Riwaya - Siitaki Yako (Utamu 18+)
“Ee Mungu mlinde mume wangu huko aliko, arudi salama, mengine tutayajulia hapahapa,” alinong'ona kwa uchungu. “Kama kweli amekumbwa na matatizo, nd'o tutajua. Mradi tu arudi salama,” alisema hayo akiwa amejilaza kitandani, saa 11:30 alfajiri, hasira zikizidi kumpanda.

Saa 12.30 akasikia mlango ukigongwa. Akashtuka na kujitoa kitandani. Akajitanda kanga na kuufuata mlango.

“Tonny! Tonny!” Lilian alinong'ona kwa hasira, macho yake mekundu yakimtazama Tonny kwa shari. “Tonny...Baba...” sauti ikamkwama. Akabaki akimtazama Tonny bila ya kupepesa.

Macho yao yaligongana. Kwa sekunde chache wakawa wakitazamana kama majogoo, kila mmoja akihema kwa nguvu. Tonny akajipa ujasiri wa aina yake, ujasiri uliomfanya ajikute akiwa na uwezo wa kumjibu Lilian.

Akaingia ndani huku akifoka, “Acha kushangaa-shangaa ovyo. Zungumza kitu kinachoeleweka sio unakalia kunitumbulia mimacho ka' vile umeona kitu kigeni.We vipi?”

Lilian hakujibu. Alimpisha mlangoni na kubaki akimsikiliza huku akimsindikiza kwa macho. Kilichomshtua na kumshangaza Lilian ni manukato makali ya mumewe yaliyokijaza chumba hicho. Humo ndani walikuwa na chupa mbili za manukato, lakini sio manukato ya aina hii.

Haya manukato yaliyotoka mwilini mwa Tonny yalikuwa makali, na Lilian alijua ni ya thamani ya kiasi gani. Lakini hakuwa na haraka. Hakutaka kuchukua pupa. Alimwacha aingie ndani akidhamiria kufanya mambo kwa utaratibu na sio kuyamwaga hadharani kwa masikio yasiyohusika.

Baada ya Tonny kuingia, Lilian naye akamfuata huku akiufunga mlango nyuma yake. Akamtazama Tonny ambaye sasa alikuwa akivua nguo na kuvaa taulo.

“Tonny,” Lilian alimwita kwa sauti ya chini.

Tonny hakuitika. Alitwaa sabuni na kuanza kuufuata tena mlango.

“Tonny, si nakuita?”

“Subiri kwanza nikaoge,” lilikuwa ni jibu la Tonny.

Lilian bado hakuwa na makuu. Alimpisha na kumwacha akielekea bafuni. Alipobaki peke yake chumbani, aliketi kitandani na kujiinamia kwa huzuni. Akajiuliza ni kipi alichomkosea Mungu? Hakuiona raha ya ndoa yake. Wala hakuiona faida ya kuolewa. Machozi yakachuruzika mashavuni na kusahau kuyafuta.

Mara akakurupuka na kuzifuata nguo za Tonny. Akazishika na kuzisogeza puani. Ile harufu kali ya manukato ikajidhihirisha katika shati. Kwa hasira akazitupa kitandani huku akisonya. Akaendelea kujiinamia.

Tonny aliporejea kutoka bafuni alimkuta bado kajiinamia. Hakumshtua, alifungua kabati na kutoa nguo nyingine. Akawa katika zoezi jingine za kubadili mavazi. Ilionekana kuwa alitarajia kutoka tena asubuhi hiyo.

“Tonny,” kwa mara nyingine Lilian alimwita, sauti yake ikitoka kwa shida. Hatimaye akaamua kumwita kwa jina mtoto wao. “Baba Sambe unanisikia au ndiyo dharau yenyewe?

“Unasemaje?” sasa Tonny alisitisha kila alichokuwa akikifanya. Akamtazama mkewe kwa macho makali.

“Una matatizo gani?” Lilian alimuuliza, safari hii naye akimkazia macho.

“Kivipi?”

“Haueleweki-eleweki. Unataka kuniambia nini kuhusu wewe kulala nje leo?”

“Hilo siyo tatizo,” Tonny alijibu kwa kujiamini. “Najua umeshawaza kuwa nimelala kwa mwanamke. Sishangai, ni kawaida ya wanawake wengi kuwaza hivyo pale mume anapotokea kurudi nyumbani asubuhi.”
 Instagram  @kulayasimilizi
“Tonny! Usinifanye mie chizi au mtoto mdogo!” Lilian aliwaka. “Nimechoka. Nimechoshwa na tabia yako. Hivi una mawazo gani wewe? Yaani hujijali wala huogopi Ukimwi!”

Tonny hakuonyesha kujali. Aliendelea kujiandaa, na sasa alikuwa akijitazama kwenye kioo huku akijifuta uso kwa leso. Hali ya kuonekana kutoyajali maneno aliyoambiwa ilimkera sana Lilian.

Akasonya huku akinyanyuka. Akatwaa mswaki na kwenda nje kusafisha kinywa. Dakika kadhaa baadye akarejea na kutwaa sabuni kisha tena akatoka. Sasa alikwenda bafuni kuoga.

Akiwa huko bafuni bado hasira zilimtawala kwa kiwango kikubwa, lakini ikafikia wakati akahisi mzigo ukimtoka. Akacheka kwa sauti ya chini, kicheko kisichokuwa na chembechembe zozote za furaha lakini kilichomtia faraja kwa kiasi fulani.

Alipotoka bafuni alifikia chumbani ambako hakujali Baba Sambe anafanya nini. Jambo jingine ambalo lilimfanya afarijike ni kutokuwapo kwa mwanaye, Sambe aliyekuwa na umri wa miaka mitano. Mtoto huyo alikuwa Arusha kwa mjomba wake. Angerudi baada ya miezi minne au mitano.

Hivyo, Lilian alijiona kuwa ana uhuru zaidi ya uhuru wa kawaida. Papohapo akatwaa mafuta na kuanza kujipodoa. Hakujali wakati huo mumewe atakuwa anafanya nini, alijali kukamilisha alichokuwa akikifanya. Kisha akatwaa suruali nyeusi, nyepesi ambayo mara nyingi alishindwa kutoka nayo kutokana na ilivyokuwa ikimshika sana makalio. Leo akaivaa na kufuatisha ‘tisheti’ nyeupe juu.

Hakuweza kutoka hivyo alivyo, bado alijali heshima kwenye macho ya watakaomtazama huko nje. Hivyo, alitwaa kanga na kujifunga kifuani; akiichukulia hatua hiyo kuwa itamsitiri kidogo kutokana na mnyumbuliko na mtimbwiliko wa hayo makalio yake manene.

Alilijua umbo lake lilivyo tata mbele ya macho ya watu hususan wanaume wanaopenda makalio-tinginya, ambao lazima walikuwa wakiguna kila alipopishana nao huku utanukaji wa mapaja yake makubwa ukijidhihirisha bayana na kuwa kivutio kikubwa kwa wanaume waroho.

Sasa akajiona yuko kamili. Akaifuata pochi yake ambako alitwaa noti moja ya shilingi 10,000, akaipachika kwenye pochi yake ndogo. Akatupa macho kitandani na kuiona simu yake. Nayo akaitwaa na kuishika mkononi akiwa ameiviringishia kitambaa.

Sasa akaanza kuvuta hatua akitoka. Alipofika mlangoni aligeuka na kutaka kusema, umeyaanza, wenzio tutayamaliza.’ Hata hivyo alisita kutamka kwa kushtukia kuwa anaweza kuwa amemzindua Tonny.
Akatoka na kuubamiza mlango kwa nguvu nyuma yake.

Tonny aliishia kucheka tu huku sasa akitwaa manukato kabatini na kujipulizia. Hakujali wala kuwaza kuwa ni kwa nini mkewe kamwambia hivyo, alijali burudiko la mwili na faraja aliyoipata kwa Caroline usiku uliopita. Caroline, mwanamke ambaye hadi asubuhi hiyo Tonny aliwaza kama kweli huyo ni mwanadamu wa kawaida aliyezaliwa katika sayari hii au kateremshwa tu kutoka katika sayari nyingine.

Aliwaza hivyo kutokana na pumzi na mbinu mbalimbali alizozimudu kitandani. Caroline aliyajua yote na alikuwa tayari kwa lolote….hakuwa na kinyaa. “Ni kama ananijulia,” alinong’ona akikumbuka jinsi mwanamke huyo alivyomudu staili za ‘MBUZI KAGOMA’ na ‘JIPIMIE MWENYEWE.’

Alizidi kumtukuza Caroline kwa kukumbuka kuwa alipenda sana kulishika ‘gunzi’ na kulinyonya kitaalamu huku akigunaguna kwa namna ambayo lazima mwanamume achanganyikiwe.

Dakika tano baadaye alijiona kuwa yuko kamili, na kwamba anaweza kuingia mitaani. Akafungua pochi yake na kuyaangalia masalia ya pesa zake. Akashusha pumzi ndefu baada ya kubaini kuwa zilikuwemo shilingi 50,000 tu.

Kwake, hizo hazikuwa pesa za kutambia kwa siku hiyo. Aliamini hivyo. Akachunguza vizuri ndani ya pochi hiyo ambayo pia kulikuwa na vijikaratasi vidogovidogo. Alikuwa akiisaka kadi yake ya benki.

Akaiona.

Sasa hakuwa na kingine cha kumkalisha humo ndani. Alitoka huku akitembea kwa madaha, akijisikia mwepesi huku pia akiiona dunia kaishika mkononi na wanadamu kawatia mfukoni.

Nani kama yeye?

******


LILIAN alitoka ndani ya nyumba hiyo bila ya kuwa na uelekeo maalum. Alishika barabara hiyo ya Rufiji hadi akaja kukutana na Mtaa wa Swahili ambako alitulia kidogo kisha akaanza kufuata uelekeo wa soko la Kariakoo.

Alitembea kwa kasi na watu wachache aliokutana nao, waliomfahamu na wasiomfahamu, kama kawaida yao walimtazama wakivutiwa na mtikisiko wa matako yake makubwa ambayo licha ya kujitanda hiyo kanga bado ni kama yalimuumbua, yakijitupa huku na kule kwa namna ya kipekee.

Hakujali kutazamwa, waliopiga miluzi, walioguna na waliomsifia wote aliwasikia na kuwaacha kama walivyo. Yeye akaendelea kutembea bila ya wasiwasi japo bado alihisi kitu kikimkera moyoni.

Alizinduka wakati alipokuwa amelikaribia soko. Akausogelea mgahawa mmoja uliokuwa jirani na soko hilo. Akaingia na kuangaza macho huku na kule. Sehemu moja ya mgahawa huo ilikuwa chini na nyingine ilikuwa juu kwenye kijighorofa.

Akaamua kupanda huko ghorofani. Alipofika alikuta watu takriban ishirini ambao baadhi walikuwa wakinywa supu, na baadhi walikuwa wakinywa bia.

Lilian hakujua kama angepaswa kunywa nini au kula nini. Akabaki kaduwaa hadi alipoguswa bega na mhudumu mmoja wa kiume aliyemwambia, “Karibu shangazi. Karibu kiti.”

Lilian alishtuka na kukumbuka kuwa alistahili kuketi na kuagiza chochote. Akakifuata kiti na kuketi. Mhudumu yule wa kiume akamsogelea na kumuuliza, “Tukusaidie nini, shangazi?”

“Kwani kuna nini?”

“Kuna supu, chapati na mtori.”

“Supu ya nini?”
 Instagram  @kulayasimilizi
“Ipo ya kuku, samaki na ng'ombe.”

“Leta supu ya kuku na chapati mbili.”


Mhudumu alipotoka Lilian alitwaa simu yake na kuanza kubofyabofya akilisaka jina fulani. Alipolipata alibonyeza sehemu ya kuita na kutega sikioni na aliposikia ikiita upande wa pili akakata. Alijua kuwa huyo aliyepigiwa atajua ni nani 'aliyem-beep.'
SAMMY alikuwa ni kijana aliyeishi kikapera. Alikuwa amepanga chumba kimoja katika mtaa huohuo wa Rufiji. Nyumba ya tatu tu kutoka pale alipoishi Lilian ndipo Sammy alipoishi.
 Instagram  @kulayasimilizi
Sammy alikuwa ni mtoto wa Mzee Kibutu. Mzee Kibutu alikuwa akifahamiana na Tonny kwa kuwa walikuwa wakifanya kazi pamoja kabla mzee Kibutu hajastaafu.

Ukaribu uliokuwapo kati ya Sammy na Tonny uliwafanya baadhi ya watu wawafikirie kuwa ni wa ukoo mmoja. Ndipo kijana Sammy ambaye wakati huo alikuwa akimalizia masomo katika Chuo cha Biashara alipojikuta akimwita ‘ba’mdogo.’ Hakuwa baba yake mdogo kiukoo bali tu ni sababu ya uhusiano mkubwa uliokuwapo kati ya Tonny na Mzee Kibutu.

Ni baba yake Sammy ndiye pia alimshawishi Tonny aachane na ukapera.
“Oa…oa uheshimike, Tonny,” mzee Kibutu alimwambia Tonny.

Mwaka mmoja baadaye Tonny alikuwa na mke. Na hakuoa, mradi anaoa, alichukua muda kuchagua mwanamke ambaye hata watu wakimwangalia mitaani wakiri kuwa ni mwanamke anayestahili kuitwa mwanamke mzuri.

Ugonjwa wa Tonny ulikuwa ni macho yaliyolegea, midomo iliyonona na makalio makubwa. Kwa mwanamke wa aina hiyo, Tonny hakusikia wala kuambiwa kitu. Ndipo siku moja akakutana na mwanadada huyu mrembo, Lilian, akamwaga sera. Urafiki ukazaliwa. Hatimaye urafiki huo ukazaa uchumba kisha ndoa.

Lilian akawa mke wa mtu, Tonny mume wa mtu. Wakaanza maisha mapya.

Mwaka mmoja baadaye mtoto Sambe akazaliwa, Mama Sambe akazidi kunawiri. Alinenepa, akawa gumzo mitaani.


 Instagram  @kulayasimilizi
*****

Siku moja Lilian alikuwa amebeba fuko la plastiki lililosheheni matunda mbalimbali. Wakatazamana. Sammy akawa mwepesi wa kuachia tabasamu la kirafiki, tabasamu lililomshangaza Lilian kiasi cha yeye pia kujikuta akalijibu tabasamu hilo kwa kuachia tabasamu la mbali.

“Vipi ma’mdogo, naona umetoka kurekebisha mambo ya msosi,” ni neno la awali lililomtoka Sammy huku akimsogelea na kumnyooshea mkono.


Lilian naye alinyoosha mkono. Viganja vyao vikakutana. Sammy akahisi vitu vikimtambaa mwilini kwa msisimko. Hakukumbuka ni lini aliwahi kushika kiganja laini na chenye joto kama hiki. Kiganja cha mwanamke ampendaye! Alihisi mabadiliko fulani mwilini kiasi cha kujikuta akiikosa sauti yake kwa muda.

Lilian na Sammy hawakuwa na mazoea sana. Lilian alimtambua vizuri Sammy kuwa ni mtoto wa mzee Kibutu, ambaye ni rafiki mkubwa wa Tonny. Hivyo mara chache ambazo iliwahi kutokea Sammy alifika kwa Tonny akiwa ametumwa na baba yake, au kwa sababu yoyote nyingine ya kawaida, walizungumza kidogo tu na zaidi ni kusalimiana na kusema kilichompeleka.

Hata hivyo, Lilian aliwahi kumfumania Sammy akimtazama kwa namna izungumzayo mengi siku walipopishana na baada ya hatua chache Lilian akageuka.

Ndiyo, ni siku hiyo alipohisi kuwa yale macho ya Sammy yalikuwa na kitu kingine kilichojificha moyoni. Kwa ujumla Sammy alimtazama kwa matamanio, jambo ambalo halikuwa la ajabu kwa Lilian kwani mara kadhaa alishawahi kuwaona watu wakimkodolea macho na hasa inapotokea akawa amevaa suruali zilizomshika vilivyo mwilini.


“Ndiyo, ma’mdogo,” hatimaye Lilian alijibu huku akiuachia mkono wa Sammy taratibu. “Za saa hizi?”

“Nzuri tu. Za kwako?”

“Shwari tu,” Sammy alijibu na kuongeza papohapo: “Vipi nd’o unakwenda home?”

“Ndiyo.”

“Hata mimi. Nadhani tufuatane.”

Walifuatana. Njiani wakawa na mazungumzo ya kawaida lakini wakati huohuo Sammy akipanga namna ya kumwingia Lilian. Walijikuta wakinogewa na story Pamoja na kubadilishana namba za simuli,
“Lakini usiwe na pupa ya kunipigia,” Lilian alimwambia, kauli ambayo Sammy aliichukulia kuwa ni hatua moja nzuri ya kwenda kwenye mafanikio.

“Muda gani ni mzuri kwa kukupigia?”

“Usipate taabu. Usipige, mimi nikiwa na nafasi nitaku-beep.”

Hisia kuwa huenda Lilian alimwambia hivyo kwa kukusudia kutokuwa na mawasiliano naye zikamjia. Ilishafika wiki nzima bila ya Lilian ‘kum-beep.’ Kuna lolote hapo? Kuna matumaini tena? alijiuliza kwa kukata tamaa.

Alianza kukata tamaa, lakini labda angekata tamaa kabisa kama siku moja, asubuhi, kitu kama saa mbili hivi, asingeona neno JIRANI kwenye ‘screen’ ya simu yake wakati ilipoita. Ndiyo kwanza alikuwa yuko kwenye daladala eneo la Makumbusho akielekea Mwenge ambako alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda cha uchapishaji vitabu.

Alishtuka na kubaki akiitazama tu simu hiyo bila kuminya kitufe cha kupokelea. Simu iliendelea kuita. Hatimaye akashtuka na kuminya kitufe hicho huku akiisogeza simu sikioni. Kwa mbali alihisi mapigo ya moyo yakimwenda kasi.
 Instagram  @kulayasimilizi
“Haloo,” alisema kwa sauti nzito na ya chini.

“Hellow,” sauti nyembamba na ya unyonge ikapenya sikioni mwake. “Ni Sammy?”

“Yeah. Ma’mdogo?”

“Ndiyo. Uko wapi?”

”Nd'o naelekea kazini. Niko maeneo ya Makumbusho.”

“N'na shida na wewe. Tunaweza kuonana mida hii?”

Sammy alifikiri kidogo na kisha akajibu, “Inawezekana. We' uko wapi?”

“Niko Kariakoo.”

“Kariakoo?! Na unataka tuonane hukohuko Kariakoo?”

Ukimya mfupi ukapita. Kisha: “Sio lazima tuonane huku. Sema wewe.”

Sammy alishusha pumzi ndefu akiwaza. Hakutarajia kupigiwa simu na Lilian leo, na siyo leo tu bali hakutarajia kupigiwa simu asubuhi kiasi hicho. Kuna nini? Kuna tatizo? Japo alimpenda na kumhitaji sana Lilian, lakini pia hakutarajia kama ingekuwa ghafla kiasi hicho.

Hata hivyo, hakuwa tayari kuipoteza nafasi hiyo. Hivyo, baada ya kufikiri harakaharaka, akasema, “Fanya hivi, njoo Kinondoni.”

“Kinondoni?”

“Ndiyo. Njoo Kinondoni. Shukia kituo cha Studio. Ukifika hapo unijulishe.”

“Ok.”

Sammy akalazimika kukiumiza kichwa chake kwa kufikiria la kufanya. Hakutaka kuipoteza nafasi hii pekee ambayo hakujua ni lini ataipata tena. Na sasa yeye anakwenda kazini. Atumie hila gani za kuwahadaa wakuu wake wa kazi ili apate mwanya wa kukutana na Lilian?
Msiba.

Naam, aliona kuwa taarifa inayoweza kukubalika kwa wakuu wake wa kazi ni inayohusu kupatwa na msiba. Hivyo, wakati alipoteremka kituoni ndipo alipoamua kupiga simu kazini kwake. Huko akaongea na bosi wake moja kwa moja akimdanganya kuwa mpangaji mwenzake kafariki.

Bosi wake hakuwa na kipingamizi chochote, akamruhusu 'kushinda msibani.' Ruhusa hiyo ilimpagawisha Sammy. Akakimbilia daladala jingine lililokuwa likielekea Kariakoo. Muda mfupi baadaye akawa njiani kwenda Kinondoni.

Akiwa ametulia kitini, daladala likipita eneo la kituo cha ITV, alitwaa simu yake na kuandika ujumbe: UMESHAONDOKA? Akautuma ujumbe huo kwa Lilian. Dakika chache baadaye, jibu likarudi: NITAKUJA BAADA YA NUSU SAA.

Sammy akasonya. Akilini mwake aliamini kuwa tangu walipowasiliana, tayari Lilian alishapanda daladala na hivyo huenda alikuwa maeneo ya Magomeni. Kumbe hata mtu mwenyewe hajatoka huko Kariakoo!

Hata hivyo hakuona kuwa kuna kilichoharibika. Subira yavuta heri. Kwa kuwa hakukuwa na foleni, aliwahi kufika kituo cha Studio na kuteremka. Na ndipo alipokumbuka kuwa alikuwa hajatia kitu tumboni tangu alipotoka kitandani.

“Usela huu!” alinong'ona huku akicheka kimoyomoyo. Alijua kuwa kama angekuwa na mke, basi asubuhi angeondoka huku akiwa amepata stafutahi nzito na hivyo labda asingehitaji kutia kitu tena tumboni mchana.

Hata hivyo, kwa kuwa hakujua kuwa lengo la Lilian ni nini, na huenda pia siku hiyo ikawa ndiyo bahati yake ya ‘kula kuku’, akaenda kwenye baa moja iliyokuwa jirani na kituo hicho. Hapo aliagiza supu na chapati tatu na kuvishusha tumboni kwa usongo. Kisha akashushia maji baridi lita moja.
 Instagram  @kulayasimilizi
Alipotoka hapo alikwenda kwenye kibanda cha kituo cha daladala na kuketi akijisomea gazeti.

***********

KITU fulani kilimwambia Lilian kuwa 'Akuanzae mmalize.' Na akaamua kuufanyia kazi usemi huo. Hivyo asubuhi hiyo, baada ya kumpigia simu Sammy, alipata kifungua kinywa cha nguvu katika mgahawa huo na alipohakikisha kuwa tumbo limetosheka alitulia kidogo, akimwazia Tonny na tabia zake mpya alizozianzisha.
“Ni kama vile kalogwa!” alinong'ona kwa sauti ambayo haikuweza kuyafikia masikio ya mteja mwingine aliyeketi jirani yake.
Akatulia hapo hadi alipopata ujumbe wa simu kutoka kwa Sammy ukimuuliza kama ameshaondoka Kariakoo. Akaujibu.

Baada ya muda aliona kuwa ni mwafaka kwake kuondoka. Akanyanyuka kitini na kulipa stafutahi kisha akashuka ghorofani. Akaenda kituoni ambako alipanda daladala la Mwenge. Alipokuwa eneo la jangwani alipiga simu na kukata kabla haijapokewa. Alitaka Sammy apige.

Sekunde chache baadaye simu ikaita. Alipopokea aliwahi kusema, “Niko njiani.”

“Umefika wapi?”

“Jangwani kwenye daraja la Kajima.”

“Ok, ukishuka njoo kituo cha magari yaendeayo Kariakoo.”

“Poa.”

“Ni kituo cha Studio. Si utakumbuka?”

“Nitakumbuka, na ninapajua.”

Simu ilipokatwa, Sammy alisimama na kuanza kuzunguka huku na kule. Kwa ujumla aliona kama vile ndoto. Hivi ni kweli Lilian anakuja? Au ananitega? Mbona amekuwa mwepesi kiasi hiki?

Hata hivyo hakutaka kuwaza mengi. Aliamini kuwa sasa bahati yake imetimia.

Akasubiri kwa shauku.


**************

LILIAN aliteremka katika daladala na kuangaza macho huku na kule, akimtafuta Sammy. Hatimaye akakumbuka kuwa alipaswa kuvuka barabara. Akavuka. Upande wa pili wa barabara alimkuta Sammy akimsubiri.
 Instagram  @kulayasimilizi
Wakapeana mikono kisha Sammy akasema, “Hapa hapajatulia. Twende huku.”

Lilian alionekana kusita kidogo lakini hatimaye alimfuata Tonny ambaye alikwishaanza kuondoka.

Walikuwa kama wanaokwenda Livingstone Hotel, lakini kabla hawajaifikia hoteli hiyo walikata kulia. Sasa Sammy alijiona yu huru zaidi. Aliamini kuwa si rahisi kwa Tonny kuja eneo kama hili na kuwafumania. Au haikuwa rahisi kukutana na mtu yeyote wa huko Kariakoo hususan mkazi wa eneo la Mtaa wa Rufiji.

Wakafika kwenye kijiduka kidogo kilichouza vinywaji baridi. Wakaketi hapo na kuagiza juisi. Hapakuwa na watu wengine katika duka hilo zaidi ya muuzaji. Hivyo Sammy aliona kuwa huo ni wakati mwafaka kwa kuzungumza.

Akilini mwake hakuamini kuwa Lilian atakuwa amekuja kwa minajili ya kustarehe kimapenzi. Kitendo cha kumtamkia mapema mambo ya kwenda gesti, aliona kuwa huenda kingemshushia hadhi. Lilian alipopiga simu alisema tu kwamba ana shida ya kuonana naye. Hakusema anataka wakutane ili wakafanye mapenzi. Hivyo, Sammy alitambua kuwa alipaswa kuwa makini.

“Umenishtua ma’mdogo. Wito wako una wema au kuna tatizo?”

Lilian alibibitua midomo na kusema, “Kwa kweli hali siyo shwari. Sasa, badala ya kuifurahia ndoa, naichukulia kama kero f'lani maishani.”

Sammy alishangaa. Akamuuliza, “Kuna tatizo gani?”

“Acha tu, Sammy. Yaani huwezi kuamini. Leo Tonny amebadilika hadi anafikia hatua ya kulala nje!”

“Yamekuwa hayo tena?”

“Nd'o ivo nakwambia!” Lilian alijibu kwa unyonge.

“Pole sana,” Sammy alimwambia huku akimwangalia kwa chati. “Hayo nasikia ndiyo maisha ya wanandoa. Mimi sijaoa, lakini kwa kweli naisikia sana migogoro ya waliooa au kuolewa. Ni mambo ya kawaida tu. Mvumiliane.”

“Hapana, nimechoka,” Lilian alisema huku kainamisha uso chini.

Watu wawili, watatu walifika dukani hapo na kuulizia hiki na kile, na wengine wakiomba viti zaidi kwa ajili ya kukaa na kunywa juisi.

Ongezeko la watu mahali hapo halikumfurahisha Lilian. Akamwambia Sammy kwa sauti ya chini, “Naona hapa kuna kiwingu sana. Hakuna sehemu nyingine iliyotulia kuliko hapa?”

Sammy alifikiri kidogo kisha akajibu. “Ipo. Na hapo siyo nje kama hapa, ni ndani ya chumba maalumu.”

Lilian alikunja uso na kufikiri kidogo. Hali hiyo ikamtia shaka Sammy kuwa huenda Lilian akamshtukia. Lakini haikuwa hivyo, badala yake Lilian aligugumia juisi yake na kuitua glasi mezani kisha akanyanyuka huku akisema, “Twende. Kwani ni mbali?”
 Instagram @kulayasimilizi
“Siyo mbali,” Sammy alijibu huku naye akiipeleka glasi kinywani. Akaimalizia juisi yake na kunyanyuka.

Wakaifuata barabara iliyoelekea chini zaidi. Kisha wakafika kwenye jengo moja zuri lililozungukwa na miti mingi iliyokiunda kivuli kizito. Sammy akatangulia kuingia, akifuatiwa na Lilian. Dakika ya kwanza Lilian alikuwa akishangaa na kujiuliza kimoyomoyo kuwa hapo ni wapi, dakika ya pili akawa ameshajua kuwa ni gesti.

Sammy akazungumza na mhudumu wa mapokezi na kumpatia shilingi 10,000 kisha akakabidhiwa funguo huku akiambiwa, “Namba nane.”

Wakaingia chumbani….. Whatsapp +255 758 018 597 kupata kamili kwa 1000 tu na unatumiwa kwa mfumo wa kitabu yaani PDF na sio vipande vipande

Post a Comment

0 Comments