Tetemo la Ghadhabu (Riwaya) - fantansia - ya kichawiNilikurupuka usingizini, mapigo ya moyo wangu yalienda kasi sana,ndoto niliyoota ilikuwa ya kutisha, sikutamani hata kuelezea. Nilinyanyuka kitandani, nikaisogelea swichi, karibu na mlango, nikawasha taa!
“,Whaaat! wewe ni nani?, ina maana nilikuwa naota ndoto ya kweli! “,niliongea kwa mshangao, binadamu wa kutisha, niliyemuota ndotoni akinikimbiza, alikuwa mbele yangu amesimama,mwanga wa taa kubwa ya umeme ulimfanya aonekane wazi juu mpaka chini,ngozi yake ilikuwa nyeupe kama karatasi,mdomoni alifungwa kitambaa cheupe, kichwani alikuwa na michirizi ya damu.
“,Nimekuja nimekuja nimekuja, nimekuja kuitoa roho yako! “,binadamu yule wa kutisha aliongea, akipiga hatua kunisogelea,ilibidi nifanye kila njia kuiokoa nafsi yangu, nikataka kukimbia, sikuweza, mlango wangu niliufunga kwa funguo kabla ya kulala, isitoshe funguo zilikuwa kitandani, nisingeweza kuzifuata, binadamu yule angenikamata kwa urahisi, aliendelea kutembea taratibu kama roboti kunisogelea, hakutembea kama binadamu wa kawaida, alitembea kwa kujiburuza sakafuni.
“,Mungu wangu, nimekwisha! “,nilitamani ardhi ipasuke niweze kutoka,haikuwezekana.
“,Wewee…e ni nani?, unataka nini kw…angu ……?”,niliuliza huku nikitetemeka,kwa mara ya kwanza nilijikojolea, niliumbuka mwezenu.
“,Naitwaa Tagrisi, mfalme wa ujinini, umenikosea sana, umenikosea, umenikosea, nimekuja kukuua, kukuua! “,nilizidi kuchanganyikiwa,nikalitazama juu mpaka chini, kweli alikuwa jini, alikuwa na kwato nyeusi, nguvu zikaniishia, nikatafakari kosa nililolifanya, sikupata jibu,kwa mbali macho yangu yakaona giza, nikahisi kizunguzungu, nikazimia palepale na kudondoka chini.
…………………………………
02:20pm
       Baada ya kuzimia, jini lile lilitoweka,lilitaka kuniuwa mpaka nitakapotambua makosa yangu,makosa ambayo sikuyafahamu. Ghafla fahamu zikanirejea tena, nilikuwa nahema na kupumua kwa kasi, mapigo yangu ya moyo hayakuwa ya kawaida,nikatazamaa juu ya dali sikuona kitu, kulia na kushoto, sikuona kitu, nikatazama chini ya uvungu, sikuona kitu chochote kile, nikaisogelea friji yangu, nikamimina maji kwenye glasi, nikanywa,angalau mwili wangu ukapoa, joto likapungua. Taratibu nikakisogelea kitanda changu, nikalala tena, baada ya dakika tano tu, usingizi mzito ukanichukuwa, nikaanza kuota ndoto nyingine ya kutisha, niliota nikiwa katikati ya msitu, mikono na miguu yangu ilifungwa kwa kamba ngumu ya katani. Jini yule aliyejitambulisha kwa jina la Tagrisi, alikuwa ameshika panga,nyuma yake alikuwa na wafuasi wake, walifanana kwa kila kitu, mavazi yao ya rangi nyeusi, ngozi nyeupe pamoja na michirizi ya damu kichwani.
“,Umenikosea sana, umenikosea sana, lazima ufe, lazima ufe, lazima nyama yako niwapatiee wafuasi wangu, wafuasi wangu ……”,jini aliyejitambulisha mbele yangu kwa jina la Tagrisi aliongea, akanyenyua panga lake kubwa, lililong’aa kutokana na makali yake, alitaka kuninyofoa kiungo kimoja baada ya kingine,akalishusha panga lake kwa kasi ya ajabu aweze kuifyeka shingo yangu…“,Mamaaaa, nakufaaaa!” Tukutane Whatsapp +255 758 018 597
Nilikurupuka usingizini, mapigo ya moyo wangu yalienda kasi sana,ndoto niliyoota ilikuwa ya kutisha, sikutamani hata kuelezea. Nilinyanyuka kitandani, nikaisogelea swichi, karibu na mlango, nikawasha taa!

Post a Comment

0 Comments