“sasa
amepita hapa akaona anisalimie kidogo mzee wake,” alijibu mzee Hewa... “Ahaa!
Oke...halafu anaondoka zake?” baba Mei alitaka kujua zaidi...
“Anaondoka...kwani vipi?” “Nimeuliza tu mzee wangu...” “Ataondoka...ataondoka.”
Baba Mei alirudi kwanza ndani kisha baada ya kama dakika tano akatoka huku akisikika
akisema... “Ole...ndiyo utanitambua mimi nani?!” Baada ya baba Mei kuondoka,
mzee Hewa na Jombi walijadili lile swali... “Huyu bwana inaonekana amekutilia
wasiwasi...maana kijana kama wewe kuja hapa
na mke
mwenyewe kama huyu ni tatizo,” alisema mzee Hewa... “Hata mimi nimemshangaa
hivyohivyo mzee Hewa kwani asingeweza kusema maneno yale mbele yangu huku
nasikia...afadhali angekuuliza nikiwa sipo,” alisema Jombi huku moyoni yeye
akiijua dhamira iliyompeleka pale... “Jana nilisoma gazeti moja linasema hizi
nyumba zetu hapa zitabomolewa, we unazo habari hizi?” mzee Hewa alikata
maongezi ya awali na kumuuliza Jombi hivyo... “Hapana mzee Hewa, ni kweli?”
“Ngoja nikalilete na wewe upitie habari hizo,” alisema mzee Hewa huku akisimama
kwenda ndani akiimba nyimbo za dini kama ilivyo kawaida yake. Mara, mama Mei
alitoka. Safari hii alikuwa amejifunga kitenge, mkononi alishika kipochi
kidogo, ilionekana alikuwa akienda dukani au gengeni. Licha ya kuvaa kitenge
ambacho kilikaribia kuburuza chini lakini mzigo ulionekana kama kawa... “Anti
naona unafuata bidhaa dukani sasa!” alisema Jombi. Mama Mei alimwangalia
kwa jicho la
uchokozi kisha akasema... “Ni kweli lakini leo jua kali kama nini Mungu wangu,
sijui niende na mwamvuli...” “Hata mimi nashauri hivyo maana...au nitume mimi.”
Mama Mei alicheka huku akimkazia macho Jombi... “Yaani nikutume wewe anko si
itakuwa dharau kubwa... nakwenda pale buchani na kwenye lile soko la pale
kona...” “Nitume tu anti,” Jombi aling’ang’ania kutumwa. “Kweli?” mama Mei
alitaka kujua ya moyoni... “Kweli kabisa anti,” alisema Jombi huku akisimama
tayari kwa kutumwa... “Basi asante, nataka nyama kilo tano maana huwa naiweka
kwenye friji kwa wiki nzima. Halafu nataka kabeji tatu... nazi sita...viazi
mviringo kisado na mchele kilo tano,” alisema mama Mei... “Mh!” Jombi aliguna
moyoni baada ya kupata picha ya ukubwa wa mzigo atakaobeba. *** Jombi, licha ya
kufanya kazi serikalini tena ya maana, pia ni mume wa mtu, bidhaa alizojituma
kununua na maeneo zinakopatikana na nyumbani kwake ni jirani tu,
hivyo
alikwenda kwa mahesabu sana. Alipokuwa kwenye soko alikumbana na maneno haya...
“Baba Hawa leo umekuja mwenyewe? Mama vipi..?” “
Leo baba
Hawa nakuona umeamua kufuatilia mahesabu mwenyewe.” Mpaka mwisho anaondoka
akiwa amebeba mfuko mkubwa kabisa, hivyo aliamua kuchukua Bajaj japokuwa
alikokuwa anakwenda si mbali sana. * Mzee Hewa alishangaa kukuta Jombi hayupo
nje alikomwacha... “Kha! Huyu bwana vipi tena?” alijiuliza bila kupata majibu
kwani hakumkuta mama Mei, aliingia ndani akijua anko huyo akirudi na mizigo
atamwita. * “Baba Hawa hiyo mizigo unaipeleka wapi mume wangu? Sikuelewi,”
sauti ya mkewe, mama Hawa ilimshtua kwa nyuma akiwa anapanda Bajaj...
“Ohoo! Ni
mzigo wa baba Kabweka, kaniambia aliacha hapo sokoni, sasa kwa vile mimi
nakwenda kule kwake kaomba nimbebee,” alipiga uongo Jombi... “Sawa mume wangu.”
Jombi alipona, alipeleka mizigo hiyo hadi nyumbani kwa mzee Hewa na kukutana na
mzee huyo nje. Alishangaa kumwona Jombi anaingia na Bajaj tena na mizogo wakati
dakika chache nyuma, alikaa naye hapo... “Imekuaje tena kijana wangu? Mbona
natoka na gazeti sikuoni?” Huyo dada mpangaji wako aliniagiza sokoni.”
Mara, mama
Mei mwenyewe alitokea huku akimshukuru sana Jombi... “Jamani anko yaani sijui
nikupe zawadi gani? Yaani nashukuru kama nini...yaani eee...na jua hili
nilikuwa najifikiria sana yaani...” alisema mama Mei huku akijifunga kanga
vizuri kwani alitoka na kanga moja tu... “Si unipe mimi mwenyewe nafasi ya
kuchagua zawadi anti,” Jombi alijisemea moyoni...Usijali anti...sisi ni wamoja mbona,”
alisema Jombi. Baada ya Bajaj kuondoka na mama Mei kuzama ndani na mizigo yake,
mzee Hewa alimtupia jicho Jombi... “Kijana,” aliita... “Naam...” “Kuna kitu...”
“Kuhusu nini mzee Hewa..?” “Huyu mama wewe unajuana naye?” “Wala! Ametoka tu
hapa akasema anasikia jua kwenda kununua vyakula nikamwambia lete hela
nikakununulie.”
“Basi,
umejishindia kijana wangu....maana kama ni mke wa mtu na anajitambua halafu
anafikia hatua ya kukuamini wewe kijana mkubwa ukamfanyie manunuzi, mshukuru
Mungu maana wenzako wengi wanapitapita hapa kila siku kufukuzia,” alisema mzee
Hewa. Moyoni, Jombi aliamini yeye ni mshindi kama kweli kuna wenzake
wanapitapita kufukuzia halafu yeye kafikia levo ile, basi yupo juu... “Yes!
Mshindi mimi bwana,” alisema moyoni Jombi... “Hapana mzee Hewa mimi binafsi
sina lengo baya na mke wa mtu...kwanza mimi ni muoga sana na wake za watu,”
alisema Jombi huku akilichukua gazeti kwa mzee Hewa na kusoma habari
aliyoambiwa. Mama Mei akatoka tena, safari hii alikata kona kwenda kwenye
kiduka cha jirani. Alikuwa ndani ya kanga moja tu, sasa ile tembea yake na
mtingishiko wa wowowo, mzee Hewa alijishika kichwa licha ya umri wake mkubwa,
Jombi yeye alijiinamia.
Walinyamza
kimya! Kimya kabisa!! Wakati anarudi sasa, macho yake yalikutana na macho ya
Jombi yakiwa yameoneka kuumizwa, mama Mei akaachia tabasamu pana kwa maana ya
kuweka ukaribu wa kibinadamu kwa vile alimsaidia jukumu la kununua mahitaji.
Jombi naye aliachia tabasamu la woga, akamwangalia kwa kumsoma kuanzia juu
kwenda chini, mama Mei akazama ndani kwake. Safari hii, mpaka Jombi anaondoka
zake, mama Mei hakuwa ametoka tena. Mbaya zaidi, hatua chache mbele, Jombi
alipishana na mume wa mama Mei akiwa anarejea nyumbani kwake. Walikutana macho,
baba Mei alionekana kummaindi sana Jombi. *** Siku ya tatu, jioni, Jombi
alishatoka kazini sasa alikuwa akirandaranda mitaani, akaibukia mtaa wa jirani
na kwa mzee Hewa ambapo pana baa.
Alikaa hapo.
Katika kutupia macho, akamwona mama Mei amekaa sambamba na mume wake,
alishtuka... “Ohoo! Jamaa si atajua namfukuzia mke wake, maana nabanana naye
sana,” aliwaza moyoni. Mama Mei naye, katika kupitishapitisha macho, akamwona
Jombi, akafurahia moyoni kwani alikumbuka alivyomtuma sokoni... “Wanaume
wengine jamani, wakarimu kweli. Baba Mei umtume vile sokoni, mbona atakung’oa
meno,” alisema moyoni mama Mei. Kuna wakati baba Mei alikwenda chooni, mama Mei
akatumia nafasi hiyo kulisisitiza jicho lake kwa Jombi ambapo yalikutana, mama
Mei akaachia tabasamu na kupunga mkono, Jombi naye akapunga mkono, wakaachiana
tabasamu.
Baba Mei
alipotoka chooni, hakukaa, aliondoka na mkewe huku baa yote wakimtupia macho,
wake kwa waume. Baadhi yao walionesha kutingisha vichwa vyao kutokana na umbo
la mama Mei. Jioni hiyo, alivaa suruali ya kubana na t-shirt pia ya kubana,
sasa wakati anakanyaga chini ili mguu uende mbele, looo! Wanaume walionekana
kuumia ndani kwa ndani, wengine walisemezana kwenye meza. Kwa upande wake,
Jombi alionekana kuumia zaidi kwani alimkodolea macho mwanamke huyo mpaka
anapotea na mume wake huku moyoni akiumia kama vile mwanamke alikuwa wake sasa
ameporwa na mwanaume mwenye fedha zake.
Saa mbili
usiku, Jombi aliondoka kwenye baa hiyo kurudi kwake, lakini akaamua kupitia
njia ya kwa mzee Hewa akiamini anaweza hata kusikia sauti ya mama Mei... “Yule
saa hizi atakuwa ameshalala,” alisema moyoni Jombi. Alipita nje ya nyumba hiyo
huku macho na masikio yakiwa hapo. Ghafla alisikia mlango mkubwa ukifunguliwa
kwamba kuna mtu anatoka. Jombi alisimama na kukazia macho mlangoni, moyoni
alimwomba shetani wake amsaidie kwamba, anayetoka awe mama Mei... “Yaani
akinipa dakika tatu tu ya kunisikiliza atajua mimi ni nani na naamini ataingia
laini,” alisema moyoni Jombi huku macho yake yakitamani sana kumwona anayetoka.
MWANAUME
mmoja mnene, mrefu, mweusi tii ndiye aliyetoka akiwa amevaa singlendi kwa juu,
chini pensi. Alionekana ana asili ya ukorofi... “Mbona umesimama hapo kijana,
una shida na nani?” aliuliza yule mwanaume huku akikohoa. “Hapana, napita tu,”
Jombi alijibu kwa upole huku akianza kutembea. Lakini muda huohuo, mama Mei
alichomoza kwenye mlango mkubwa, akashuka ngazi na kuelekea uelekeo wa ile baa
waliyokaa. Kwa usiku ule na kwa kutumia mwanga wa taa ukijumlisha na tembea
yake, hata yule mwanaume pale nje alimwangalia kwa macho yenye matamanio
makubwa...
“Haya bwana,
ulimwengu shujaa,” alisema yule mwanaume huku mama Mei kama vile anafanya
kusudi sasa, maana ungeweza kusema mzigo utaanguka wakati wowote ule. Jombi
alitamani kugeuza njia kwani aliamini mama Mei anarudi kule baa kwa ajili yake.
Alichofanya, alikatiza mbele akageuza kwa njia nyingine na kutokea baa. Alivuta
kiti na kukaa huku macho yake yakimulika kila kona kama atamwona mama Mei.
Lakini hakumwona! Jombi alijisikia unyonge sana, akaondoka kurudi kwake lakini
safari hii akitumia njia nyingine. *** Ilikuwa siku iliyofuata asubuhi, mzee
Hewa alikuwa uani akipiga mswaki ili afuate mafao yake, NSSF, mama Mei alitoka
ndani kwake akiwa ndani ya kanga moja tu... “Shikamoo mzee Hewa...” “Marahaba
mwanangu, umeamkaje mama?” aliitika mzee huyo huku akimwangalia mama Mei
anavyokwenda chooni huku wowowo likisomeka kwa baba mwenye nyumba wake
kwa
mtetemeko... “Leo mbona asubuhi sana mzee Hewa?” mama Mei alimuuliza bila
kusimama... “Nafuata vijisenti vyangu NSSF bwana...” “Ahaa! Kavilite tule hata
nyama,” mama Mei alimtania mzee huyo. Mzee Hewa hakuongeza neno kwani tayari
mama Mei alishazama chooni åΩLakini wakati anatoka, baba Mei naye alikuwa
ameshatoka alikuwa uani hapo akipiga mswaki. Kwa hiyo mzee Hewa alishindwa
kutia neno mbele ya mali za watu... “Hivi wewe mbona hunisikii?” baba Mei
alimuuliza mkewe kwa sauti ya chini lakini yenye hasira sana, mama Mei
hakujibu, akaenda ndani. Kwa mzee Hewa baba Mei kumlalamikia mkewe kwamba
hamsikii ilikuwa kama mara ya saba tangu wamehamia pale... “Kama ni mara saba
je mara ambazo mimi sijasikia ni ngapi? Kuna jambo, huyu mama hataki kumsikia
mume wake na hawa ndiyo wanawake wetu siku hizi,” alisema moyoni mzee huyo,
akaenda kuoga akarudi
ndani kwake
kujiandaa. Baba Mei ndiye aliyeanza kutoka ndani ya nyumba ile. Wakati mzee
Hewa anatoka, alimwita ili ampe lifti... “Ameshaondoka mbona,” alijibu mama
Mei... “Ooo! We upo?” mzee Hewa alimuuliza akiwa amesimama mlangoni, mama Mei
akatoka huku na kusimama mlangoni... “Mimi nipo baba,” alisema mama Mei. Mzee
Hewa alimwangalia mama Mei, mama Mei naye akagundua anamwangalia,
wakaangaliana, mama Mei akainamisha uso... “Hivi mjukuu wangu...” “Abee...”
“Mumeo anapenda kukulalamikia kwamba humsikii, kuna nini kati yenu?” Mama Mei
akaachia tabasamu... “Mzee Hewa, baba Mei hana lingine zaidi ya wivu. Yeye
hataki mimi nivae kanga, nivae suruali, anataka nivae magauni makubwa tu...sasa
kwa mfano saa zile natoka kwenda chooni, nivae gauni kama nakwenda kanisani,
inawezekana kweli..?
“Haya, kama
vile haitoshi, hali ya jiji letu la Dar inafahamika, sasa mchana na jua kali
mimi naenda sokoni, nivae gauni kama nakwenda kwenye mkutano wa wazazi shuleni,
ni sawa kweli?” Mzee Hewa alibaki akisikiliza, ikafika mahali akasema... “Kuna
dozi yake nitakupa...” “Ya kunywa ya kumeza?” aliuliza kwa haraka mama Mei... “Ya
kawaida tu, wivu wote huo utakwisha...” “Kweli mzee Hewa? Maana ananikwaza sana
ujue...” “Dawa yake ndogo tu nitakupa dozi mimi,” alisema mzee huyo huku
akiondoka... “Mzee Hewa naisubiri kwa hamu kubwa hiyo dozi,” mama Mei
alimsindikiza kwa maneno hayo. *** Alasiri ya saa tisa, mzee Hewa alirudi kabla
baba Mei hajarudi, alimkuta mama Mei amekaa nje kwenye mkeka.
“Pole mzee
Hewa, inabidi uoe sasa...maana kama hivi umerudi huna wa kukupikia,” alisema
mama Mei kwa sauti iliyojaa utani... “Kama wewe upo mimi sina haja ya kuoa,”
mzee Hewa naye alirudisha utani... “Wee! Unataka kupigwa mzee Hewa? Hivi hapa
nilikuwa nakusubiri kwa hamu kubwa unipe hiyo dozi uliyoahidi,” alisema mama
Mei...
“Njoo ndani
nikupe dozi yake,” mzee Hewa alisema akiingia. Mama Mei alisimama, akamfuata
mzee huyo kwani ni kweli kutoka moyoni alitamani sana kupata ufumbuzi juu ya
wivu mkubwa alionao mume wake, baba Mei. Mzee Hewa alizama hadi chumbani, mama
Mei yeye akasimama akijua mzee huyo atatoka... “Pitapita mama Mei pita,”
alisema mzee Hewa huku akiangalia mlangoni. Hapo alikuwa sebuleni kwake, sebule
ambayo ilisheheni vitu vya kisasi licha ya uzee wake... “He! Mzee Hewa, mpaka
niingie ndani jamani?” aliuliza mama Mei huku akifungua mlango. Mzee Hewa
alisimama, akafunga mlango na funguo kisha akazichomoa...
Kama kawaida ni
Kama kawaida ni
Whatsapp
+255 758 018 597
Email –
emanmic@yahoo.com
0 Comments
Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu
Emoji