Jastin ni kijana mwenye miaka
ishirini, nimpole sana kumsikia anaongea ninadla sana, hata uongeaji wake
niwataratibu sana, tena uongea mara chache na kwa sauti ya chini, hata huko
shuleni alikokuwa anasoma wenzake walikuwa wanamwita paroko.
Kwa sasa Jastin alikuwa amemaliza kidato cha sita, katika shule ya
sekondari ya Luhuwiko huko mkoani Ruvuma, kipindi cha kusubiri matokeo alienda
Dar es Salaam, kumtembelea kaka yake mkubwa Higno, ambaye alikuwa akifanya kazi
kwenye kampuni moja yausafirishaji, kama dereva wa magari makubwa yamizigo
yanayo safari kwenda mikoani na nje ya nchi kupeleka mizigo mbalimbali, kipindi
Jastin anafika Dar es Salaam shemeji yake yaani mke wa kaka yake alikuwa
ameenda kwao Morogoro kujitazamia kwaajili yakujifungua yaani alikuwa mjamzito,
Higno alikuwa anakaa Dar es Salaam mbezi, mtaa wa makondeko, unaingia ndani
kidogo ukiihacha barabara kuu iendayo Morogoro, nje kidogo ya jiji Higno
alipata eneo dogo nakujenga chumba kimoja na sebule, mtaa huo ulikuwa ni mtaa
mpya wenye nyumba chache tu kubwa sana zenye fensi na mageti makubwa na nyumba
ndogo kama ya Higno kaka yake Jastin, nyumba za mtaa huu mpya zilikuwa
zimeachiana nafasi, kubwa kati ya nyumba na nyumba.
Shuguli za Jastin kila siku, tokea ameingia Dar ni kuweka mazingila
safi nakujipikia, kisha anachukuwa simu yake nakufungua facebook hapo ushinda
mpaka anaingia kulala, siku moja moja alikuwa akienda na kaka yake ofisini kwao
Mwenge huko alimsaidia kaka yake shuguli za ufundi wa gari analo tumia kwa
safari za kupeleka mizigo mikoani na nje ya nchi, kama service za kawaida za
gari, maana alikuwa anafahamu ufundi wa magari kutokana na baba yao kumiliki
garage japo siyo kubwa huko Nachingwea Lindi, lakini kwa Nachingwea magari
mengi sana yanatengenezwa pale, ndipo yeye utumia kipindi cha likizo kusaidia
kazi ndogondogo za kiufundi.
Siku moja Higno alisafiri kwenda nchini congo DRC, akipitia Rwanda
kupeleka magari ya umoja wa mataifa angetumia wiki mbili kwenda na kurudi huku
nyuma Jastin alibaki peke yake haikuwa tatizo kwake, siku ya pili toka kaka
yake asafiri Jastin aliamka mapema sana akiwa amevalia tracksuit nyepesi,
akaanza kufanya shuguli zake za kila siku ikiwa pamoja na mazoezi ya viungo
kidogo, tena ufanyia ndani kwao kisha akatoka nje akawasha jiko la mkaa kwa
ajili ya kutengeneza kifungua kinywa.
Wakati jiko linakolea akaanza kufagia, wakati anaendelea kufagia
akaona geti la nyumba ya jirani yao linafunguliwa, mfunguwaji alikuwa mama
mmoja alievalia gauni fupi kidogo lililokamata mwili wake vyema kiasi kwamba
Jastin aliweza kushuhudia umbile zuri la yule mama yaani vizuri kabisa,
kiukweli hakuwahi kumuona yule mmama zaidi ya binti mmoja ambaye kama siku
mbili sasa hajamwona, wakati akiendelea kumwangalia yule mama akamwona amefungua
geti kisha akarudi ndani hakuweza kumwona tena sababu ya ukuta mkubwa
ulioizunguka ile nyumba mara akasikia mlio wa gari likitoka kwenye lile geti,
ni prado nyeusi, likasimama nje kisha akashuka yule mama akaenda kufunga geti,
wakati anafunga geti gari likajizima, yule mama alipomaliza kufunga geti
alirudi kwenye gari nakujaribu kuliwasha tena lakini alikuwaka, alijaribu mara
tatu zaidi alikuwaka akamwona akishuka na kutazama huku na huko, alipotazama
upande aliopo Jastin, Jastin akajifanya anaendelea kufagia lakini aliendelea
kumtazama kwa macho ya wizi.
“We! anko, We! anko unayefagia” yule mama akaita huku akitazama
kule alipo yeye, Jastin akasimama na kujionyeshea kifuani kwamba “Unaniita
mimi?” “Ndiyo anko, samahani nakuomba mara moja” Jastin akaweka mfagio chini
kisha kamfuata yule mama huku akiuangalia ule mwili wakipekee wa yule mama wa
jirani, kila alipozidi kumsogelea ndipo alipoanza kugundua kuwa, licha ya
umbile lenye kutamanisha pia huyu mama alijaliwa sura nzuri na ya kuvutia
“Shikamoo mama” Jastin alimsalimia yule mmama wa jirani baada tu yakumfikia
“Marahaba mwanangu, samahani kwa kukukatisha shuguli zako” aliongea yule mama
huku akionyesha uso wa tabasamu, nakufanya midomo yake yenye lips pana
zilizopakwa rangi nyekundu ya midomo kumchanganya Jastin japo kwa umri huyu
mama ni ni mkubwa sana kwake lakini alionekana bado wamoto “Usijali mama”
alijibu Jastin kwa sauti yake ya upole huku akijitaidi kuyakwepa macho mazuri
yaliyo kolea wanja ya yule mama, “Wewe ni ndugu wa yule kaka anaekaa pale?”
aliongea yule mama huku akionyesha kwa kidole nyumbani kwa akina Jastin, hapo
Jastin alipata nafasi ya kushuhudia pete na bagili za dhahabu zilizo jaa
mkononi kwa mama huyu, “Ndiyo ni kaka yangu mimi ni mdogo wake wa mwisho”
alijibu kwa sauti yake ya upole “Ok! naliacha hapa nje gari langu naomba
uniangalizie, maana limezima ghafla” aliongea yule mama akionyesha kupendezwa
na upole wa Jastin “Kwani lina tatizo gani?” aliuliza Jastin kwa sauti ileile
ya upole, akiligeukia gari la mama wa jirani “Kwakweli mimi hata sijui, yani
limezima lenyewe ghafla, nitachukuwa gari jingine hili nalihacha hapa” hapo
Jastin akazunguka kwenye boneti “Hebu fungua boneti niangalie kama litawaka”
hapo mama jirani akashangaa kidogo, “He! kumbe wewe ni fundi?” aliongea yule
mama huku anafungua mlango wa gari kisha akalifyetua boneti “Hapana nina
ufahamu mdogo tu wa magari” Jastin aliinua boneti alafu akalizuwia na kifimbo
chake cha chuma kisha akaanza kukagua huku akirekebisha kila alipoona panafaa
kurekebishwa, lakini kwa macho ya wizi hakuacha kutazama maumbile ya mama
jirani yalivyo jichora kwenye kile kigauni matata.
0 Comments
Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu
Emoji