Just Relax (Riwaya) - Utamu


Ilikuwa mida ya saa tano usiku, mida ambayo Frank alikua njiani ndani ya gari lake Toyota Voltz akirudi nyumbani kwake Mbezi kwa Yusuph toka kazini kwake saa tano usiku, ni masaa nane toka kijana huyu atoke ofisini kwake iliyopo maeneo ya Poster Mpya mjini Dar s Salaam, ni kawaida yake kupitia kwanza bar ilikupata moja moto moja baridi, akishushia na nyama choma, kabla ya kurudi nyumbani kwake ambako alikuwa ana kaa peke yake, tabia ya kupenda kukaa bar baada ya kutoka kazini aliianzisha miaka miwili iliyopita, na sababu kubwa ikiwa ni mapenzi.
Ilikuwa hivi, Frank baada ya kumaliza Elimu yake ya kidato cha sita, akiwa kijana mwenye umri wa miaka ishilini na mbili(22), alipata kazi(ajira ya muda) kwenye kampuni moja ya kununua mazao, huko Mtwara kusini mwa Tanzania, na zao kubwa walilokuwa wananunua ni korosho, Frank aliajiliwa kama muhasibu wa manunuzi kwenye ghala moja lililopo Newala, baada ya kufanya kazi kwa uaminifu kwa kipindi chote cha msimu wa manunuzi, hata msimu wa korosho ulipokwisha Farank alisaidiwa na wamiliki wa kampuni hiyo kupata ajira ya kudumu kwenye kwenye kampuni yao, ambayo licha ya kununua mazao pia walikuwa wanatengeneza bidhaa zitokanazo na mazao hayo, kama biskuti, unga unaotumika kwenye vinywaji mbalimbali, pia hata korosho zilizowekwa kwenye vikasha nakuuzwa ndani na nje ya nchi, Frank akiwa amewekwa kwenye idara ya masoko, ofisini kwao poster mpya, ambapo kiwanda chao kilikuwa maeneo ya Mbagara barabara ya kuelekea kusini mwa Tanzania.
Frank alikua ni mtoto wa kwanza kati ya wawili pekee kwa baba na mama yake, mtoto wapili alikuwa ni dada yake, ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Mapinduzi huko Lindi, wakati huo wazazi wao walikuwa wanaishi Masasi mjini, ni sehemu ambayo wazazi wao waliichagua baada ya kuwa baba yao amestaafu kazi ya Jeshi la wananchi, bahati nzuri kwake mzee huyo alikuwa amejipanga kimaisha kabla ya kustaafu, nakufanya maisha yake yawe mazuri kidogo, kiasi kwamba mzee huyo hakuwa tegemezi kwa watoto wake, kitu kilicho sababisha ata watoto wake waweze kufanya maisha yao kwa nafasi zaidi.
Ndani ya miezi sita baadae Frank akiwa anakaa maeneo ya Mbezi Mwisho, kwenye chumba chake kimoja alicho panga, ndicho kipindi ambacho Frank alikutana na Christina, msichana aliyekuwa anasoma chuo cha usimamizi wa fedha IFM, huko huko maeneo ya Poster, walikaa wote Mbezi Mwisho, Frank anamkumbuka sana Christina au Tina kama wenzake walivyo zoea kumuita, hakika ni vigumu sana kumsahau binti huyu wa Kihaya, Frank alikumbuka siku ya kwanza kukutana na Christina ilikuwa asubuhi, kwenye daladala Toyota Coster akielekea kazini, kwenye Seat aliyokaa pembeni yake alikaa msichana mrembo sana mwenye rangi ya chokoleti mzuri wa sura na umbo pana lililo jazia kisawasawa, akionyesha ameenda hewani kidogo, “Mambo vipi dada” alisalimia Frank kwa sauti ya chini, kana kwamba hakutaka watu wengine wasikie ile salamu zaidi ya muhusika, lakini yule msichana mrembo ambae kiumri wanalingana, alimtazama Frank na kumpotezea kana kwamba hakuwa yeye anayesalimiwa, kitendo hicho kilimfanya Frank ajisikie aibu sana, akazuga na kutoa simu yake ndogo zile zinazoitwa za tochi, akaanza kucheza game la nyoka, safari iliendelea huku watu wakizidi kujaa kwenye daladala.
Wakiwa Kimara mara hii hapa Kologwe, Butcha, Baruti mpaka Ubungo Maji, mara ukazuka ugomvi wa kijana mmoja ambaye alitaka kutoa nauli nusu, hapo Kondakta akawa mkali kweli kweli, akimkunja yule kijana ambae alikuwa akilalamika kuwa hakuwa na fedha ya kutosha, lakini haikusaidia hata kidogo mpaka mtu mmoja alipojitolea kumsaidia kwa kumuongezea fedha iliyopelea, hapo Frank akamuona yule dada jirani yake akichukua mkoba wake na kuanza kuupekua, kana kwamba kuna kitu anakitafuta bila mafanikio, baada ya kuvuka mataa ya Ubungo kondakta akaaza kukusanya nauli toka kwa abiria, huku akitoa maneno ya kashfa kwa wale walioomba kupunguziwa nauli, hatimaye kondakta akaifikia siti aliyokuwa amekaa Frank na yule mrembo Jeuri, ambaye bado alikuwa anapekua pekua mkoba wake pasipo mafanikio, kondakta akawaomba nauli, yule dada akamtazama Frank kwa macho ya kuomba msaada, kwa yule kijana ambaye muda mfupi uliopita alishindwa kuitikia salamu yake.
“Nimeumbuka leo, sijui lile buku nimetupia wapi?” aliwaza yule binti huku akimtazama Frank ambaye pasipo kumbabaika akaingiza mkono mfukoni mwake na kutoa wallet yake akaifungua, kwa hakika zilionekana noti za elfu kumi kumi zikiwa zimejipanga kweye pochi ya Frank, akaichomoa moja na kumpa yule Kondakta, “Poster Mpya” alisema Frank baada ya kumpatia kondakta ile fedha, “Nikate wawili?” aliuliza yule kondakta baada ya kuona yule msichana pembeni ya Frank akiwa ametulia pasipo kuonesha dalili ya kutoa nauli, Frank akamtazama yule msichana pembeni yake, kwa yule dada ambaye muda mfupi uliopita alizarau salamu yake, sasa alikuwa amemtazama kwa macho yaliyoashilia alikuwa anahitaji msaada wake, huku akiwa ameshikwa na aibu.
Kwanza Frank hakuamini kama yule mdada alikuwa analenga kuomba msaada, maana licha ya nyodo alizozionyesha kwake, pia yule dada alikuwa mzuri sana wa umbo na mwili, tena mavazi yake aliyoyavaa ndiyo yalimfanya Frank akubari kuwa yule dada ni mzuri na umbo lake ni matata, “Oya braza vipi mbona kimya nikate wote?” aliwastua tena kondakta mkorofi, ambaye alikuwa amewasimamia karibu yao, Frank akamtazama tena yule dada na macho yao yakagongana, hapo Frank akashuhudia midomo ya yule dada ikicheza-cheza kama anayesema “Please” lakini pasipo kutoa sauti, huku macho yake yakionesha kila dalili ya kuhitaji ule msaada wa kulipiwa nauli, “Poa kata wawili” alijibu Frank, kama vile hajiamini, maana aliogopa pengine hakumuelewa yule dada hivyo angejikuta akishushiwa mvua ya matusi, lakini ikawa tofauti baada ya kuliona tabasamu mwanana usoni kwa yule dada mrembo wenye zarau, “Ahsante anko” Frank kwa mara ya kwanza aliisikia sauti tamu ya yule binti mrembo, “Ok! Usijali” alijibu kwa kifupi Frank huku akipokea chenji yake toka kwa kondakta.
Safari iliendelea Frank akiendelea kucheza game lake la nyoka, huku akiibia kumtazama yule dada na kuusaminisha uzuri wake, “Kweli huyu dada ni mzuri, yaani daaaah! nikimpata naoa kabisa, sema ananyodo huyooo, halafu anaonekana hataki mazoea ya kijinga” aliwaza Frank akimuona yule dada anatoa simu yake nzuri ya kisasa, tofauti na yake, kisha akamuona akitafuta namba kisha akaipigia, sekunde chache akaanza kuongea kwa hasira, sauti ikiwa ya chini kidogo na uso ameukunja kwa hasira “Lakini Fred mbona umechukuwa hela yangu bila kuniambia,......... hapana bwana, mwenzio ndio nilikuwa naitegemea kufanya nauli, sasa mimi nitapata wapi,......... siyo hivyo bwana yaani mwenzio nusu niaibike,......... yaani kuna Anko mmoja amenisaidia bila hivyo sijui ingekuwaje,.........” kisha yule dada akakata simu huku bado uso ameukunja kwa hasira, baada ya hapo safari iliendelea kimya kimya mpaka Frank alipofika kwenye kituo cha Poster Mpya, nakujiandaa kushuka, “Kumbe umeshafika Anko, poa mimi nashukia hapo mbele” aliongea yule dada mrembo huku akiachia tabasamu, usingezani kuwa ni yule alieshindwa kuitikia salamu yake muda mfupi uliopita, “Poa dada tutaonana” alijibu Frank huku akishuka na kumuacha yule dada akiendelea.
“Daaa! ningejaribu kumuomba namba ya simu, lakini mh! angenishushua pale sijui ingekuwaje?” ni baadae sana Frank akiwa ofisini aliwaza mengi sana juu ya yule mwanamke mrembo, wa kwenye daladala, hakuwa na wa kumsimulia maana ofisini kwake alikuwa mwenyewe tu! zaidi wasaidizi wake ambao walikuwa counter wakiendelea na mauzo, “Sijuwi kama nitamuona tena, ila nikimuona tu! namchana live, kwanini nimuogope” mawazo juu ya yule mwanamke mrembo, yalikisumbua kichwa chake kwa muda wa siku tatu, ndipo yakaanza kufutika mawazo hayo, mpaka inatimia wiki alikuwa ameshasahau nakuona yaliyopita si ndwele.
Ilikuwa Jumamosi siku ambayo huwa wanafanya kazi mpaka saa sita mchana kisha wanafunga ofisi na kurudi makwao mpaka Jumatatu, siku hiyo Frank baada ya kufunga ofisi alionelea awahi nyumbani kucheki movie za kivita huku anapata kinywaji na kinywaji chake kikubwa ni mvinyo wa zabibu kutoka Dodoma, maana ndiyo starehe yake kubwa sana akiwa nyumbani, hata chakula cha mchana akale huko huko mitaa ya Mbezi, alipofika kwenye kituo cha daladala alikuta watu ni wengi sana wakigombania daladala zilizojipanga pale kituoni, hapo akaona mambo magumu, “Daaa! wenye magari yao wanafaidi kweli-kweli” aliwaza Frank.
“We Anko ingia humu nimekuwekea siti” Frank alistuliwa na sauti ya kike toka kwenye moja ya daladala, akatazama ilipookea ile sauti, akamuona yule mrembo mwenye nyodo na chuchu saa sita zilizosimama kama
Whatsapp +255 758 018 597 kupata Full
Email - emanmic@yahoo.com

Post a Comment

0 Comments