuelekea nchini Iraq ikaanza. Ndani ya ndege, Emanuel hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, kila wakati alikuwa na mawazo kupita kawaida.
Hakujua kama angeweza kurudi salama nchini Tanzania, hakuamini kama angeweza kurudi na kumkuta mkewe akiwa amekwishajifungua. Alitamani kumuona mkewe kwa mara nyingine lakini uhakika wa kumuona tena haukuwa moyoni mwake.
“Naomba unilinde Mungu, naomba unirudishe salama nyumbani. Naomba mkono wako unitangulie. Amin” Emanuel alijikuta akisali huku ndege ikianza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Saddam uliokuwa katika jiji a Baghdad.
Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege wakaanza kuteremka, Emanuel akaanza kuyapitisha macho yake katika baadhi ya maghorofa yaliyokuwa yamejengwa katika jiji hilo ambalo alikuwa akilisikia tu katika vyombo mbalimbali vya habari, Baghdad.
Majengo hayakuwa yakivutia sana kama yale ambayo aliyaona nchini Marekani, Uingereza, Uholanzi na nchi nyingine za Ulaya. Idadi kubwa ya watu ilikuwa ikionekana vizuri machoni mwake huku idadi hiyo wengi wao wakiwa wamevaa kanzu na vilemba vichwani.
Emanuel akaanza kuelekea nje ya jengo la uwanja huo, kijana mmoja ambaye alishika bango lililoandikwa jina lake lilikuwa likionekana vizuri machoni mwake. Kwa hatua fupifupi zilizojaa haraka, Emanuel akaanza kumsogelea kijana yule ambaye akampeleka moja kwa moja mpaka katika teksi iliyokuwa nje.
“Welcome to Baghdad City” Kijana yule ambaye alikuwa akindesha gari alimkaribisha kwa kutmia kingereza kilichojaa lafudhi ya kiarabu.
“Thank you” Emanuel aliitikia huku macho yake yakiangalia nje.
Gari lilikuwa likitembea kwa mwendo wa taratibu sana, idadi kubwa ya watu wengi ambao walikuwa wakiandamana mitaani huku wakiwa na mabango ndio ambao walisababisha foleni kubwa ya magari. Emanuel alibaki akiwaangalia waandamanaji wale pamoja na kuyasoma baadhi ya mabango ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya Kingereza.
Hadi kufikia hatua hiyo tayari Emanuel akaonekana kuanza kuogopa. Waandamanaji ambao walikuwa wameshika mabango ya kumkataa rais wa nchi hiyo bado walikuwa wakiendelea kuandamana huku mikononi wakiwa wameshika picha za rais huyo.
Ingawa mabomu ya machozi yalikuwa yakipigwa lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeonekana kuogopa na kurudisha mguu wake nyuma, wote walikuwa wakisonga mbele kuwasogelea mapolisi ambao walionekana kuwa na hasira muda wote.
Sala za Emanuel za kumuomba Mungu zikaanza tena. Alitamani waandamaji wale wasogee pembeni kwa ajili ya kulipisha gari lao lipite. Walichukua dakika kumi mpaka kuwapita waandamaji wale na baada ya kipindi kichache wakafika nje ya hoteli moja iliyoitwa Majifallus.
“This is the hotel I was told to take you to (Hii ndiyo hoteli niliyoambiwa nikulete)” Kijana yule alimwambia Emanuel.
Emanuel akaufungua mlango na kushuka garini na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo la hoteli ile. Moja kwa moja akaanza kupiga hatua kuelekea sehemu ya mapokezi. Kila kitu alikikuta kikiwa kimewekwa tayari kwa ajili yake.
“Thank you” Emanuel alimwabia dada wa pale mapokezi huku akiupokea ufunguo.
Emanuel akaanza kupiga hatua kuzifuata ngazi za kuelekea katika ghorofa za juu. Wasiwasi bado ulikuwa ukiendelea kutawala moyoni mwa Emanuel, fujo ambazo alikuwa akizisoma katika magazeti hasa za maandamano tayari zilikuwa zimekwishaonekana.
Huku Emanuel akiendelea kupandisha ngazi, akashtukia akishikwa bega kwa nyuma. Akageuka na macho yake kugongana na macho ya mtu ambaye wala hakuwa mgeni machoni mwake. Kwa haraka haraka akavuta kumbukumbu juu ya mtu yule kama alikwishawahi kumuona kabla.
“Emanuel....” Mwanaume yule aliita.
“Brian..”
Wote, huku wakionekana kuwa na furaha wakaanza kuelekea katika ghorofa ya juu. Maswali mfululizo yalikuwa yakimjia Emanuel, hakuwa akifahamu sababu ambayo ilimleta Brian nchini Iraq, kila alipotaka kumuuliza, alisita kufanya hivyo.
“Nilikuona tangu uwanja wa ndege, kila nilipojaribu kukuita, haukugeuka” Brian alimwambia Emanuel.
“Ulijua kama nilikuwa naingia hapa leo hii?”
“Ndio. Nilipewa taarifa na mkurugenzi wa CNN, Bwana Swan” Brian alijibu.
“Umekuja kufanya nini huku?”
“Kufanya kazi pamoja nawe. Natamani kujifunza mambo mengi kutoka kwako” Brian alijibu.
“Na vipi kuhusu kazini kwako? Hauoni kama utatumia muda mrefu kuwa huku?”
“Hilo si tatizo. Nimeomba ruhusa. Waliniruhusu kwa sababu tu nilikuwa nakuja kufanya kazi na mmoja wa waandishi aliyetumwa na shirika la CNN” Brian alijibu.
Ukaribu wao ukaonekana kuanza kurudi kwa mara ya pili. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye walikuwa wamemzoea nchini Iraq zaidi ya kuzoeana wenyewe kwa wenyewe. Ukaribu wao ukazidi kuongezeka kila siku, wakawa wakitoka pamoja na kwenda kufanya kazi pamoja mitaani, waliandika kila kitu ambacho walikiona kufaa kuandikwa katika vitabu vyao vidogo.
“Nimefurahi kukutana nanyi. Mimi ni Mchungaji Joseph Terence wa kanisa la Salvation jijini New York. Huyu ni mke wangu, anaitwa Mary” Mwanaume mmoja alevalia suti alijitambulisha mbele yao. “Bwana Asifiwe” Mary alisalimia.
“Amen” Wote wakajikuta wakiitikia.
“Tumekuja hapa kwa kazi moja tu, tumekuja kufungua kanisa hapa Baghdad. Nafikiri kazi hii tutaifanya kesho pamoja na mke wangu” Mchungaji Joseph aliwaambia.
***
Uongozi wa rais Yassin Idrisour ulikuwa ukiwakasirisha wananchi wote wa Iraq. Vita ambavyo vilikuwa vimetokea katika miaka kadhaa ya nyuma dhidi ya Wamarekani na Waingereza bado viliwaacha katika maumivu makali, maumivu ambayo hayakuwa na dalili yoyote ya kupona.
Kila raia wa Iraq alikuwa akiwachukia Wamarekani na Waingereza kuliko mtu yeyote duniani, walitamani mataifa ya Marekani na Uingereza yapotee ili nchi hizo zisiweze kuonekana katika uso wa dunia hii. Wanajeshi mbalimbali wa Kimarekani na Uingereza ambao walikuwa nchini Iraq kwa ajili ya kulinda amani walikuwa wakiuawa kila siku.
Mauaji ya siri siri dhidi ya Wamarekani na Waingereza bado yalikuwa yakiendelea kila siku. Waandishi wa habari na watalii kutoka katika nchi hizo walikuwa wakikamatwa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alijua mahali ambako watu hao walipokuwa wakipelekwa, wapelelezi wa Kimarekani wa F.B.I na wale wa Uingereza walijitahidi kupeleleza lakini hawakuwa na jibu lolote katika upelelezi wao.
Nchi ya Iraq ikaonekana kuwa chungu. Japokuwa mauaji yalikuwa yakishamiri nchini Iraq lakini Wamarekani na Waingereza hawakukoma kabisa kuingia ndani ya nchi hiyo iliyoonekana kujaa damu.
Rais Yassin alionekana kuwa kama kibaraka wa nchi hizo, kila siku alikuwa akiwatetea. Alipokuwa akiongea na vyombo mbalimbali vya habari nchini Iraq, alizidi kuutetea uwepo wa Wamarekani nchi humo, uwepo ambao aliutetea kwamba ulikuwa ni wa kuhakikisha amani nchini humo.
Kila siku Wananchi wa Iraq walikuwa wakiandamana kutaka rais huyo atoke madarakani, hawakumtaka rais ambaye alionekana kuwa karibu na Wamarekani ambao walikuwa wamewapa vidonda visivyokuwa na uhakika wa kupona mioyoni mwao.
Waliwapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao wa karibu katika vita ambavyo vilikuwa vya kumtafuta gaidi ambaye alikuwa ameitikisa dunia katika kipindi hicho, Allabdullah Massoud. Uwepo wa Mmarekani ukaonekana kuwa ghadhabu katika maisha ya kila mwananchi wa Kimarekani.
Ingawa Wamarekani wakishirikiana na Waingereza walijitahidi kuijenga nchi hiyo lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na upendo na Wamarekani hao. Chuki dhidi ya Wamarekani ilikuwa ikiongezeka kila siku, mtoto alipokuwa akikua, alijikuta akiwachukia Wamarekani pasipo sababu yoyote ile.
Watu walipigwa na mabomu ya machozi mitaani huku wengine wakipigwa na risasi za moto lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kupiga hatua kurudi nyuma katika maandamano ambayo walikuwa wakiyafanya kila siku.
Walionekana kuwa radhi kupoteza maisha yao katika maandamano hayo lakini ili mradi Wamarekani hao waondoke nchini humo. Mabango yaliyokuwa yakimtaka rais wa nchi hiyo atoke madarakani bado yalikuwa yakionekana katika kila makundi ya maandamano nchini Iraq.
“Ni lazima tuwaue Wamarekani wote waliokuwa wamepanga katika hoteli nchini hapa” Baadhi ya Waarabu ambao mara kwa mara walikuwa wakionekana kuwachukia Wamarekani walisema.
Msako wa Wamarekani ukaanza kufanyika kimyakimya. Hawakutaka taarifa hizi zijulikane na mtu yeyote ambaye alikuwa nje ya kundi hilo lililopewa kazi ya kuwamaliza Wamarekani. Wamarekani ambao walikuwa katika hoteli katika miji mingine walitekwa.
Kazi ya kuwateka Wamarekani waliokuwa wakiishi katika hoteli zilizokuwa ndani ya jiji la Baghdad ikaanza mara moja. Waarabu wakaanza kuingia katika kila hoteli na kuanza kuwatafuta Wamarekani. Wamarekani wengi walikamatwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana.
Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Iraq kilifanyika kimyakimya. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifahamu juu ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo. Kila siku Wamarekani walikuwa wakitekwa na kupelekwa katika sehemu zisizojlikana kabisa.
“Hoteli zote tumemaliza mkuu. Tumewapata Wamarekani mia nane” Bhazir alimwambia kiongozi wao, Ashraf
“Mmekwenda katika kila hoteli?” Ashraf aliuliza.
“Ndio Mkuu”
“Na hapa Baghdad, mmemaliza hoteli zote?”
Bhazir hakutoa jibu lolote lile, alikaa kimya kwa muda huku akionekana kufikiria kitu. Baada ya sekunde kadhaa, akauinua uso wake na kumwangalia kiongozi wake.
“Kuna hoteli moja hatukuingia” Bhazir alijibu.
“Hoteli gani?”
“Majifallus Hotel”
“Kwa nini?”
“Kuna ulinzi mkubwa mkuu”
“Hata kama kuna ulinzi, hakikisheni mnakwenda na kuwateka Wamarekani wote. Kama mkiona mnashindwa, tumieni bunduki” Kiongozi yule alisema.
Kwa haraka sana pasipo hata kupoteza muda wowote ule, Bhazir akatoka ndani ya chumba kile na moja kwa moja kuanza kupiga hatua kuelekea nje. Akawachukua vijana kumi waliokuwa na bunduki mikononi mwao na kuanza kelekea katika hoteli ya Majifallus.
“Kama kuna yeyote atakataa, tumuueni huko huko hotelini. Mmenielewa?”
“Ndio” Vijana wale waliitikia huku wakiwa wamebakisha hatua themanini kuingia ndani ya eneo la hoteli ile aliyopanga Emanuel, Brian, mchungaji Joshua na mkewe.
“Are we going to leave this place? How? (Tutaondoka mahali hapa? Kivipi?)” Mzungu mmoja aliuliza.
“I don’t know but you have to trust me that we are going to leave this place very soon (Sijui lakini inabidi mniamini kwamba tutaondoka ndani ya chumba hiki hivi karibuni)” Mchungaji Joshua aliwaambia.
Maneno ambayo alikuwa ameyaongea yakaonekana kuinua matumaini ndani ya mioyo ya wazungu wale lakini swali lilikuwa moja tu kichwani mwao kwamba ni kwa namna gani wangeweza kuondoka ndani ya chumba kile ambacho hakikuwa chumba cha amani kabisa katika maisha yao. Kitu ambacho walitakiwa kukifanya kwa wakati huo ni kuamuamini mchungaji Joshua maneno ambayo alikuwa amewaambia.
Baada ya dakika kumi, Waarabu nane wakaingia ndani ya chumba hicho na kuanza kuwaangalia mateka wote. Kwa wakati huu walikuwa wameingia kitofauti sana, mikononi hawakuwa na bunduki kama ambavyo walivyokuwa wakiingia katika kipindi cha nyuma, katika kipindi hiki walikuwa na majambia pamoja mapanga huku wengine wakiwa na visu.
Ukiachilia silaha hizo, kulikuwa na mwarabu mwingine ambaye alikuwa ameshika kamera pamoja na vifaa vingine ambavyo vilikuwa vikitumika katika upigaji picha. Tayari akili yao ilikuwa imepata majibu juu ya kitu kile ambacho kingekwenda kutokea mahali hapo, kuchinjwa kama wanyama huku picha za video zikichukuliwa. “Pakua KULAYA SIMULIZI APP ipo play store”
Baadhi ya wazungu wanne wakainuliwa na kisha kuvalishwa vitambaa vyeusi usoni mwao na kuanza kupelekwa nje ya chumba kile. Kila mtu kwa wakati huo alikuwa akipiga kelele za kutaka watu hao waachiwe lakini Waarabu wale hawakuonekana kujali kabisa, walichokuwa wakikitaka ni kuondoka na wazungu hao na kufanya kile ambacho walikuwa wakitaka kukifanya.
“They are going to slaught them (Wanakwenda kuwachinja)” Mwanaume mmoja alisema huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Please! Lets pray for them (Tafadhali! Tuwaombeeni)” Mchungaji Joshua alisema na kisha wote kwa pamoja ndani ya chumba kile kushikana mikono na kuanza kuwaombea wale wazungu ambao walikuwa wamechukuliwa na kupelekwa nje, mahali ambapo walijua fika kwamba walikuwa wakielekea kuchinjwa.

Kwa harakaharaka Brian akapiga hatua na kuanza kuchungulia nje kupitia mlangoni, Waarabu wanne waliokuwa na bunduki walionekana wakiongea na Waarabu wale ambao walikuwa wakikaa ndani ya ile nyumba. Japokuwa walikuwa wakiongea Kiarabu lakini Brian alikuwa akiwasikia vizuri kabisa, alichokifanya ni kumgeukia Emanuel na kumwambia kwamba iliwapasa kuondoka mahali hapo.
Wote wakatoka chumbani na kuelekea upande ambao hakukuwa na mtu yeyote. Mwendo wao ulikuwa ni wa harakaharaka sana, hawakutaka kuchelewa, walihitaji kufanya kila kitu kwa kasi kubwa. Walipotokea upande wa pili, wakasikia kwa mbali mlango wa chumba walichokuwa wakikaa ukifunguliwa.
Hapo ndipo walipofanya haraka zaidi. Ngamia kadhaa waliokuwa wamefungwa sehemu mbalimbali katika maeneo hayo walionekana kutaka kuharibu kila kitu mahali hapo. Kwa sababu walikuwa ni wageni na ngamia walikuwa wakifahamu harufu za wenyeji wao, walikuwa wakipiga kelele ambazo zilikuwa zimewashtua Waarabu wale ambao walikuwa ndani.
Kwa mwendo wa kasi wakazidi kukimbia kuelekea katika sehemu iliyokuwa na magari mawili aina ya Land Rover.
Walipoyafikia magari yale, Brian akakipiga kioo kwa kutumia jiwe alilolishika na kioo kuvunjika na kisha kuingia ndani. Muda wote Emanuel alikuwa akishangaa, mwandishi mwenzake wa habari, Brian alionekana kuwa mtu hatari sana kwa wakati huo, hakujua mambo hayo yote alikuwa amefundishwa wapi.
“Hatuna funguo” Emanuel alimwambia Brian.
“Subiri. Kazi ndogo sana” Emanuel alimwambia Brian.
Kwa kasi ya ajabu, Brian akafungua sehemu iliyokuwa katika sehemu ya ufunguo na macho yake kukutana na nyaya mbalimbali zisizopungua kumi. Akaanza kuzichukua yanya moja baada ya nyingine, alipozishika nyaya alizokuwa akizihitaji, akazikata na kuanza kuziunganisha.
Mpaka katika kipindi hicho, Brian akaonekana kuwa komandoo au mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi sana ambayo Edmund hakuwa akiyafahamu.
Waarabu wale waliokuwa ndani wakatoka nje na kuanza kuelekea kule ambapo kulikuwa na magari yale. Brian alifanya vitu kwa haraka sana, mara gari likaanza kushtuka shtuka na hatiame kuwaka. Brian akashikilia uskukani na kisha kuingiza gia na kuliondoa gari mahali hapo katika kasi ambayo ilionekana kumshangaza Emanuel ambaye alikuwa haamini kile kilichokuwa kikitokea mahali hapo.
“Unanichanganya. Hivi kweli wewe kweli ni mwandishi wa habari?” Emanuel alimuuliza Brian.
“Utajua tu. Cha kwanza twende hotelini” Brian alimwambia Emanuel.
“Kufanya nini?”
“Kuchukua begi langu. Kazi inaanzia mahali hapa. Tayari tumechokoza vita na wao, ni lazima tuvimalize hata kabla hatujaelekea nchini Marekani” Brian alimwambia Emanuel huku akiendesha gari kwa kasi.
“Vita! Tumeanzisha vita?” Emanuel aliuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo. Hatuna budi kupambana kwa sasa. Unajua kutumia bunduki?” Brian alimuuliza Emanuel.
“Hapana.”
“Nitakufundisha”
“Mpaka sasa hivi umekwishanichanganya”
“Usichanganyikiwe kwa sasa. Kazi yako kama mwandishi wa habari imekwishaisha. Imebakia kazi yangu tu” Brian alimwambia Emanuel maneno ambayo yalionekana kumshtua zaidi.
“Bado unanichanganya”
“Usiwe na pupa. Utajua kila kitu. Twende hotelini kuchukua begi langu. Baada ya hapo nitakwambia kila kitu” Brian alimwambia Emanuel huku tayari wakiwa wanaana kuuacha mji huo wa Wassit uliokuwa katika jiji hilo la Baghdad.
***** “Pakua KULAYA SIMULIZI APP ipo play store”
Bado safari ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi. Mwendo ulikuwa ni wa kasi sana kiasi ambacho Emanuel aliona muda wowote ule walikuwa wakienda kupata ajali. Barabara ilikuwa mbaya, mashimo ambayo yalikuwa barabarani yaliifanya gari lile kudundadunda muda wote wa safari.
Kichwa cha Emanuel bado kilikuwa kikimfikiria Brian, kitendo cha kujitambulisha kwamba alikuwa mwandishi wa habari huku akiwa amefanya mambo mengi ya hatari kilionekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Maswali yalikuwa yakizidi kumiminika kichwani mwake, alitamani sana kuuliza lakini kwa hali ambayo walikuwa nayo katika kipindi hicho hakuona kama lingekuwa jambo la busara kufanya hivyo.
Baada ya dakika kadhaa wakawa wamekwishafika katika hoteli ya Majfallus. Polisi wengi pamoja na waandishi wa habari walikuwa mahali hapo huku wakiangalia namna hali ilivyokuwa mbaya. Miango mingi ilikuwa imevunjwa, kila mhudumu ndani ya hoteli ile alikuwa akizungumza lake kuhusiana na uvamizi ule ambao ulikuwa umetokea.
Brian na Emanuel wakateremka kutoka garini na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo la hoteli ile. Polisi waliokuwa mahali pale wakajaribu kumzuia lakini mara baada ya kujitambulisha kwamba walikuwa miongoni mwa wateja waliopanga ndani ya hoteli ile, wakawaruhusu kuingia.
Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika chumba alichokuwa akikaa Brian. Hakukuwa na mlango, mlango ulikuwa umevunjwa kama ambavyo ulivyokuwa katika kipindi kilichopita wakati ambao Waarabu wale walipokuja kuwateka baadhi ya wazungu ambao walikuwa wamepanga ndani ya hoteli ile.
Brian akaanza kulifuata begi lake, alipolifikia, akalichukua na kuliweka kitandani. Muda wote Emanuel alikuwa kimya akimwangalia tu, bado maswali mengi yalikuwa yakiendelea kumiminika kichwani mwake juu ya Brian ambaye wala hakuwa akieleweka vizuri kwake. Macho yake yakahamia katika begi lile aliloliweka Brian pale kitandani.
Brian akalifungua begi lile, nguo zilikuwa zikionekana kwa juu, akaitoa fulana moja ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiarabu ambayo yalimaanisha ‘TUMUABUDU ALLAH’ na kisha kuivaa. Akazitoa nguo nyingine na macho ya Emanuel kutua katika bunduki tatu ambazo zilikuwa na vyombo vilivyokuwa na sauti ya kuzuia mlio wa risasi.
Emanuel akashtuka kupita kawaida, tayari kichwa chake kikatambua kwamba Brian alikuwa mtu hatari sana na wala hakuwa mwandishi wa habari kama ambavyo alijitambulisha kabla. Brian akazitoa bunduki zile zote na kisha kuziweka kiunoni mwake.
“Who are you? (Wewe ni nani?)” Emanuel aliuliza huku akionekana kuhofia.
“We don’t have enough time for conversation, we have to leave (Hatuna muda wa kutosha wa mazungumzo, tuondoke)” Brian alimwambia Emanuel.
Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kwenda kwenye chumba alichopanga Emanuel na kisha kuchukua begi lake. Katika kila kitu ambacho kilikuwa kikifanyika mahali hapo kilikuwa kikifanyika kwa harakaharaka. Hakukuwa na muda wa kupoteza hata mara moja, tayari maisha yao yalionekana kuwa katika hatari kubwa.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa katika upande wao nchini humo, walitakiwa kujitetea wao kama wao. Wakaanza kutoka nje na kuelekea kule ambapo walikuwa wamelipaki lile gari ambalo walikuja nalo, Brian alipoangalia vizuri katika eneo lile, macho yake yakatua katika gari ambalo alikuwa ameliona kabla ya kufika mahali hapo. Akamsimamisha Emanuel.
“What is happening? (Nini kinaendelea?)” Emanuel aliuliza huku akionekana kushtuka.
“They are here (Wapo hapa)”
“I don’t get you. Who is here? (Sijakupa. Nani yupo hapa?)”
“Kidnapers (Watekaji)” Brian alijibu.
Akaanza kuyapeleka macho yake huku na kule, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuweza kuingia ndani ya gari lile, ushauri ambao alikuwa ameutoa mahali hapo ni kuondoka kwa miguu kutafuta sehemu nyingine huku ikiwa imetimia saa sita usiku.
Wakaanza kutembea kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na majengo kadhaa ya ghorofa huku watoto wengi wa mitaani wakionekana katika eneo hilo. Mwendo wao ulikuwa ni wa harakaharaka sana. Walipogeuka nyuma, watu watano walikuwa wakiwafuata huku wakiwa wamevalia kanzu kubwa. Brian akaiinua fulana ile aliyokuwa ameivaa na kisha kuchomoa bunduki na kuishika mkononi mwake.
Hakukuwa na amani kabisa, tayari muda wa vita ukaonekana kuingia. Kutokana na kuwa na idadi kadhaa ya watu katika mitaa ya hapo walipokuwa pamoja na msikiti mkubwa kuliko misikiti yote jijini Baghdad, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alithubutu kupiga risasi. Bado waliendelea kwenda mbele ambapo Brian akamwambia Emanuel ulikuwa ni wakati wa kukimbia kwa ajili ya kuziokoa roho zao.
Walipoona kwamba wameupita msikiti na kuuacha kwa umbali wa mita mia moja, hapo hapo milio ya risasi ikaanza kusikika. Brian hakuonekana kuwa na wasiwasi kabisa, alizidi kukimbia pamoja na Emanuel mpaka kufika sehemu ambayo ilikuwa na ghorofa moja na kumwambia Emanuel asimame nyuma ya ukuta ule.
Brian akaishika bunduki yake na kisha kuanza kumlenga mmoja baada ya mwingine. Kutokana na bunduki zile kuwa na vyombo vya kuzuia mlio wa risasi, wakajikuta mmoja baada ya mwingine wakianguka chini bila kusikika sauti yoyote ambazo zingewafanya kujificha. Ni ndani ya dakika moja, Waarabu wote watano walikuwa chini huku damu zikiwatoka.
“Hivi ni vita. Wewe baki kama mwandishi. Umesikia?” Brian alimuuliza Emanuel ambaye alijiona kuishi na roho mkononi.
“Sawa” Emanuel aliitikia huku akitetemeka.
Walipoona kwamba Waarabu wote walikuwa chini, wakatoka kutoka katika sehemu ile na kisha kuanza kuifuata miili ile na kuanza kuiangalia. Damu zilikuwa zimetapakaa katika eneo zima mahali pale. Kila kitu kikaonekana kwenda sawa mahali hapo. Huku wakiwa wanaendelea kuiangalia miili ile, mara wakaanza kusikia sauti za watu ambazo zilikuwa zikiwataka kutokufanya kitu chochote mahali hapo. “Pakua KULAYA SIMULIZI APP ipo play store”
Brian alipotaka kugeuka kuona ni walikuwa ni watu gani, milio ya risasi ikasikika na risasi kudhaa kupiga ardhni. Brian akatakiwa kuweka bunduki zake chini na kufanya hivyo.
Huku wakisubiria kuona ni kitu gani wangeambiwa au hata kuziona sura za watu wale waliokuwa nyuma yao, wakashtukia wakipigwa na vitako vya bunduki kichwani…. Whatsapp +255 758 018 597

Post a Comment

0 Comments