Riwaya - Yamotokale (18+)

Whatsapp 0758 018 597
Usiku wa siku hiyo, Os Anjelus hakupata usingizi aliouzoea kule alikohama. Ni kawaida, watu wengi hukosa mtiririko mzuri wa usingizi wanapolala eneo geni…

“Iko haja ya kumwita mke wangu sasa. Si nilimpeleka nyumbani ili nitafute chumba kingine? Si nimeshakipata? Sasa nini tena?

“Lakini loh! Yule mama mwenye nyumba kule nilikohama kiboko. Mama mdomo mchana kutwa! Uchafu kidogo wa kuufagia sekunde kumi yeye anafoka nusu saa? Sijawahi kuona mimi.

“Sasa kwa mfano siku ile alipotupa notisi kwa ule uchafu wa kuufagia dakika mbili tu kama nisingemtishia kwenda polisi, si angeongea siku nzima?” aliwaza Os Anjelus huku akihisi kizunguzungu cha ugeni, lakini msisitizo wake mkubwa ndani ya moyo ni kumwita mkewe, Happy.

***
Asubuhi kulikucha, Os Anjelus alikuwa wa pili kutoka nje. Wa kwanza alikuwa mama Tina, baada ya yeye ndiyo akatoka Halima ambapo alimtengea maji ya kuoga mwanaume aliyerudi naye usiku uliopita.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa Halima kuonana uso kwa macho na Os Anjelus kiasi kwamba, mwanzoni Halima alijua ni mgeni wa mama Tina…
“Za leo anko?”

“Nzuri sista, mzima wewe?”
“Mzima, karibu sana.”
“Asante nimekaribia.”

Lakini Halima hakumuuliza Os Anjelus kama yeye ni nani kwenye nyumba ile, aliogopa kuonekana ni ‘mshankupe’ wa mtaa.
Kila mmoja aliendelea na lake, Os Anjelus aliingia chooni, Halima alitenga maji akaenda ndani kumwita jamaa yake, anaitwa Mabange.

***
Halima alitoka na Mabange kwenda kwenye saluni yake, kwenye korido akakutana na mama Tina…
“Za asubuhi mama Tina?”
“Nzuri Halima, umeamkaje?”
“Salama tu,” alisalimia Tina, akapunguza sauti…

“Eti huyu kijana ni nani, mgeni wako?”
“Mgeni wangu?! Aka! Si mpangaji mpya aliletwa na mwenye nyumba juzi.”
“Ooo, kwa sababu sikuwepo. Anafanya kazi wapi?”

“Mi sijui Halima.”
“Ana mke?”

"Halima, mimi sijui lolote."
"Ana gari?"
"Halima bwana, mi sitaki," alisema mama Tina huku akiondoka kwa mwendo wake wa madaha.
Halima aligeuka kumwangalia huku akimtamani maana japokuwa ni mwanamke mwenzake lakini moyoni amekuwa akikiri kwamba, mama Tina aliumbika kuliko yeye.

Mama Tina alijaliwa. Kwenye bodi nyuma alikuwa amefungashia, kiuno kilikatika vizuri, japokuwa alishazaa mtoto mmoja lakini bado nido zake zilikuwa zinadai kama za binti aliyeingia ukubwa.
Mviringo wa miguu yake na kuitwa jina la bia lilimfanya azidi kutamanika hata machoni pa wanawake wenzake. Sura yake ilijaliwa duara lenye upole na macho ya kulewa huku midomo ikishibishwa na unene wa rangi nyeusi.

Sauti ya mama Tina ilikuwa na uwezo wa kuwafanya wananchi wenye hasira kali wamsamehe kumchoma moto kibaka aliyemkwapulia simu mzee maarufu wa mtaa.
Siku mojamoja, hasa Jumapili alipokuwa akienda kanisani, aliwaacha hoi watu wa mtaani kutokana na magauni yalivyokuwa yakimkaa.

Umri wake wa miaka 32 ulimtosha kuendelea kuonekana msichana mbichi kutokana na kujitunza na kujaliwa ngozi nzuri na Muumba.

***
Asubuhi iliyofuata, Os Anjelus alitoka chumbani kwake na kukutana na mama Tina kwenye korido
"Za asubuhi anko?"
"Nzuri anti, umeamkaje?"
"Salama tu. Naona kumekucha?"

"Ee, kumekucha anti, nataka kufua kwanza halafu ndiyo niende kibaruani."
"Pole sana. Ungetafuta mtu wa kukusaidia kazi kama hizo anko."
"Ni kweli, unajua nina mke lakini yupo kwao, nadhani mwisho wa mwezi huu atakuja."
"Hapo itakusaidia."

Mazungumzo yao yalitumia kama dakika moja, kila mmoja akaendelea na mambo yake.
Baba Tina aliondoka kwenda kazini, Os Anjelus alikuwa amemaliza kufua na sasa alikuwa akijiandaa kwa kutoka
"Ngongo;ngo," mlango wake uligongwa.
"Karibu," alisema kijana huyo huku akifungua mlango

"Oo anti, karibu."
Mama Tina mkononi alishika sinia lenye chupa ya chai, sukari, kikombe na vitafunwa
"Karibu chai anko."
"Ooo. Anti mbona unasumbuka jamani?"
"Usijali anko, we kunywa tu."
"Asante sana."

Os Anjelus alipokea sinia hilo na kurudi ndani kwake, akanywa chai na kurudisha vyombo
"Anti vyombo hivi."
Mama Tina alitokea, akapokea sinia lake huku akishukuru
"Baadaye basi anti."

"Sawa anko, nilikuwa na wazo moja anko. Ungeacha funguo nikufanyie usafi chapuchapu."
"Hapana nitafanya mwenyewe anti, nisikusumbue."
"Noo, hunisumbui anko, we acha tu."
"Jamani, nitakuchosha anti."
"Wala ndiyo kazi zetu akina mama tukiwa nyumbani."

Os Ajelus aliacha funguo, mama Tina akaipokea na kuifunga kwenye pindo la khanga aliyovaa.
Nusu saa mbele, mama Tina alikuwa ndani ya chumba cha Os Anjelus akifanya usafi. Baadhi ya vitu havikuwa vimepangwa, akapanga yeye alivyoweza huku moyoni akimsifia kijana huyo kwa kuwa na vitu vizuri na vya kisasa.

Alibabaika zaidi kwenye kitanda na mashuka. Ilifika mahali alijitupa kitandani na kunesanesa huku moyoni akisema
"Kinaonekana kinatoa usingizi mnono."


********************************



"Nimekuletea chakula anko," mama Tina naye alitumia sauti ya chini.
"Da! Asante sana anti."
Wakati Os Anjelus anapokea, sauti ya Halima mlangoni ilibisha hodi
"We kaka wa Kingoni."

Ukimya ulitawala kwa muda kwani Os Anjelus alishindwa kuitikia kutokana na uoga kwamba angeingia angemkuta mama Tina
"Wenyewe humu ndani, hodini," alikomaa Halima.

"Sikia, nenda, fungua mlango lakini usimruhusu aingie ndani hata sekunde moja," mama Tina alimwambia Os Anjelus kwa sauti ya chini sana ili asisikie Halima kule mlangoni.
"Sawa," Os Anjelus alikubali huku akienda kufungua mlango. Mama Tina akijibana kwenye kona ya chumba ili asionekane maana mlangoni hapakuwa na pazia.
"Vipi we Mngoni, mzima?"

"Mzima dada angu, karibu sana."
Mama Tina kule ndani aliposikia karibu sana, alishtuka sana, alijua kijana huyo atamruhusu Halima apite kuingia
"Mwenzetu ujio wako kufahamiana ni muhimu, ulikuwa ukiishi wapi zamani?"
"Mburahati."
"Una mke?"

"Nina mke na mtoto mmoja."
"Wako wapi sasa?"
"Wako kijijini."
"Watakuja lakini?"
"Mwisho wa mwezi huu watakuwa hapa."

"Sawa, sasa unakula nini maana napika."
"Hapana anti, usijali kuhusu suala la chakula, mi tayari."
"Kwani unapika humu ndani?"
"Nakula gengeni."
"Hivi hiki chumba ni kikubwa kweli?" Hebu nione ndani," Halima alisema akionesha dalili za kutaka kuingia kwa kuinua mguu mmoja na kukanyaga mbele.
"Sista samahani, iko siku utaingia lakini si leo," alisema Os Anjelus huku akiinamia chini kwa aibu.
"Yaani mimi kuingia kwako anko mpaka unipangie siku, unajua ni kwa kiasi gani nimekupenda?" Halima alipasua jipu kwa mara ya kwanza
"He!" kule ndani mama Tina alijikuta akisema kwa sauti ya mshangao
"Yaani mwanamke anajitongozesha hivihivi, ama kweli Halima ni malaya sana jamani," alisema mama Tina lakini huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi.
"Sista utanipendaje wakati nimekwambia nina mke wangu? Mimi hapa ndani hakuna mwanamke nitakayetembea naye kwa sababu kati ya mambo siyataki ni pamoja na usaliti."
"Ina maana hujawahi kumsaliti mkeo?"

"Na wala sina wazo hilo."
"Basi mwenzetu kumbe ana bahati ya mtende, kuota jangwani."
Mama Tina alimsifia kijana huyo, hasa kwa msimamo wake aliouonesha kwa Halima kwamba hawezi kumsaliti mke wake.

Halima aliondoka, Os Anjelus akafunga mlango kwa funguo na kurudi, akakaa kitandani huku akimwangalia mama Tina kwa macho ya huruma kwa jinsi alivyokuwa amejibanza kwenye kona
"Pole sana anti."
"Usijali anko, kawaida tu. Unajua huyu msichana ana mdomo sana, angeniona hapa angekwenda kuyatangaza nje."

"Ni kweli kabisa, umetumia busara kushauri asiingie."
"Sasa mi nitatokaje humu?" alihoji mama Tina.
"Ngoja nitoke mimi niangalie hali ya hewa."
"Sawa."
"Mama Tina," aliita Halima kule nje..
"We mama Tina."

Mama Tina aliogopa zaidi, alijua Halima ataingia kwake na atamkuta mtoto. Na ikawa hivyo kweli
"We Tina mama yuko wapi?"
"Katoka."
"Kaenda wapi?"
"Sijui, aliweka chakula kwenye sufuria akatoka."
Tina alijua hotipoti ni sufuria.
Halima alishtuka kusikia mama Tina aliondoka na sufuria yenye chakula
"Kaenda nacho wapi? Atakuwa kampelekea yule kijana."
***
Wiki moja tu mbele, siku hiyo mama Tina alikuwa akitoka gengeni, akakutana na mama mmoja jirani yake anaitwa mama Sindilia.

"Nilikuwa nakutafuta sana mama Tina."
"Kuna nini tena mama Sindilia."
"Mwenzangu si umbeya wa mtaani, uhujui?"
"Upi huo mama Sindilia."

"Nasikia unatembea na kijana mpangaji mwenzenu ndani."
"Eti nafanyaje?"
"Nasikia kuna kijana mmoja kahamia kwenu, ndiyo unatoka naye. Nikasema mama Tina huyuhuyu ninayemjua mimi anaweza kufanya upuuzi huo kweli?"

Ha! Mama Sindilia, unavyoona naweza kufanya upuuzi kama huo kweli, mimi mama Tina? Na ndoa yangu tamu?"
"Ndiyo nikashangaa. We hujasikia?"
"Sijasikia kokote."

"Basi kaa ujue hivyo."
"Wewe nani kakwambia?"
"Mh! Mwenzangu hayo mengine sana, tutaonana siku nyingine," alisema mama Sindilia huku akiondoka zake.

Mama Tina nusura presha impande kwani watu wa mtaa ule anawajua vizuri, si ajabu kumwambia mume wake kuhusu tetesi hizo jambo ambalo litamuweka pabaya.
"Hivi atakuwa nani? Au Halima? Huyu atakuwa Halima tu," alisema moyoni mama Tina wakati akiingia nyumbani kwake.

Licha ya kuwepo kwa madai hayo, mama Tina alitafuta muda wa kuonana na Os Anjelus ili amsimulie habari za mtaani.
Ilikuwa wakati kijana huyo amerudi, kabla hajaingia kwake, mama Tina alimdaka kwenye korido
"Anko kuna kitu kikubwa sana na cha hatari kinataka kutokea."

"Kinahusu nini anti?"
"Mimi na wewe."
"Nini tena anti?"
"We nenda, usifunge mlango nitakuja kukwambia."
"Poa."

Os Anjelus alizama chumbani mwake, akapumzika kidogo kisha akatoka kwenda kuoga, aliporudi alivaa bukta tu na kujitupa kitandani huku akiwa amefungulia feni kwa spidi ya kawaida.
Mama Tina alimalizana mambo yake, akatembea kuelekea kwa kijana huyo huku akiwa katika hali ya tahadhari. Kabla ya kuingia alimpigia simu Halima akiwa amesimama usawa wa mlango wa chumba chake
"Halina leo unarudi saa ngapi nataka kukuagiza kitu."
"Mh! Kusema ukweli nitachelewa sana, kuna sehemu nitakwenda kujirusha, labda kwenye saa sita, saba usiku. Ulitaka kuniagiza nini?"
"Sabuni."

"Labda nikununulie nikupe asubuhi."
"Hapana, nitakwenda kununua pale kwenye duka la urembo la kisimani."
"Poa."
Mama Tina akaondoa wasiwasi, maana alidhani Halima angeweza kuingia muda wowote ule. Alizama ndani kwa Os Anjelus.

"Vipi, naona umelala?"
"Nimepumzika tu anti, si unajua tena."
"Ni kweli," alisema mama Tina akikaa pembeni ya kitandani, akashika godoro kulia na kushoto kama anayetaka kuaga kuondoka.

"Mwenzangu, leo nimekutana na mama mmoja jirani, akasema amesikia eti mimi natembea na wewe, he! Nilishangaa sana, mimi sijawahi kupata kashfa kama hiyo hata siku moja katika maisha yangu ya ndoa."
"Mh! Kweli? Yeye huyo mwanamke alisikia wapi?"
"Kagoma kuniambia, lakini mimi nahisi Halima."
"Halima yupi, huyu dada wa chumba cha pili?"
"Huyohuyo."

"He! Mbona anataka kuleta balaa."
"Balaa balaa, tena ni uuaji, maneno kama hayo yakifika kwa mume wangu si ndoa sina!"
"Kabisa anti. Dah! Ni wa kumwonya lakini."

"Mh! Mimi sitamwambia kitu, ila Mungu atanilipia, iko siku yake. Mi najua anakutaka ndiyo maana anafanya hivi, yeye anadhani mimi na wewe ni wapenzi," sasa mama Tina alianza kupunguza sauti. Akaendelea
"Tena naomba anko, isije ikatokea hata siku moja umekaa naye ukasema ninavyokusaidia kusafisha nyumba au kukupa chakula

"Anti, mi si mtoto, siwezi hata siku moja
"Unanihakikishia anko?"
"Kweli kabisa."
"Mh! Tushikane mikono tule kiapo."

Os Anjelus akatoa mkono, mama Tina akaupokea, akaubana;
"Ukikiuka itakula kwako."
"Siwezi kukiuka."
"Kweli?"
"Kabisa."

"Siamini," sasa mama Tina alimsogelea usoni kijana huyo;
"We amini."
"Nifanyie kitu chochote niamini," alisema mama Tina.
"Unataka nikufanyie kitu gani?"
"Chochote ambacho mimi nitaamini kweli hutaweza kuanika siri yetu."
Os Anjelus akashtuka,

Fika whatsapp +255 758 018 597 (1000Tsh utaipata ikiwa kamili)

Instagram @kulayasimulizi

Post a Comment

0 Comments