Ninja wa Chuo (Riwaya) - Utamu, Vita



Kijana Martin anaamua kujiunga na chuo hicho maarufu kwaajili ya kupata diploma ya ufundi wa magari yaani Diploma of motor vehicles mechanical,  baada ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga chuoni hapo aliamua kuanza masomo yake, kijana Martin alikuwa mpole sana ingawa alikuwa mtu hatari katk mapigano ya ngumi, kwa tabia yake ya kutoongea ovyo ovyo walimpa jina la Domo ganzi yani ni mzito kuongeaongea, lakini alimpata rafiki yake anaeitwa Japhet ambae walilala katika bweni moja wanafunzi wa chuoni hapo walimdharau Japhet kwa kuwa marafiki na mtu asiependa kuongea na wengine, waschana nao walikuwa wakimdharau sana Martin na kumuita bwege au domo ganzi, lakini hapohapo chuoni kulikuwa na vijana wanajiita The black Tiger, ambao walikuwa wakorof sana na kuwafanya wanafunzi wote hapo chuoni kuwaogopa kwani walimnyanyasa kila mtu, siku Martin akiwa ktk mti wa kimvuli pamoja na rafiki yake Japhet kundi la watu wanne the black tiger walipita karibu yao na kumkejeli Japhet we jinga naona upo na domo zege hapo ni maneno yaliyotamkwa na kijana aliefahamika kwa jina la Samson Nyigenda,  kwa kusema kweli Japhet hakupendelea kitendo kile akaamua kumjibu Samson kama ifuatavyo nyinyi msijione mmewini sana kwa ubabe mlionao msimdharau mtu et kisa sio mzungumzaji hapana MUNGU hapend hivyo hiv nyinyi mtajibu nn kwa MUNGU Samson maana ubabe na ukorofi mnafanya kama sifa flan hiv hiyo siyo ishu, alifoka Japhet, mnamsikia huyofala alisema Samson kuwaambia wenzake, wenzake wakasema yaa bac mpe vitasa akuheshimu,  Samson alimsogelea Japhet akamkwida shati huku akimtikisa afu akamzaba kibao taa, huku akisema acha ujinga we fala naweza kukuua af sifungwi mm na kumuacha af akawaita wenzake wakaondoka, hukunyuma Martin alimsogelea rafikiyake akiwa analia kwa kwikwi, na kumpa pole lakin Japheth alisema kwa huzuni sana tutaonewa mpaka lini hapo chuoni mana kuna watu wamebakwa kesi zimeishia juujuu kutokana na wazazi wa hawa watu kulipa pesa mahakamani na hata kuamua kufukuzwa chuo kwa mtu anaewapinga hawa watu hadi wakufunzi wanaogapa kuwashutumu hao watu kwakuhofia kupoteza ajira zao tumechoka Martin mkomboz wetu atakuwa nani sisii, Ndugu yangu tumuombe MUNGU tu atuepushe na mabaya ya hawa watu wasitudhuru wahenga wanasema penye taabu mafanikio hupatikana hapo hao we achana nao tu MUNGU atawaadhibu siku yao tulia rafki yangu Japhet alinena Martin na kumchukua Japheth na kuenda bwenini kwao, walivyofika Martin alimsihi rafiki yake kuwa mtulivu asiwe na jazba kwani yale ni mapito tu,  baada ya wiki 3 martin akiwa zake ametulia ktk mti wa kimvuli alionekana binti mmoja mrembo akija upande wake akiwa kabeba biblia mkononi mwake huku akiwa na tabasamu pana alifika pale alipokaa martin na kukaa chini,  mambo! yule bint alimsalimu Martin huku akitoa tabasamu nene,  poa alisema Martin kwakuitikia salamu, yule bint aliendelea kaka mbona unaonekana ni mpole na mtulivu sana yani hadi najikuta natamani the way you live jamani,  a ni kawaida wanasema jogoo wa shamba hawiki mjini alijibu Martin,  ni kweli lakini mimi sijaona mvulana mtulivu kama wewe hapo chuoni kwani wengi wao ni wakorofi na waasharati, walev wa kupindukia,  ni kweli lakini mimi ndivyo nilivyo na sipendi kusifika kwa mabaya MUNGU ataniadhibu kwa uzembe, alisema Martin kumjibu yule mschana,  Mimi naitwa Jackline Mwasonye natokea mbea na ni mtoto wa mchungaji mwasonye nasomea IT information technology, sawana mm naitwa Martin Jinu natokea morogoro nasomea motorvehicle machanics,  vizuri kwa hilo mimi nataman watu wenyetabia nzuri kama yako na napenda tuwe tunashirikiana kwa mambo mbali mbalimbali
Sawa lakini watakuonaje waschana wenzako ukishirikiana na mm domo ganzi sihitaji utengwe kwaajili yangu,  hapana kaka watajaza wao mm sijali huko, alisema Jackline,  sawa chukua namba ya simu nami nipe yako, wakapeana namba za simu hatimae jackline aliondoka, kumbe wale black tigers waliona jackline alivyokaa muda mref na Martin si wakajisogeza,  we fala unaongea na mrembo yule yan hatutaki sisi yupo na wewe fala yalikuwa maneno ya Samson akimuambia Martin,  aliendelea yani ukitaka kupingwa endelea kuwa nae yule mtu, jamani mnisamehe mm sikuongea nae mabaya zaidi ya story tu, alijtetea Martin,  maongez tu ndiyo nusu saa nzima alijibu samson na kumsukuma Martin afu akasema jiangalie na wakaondoka zao, walivyoondoka tu martin alijuliza kwanini wananyanyaswa hivyo,  upande wa jackline alijiuliza sana mbona yule martin ni mtulivu kuliko wengine wanaokuwa wez na wagomvi, sina budi kuwa nae i love him sipotayari kumkosa Martin na ntaendelea kuwa karibu nae Martin alitamka Jackline akiwa anapanga nguo zake kwenye begi huku akisikiliza mziki kwenye simu yake,  upande wa The Black Tigers walipanga kumteka jackline wakambake..
*****
Wakipanga kumteka Jackline ili wakambake lakini ulikuwa ni muda wa usiku wakina Samson wakiwa katka ua lililo kuwa karibu na ukuta lakini Martin alikuwa akiwa karibu na ua hilo alisikia yote yaliyokuwa yakizungumzwa, yule Jackline anatukataa sisi anampenda Martin lazima tumteke tukambake ili atuheshimu,  alisema Samson akiwaambia wenzake,  a yule mbona lazima anyakwe na akawekwe kwenye mitambo huyu, alijibu jamaa mwingine aliekuwa upande wa pili,  na walipanga mpaka kwa kumtekea Jackline,  lakini martini alikuwa anasikia ya yote…
Jiaulize Mwanaume atawafanyaje… +255 758 018 597 whatsapp. Kutana Na ACTION NOVEL Inayosisimua..
+255 758 018 597
DARASA LA ENGLISH COURSE
Nafahamu wewe ni msomaji mzuri wa simulizi zetu na unatuamini sana, zaidi tumependa kukuletea huduma ya ENGLISH COURSE kwa njia ya online na uso kwa uso kwa walio ndani ya Dar es Salaam (+255 758 018 597) .


Post a Comment

1 Comments

Karibu sana, tuma ujumbe whatsapp +255 758 018 597 kujipatia simulizi zetu

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)